RC CHALAMILA: DAR- KUZINDUA BIASHARA SAA 24 FEBRUARI 22,2025

Asema maandalizi ya kufunga taa na Camera za usalama yanendelea vizuri. Mara baada ya jiji la Dar es salaam kufanikiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Nishati wa wakuu wa Nchi za Afrika Mkuu wa Mkoa huo Mhe Albert Chalamila ametangaza rasmi kuanza kwa shughuli za biashara kwenye jiji hilo saa 24 ambapo uzinduzi rasmi utafanyika februari 22 mwaka huu. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo Januari 30,2025 katika ukumbi wa Hotel ya Johari Rotana, RC Chalamila amesema jiji hilo ni muhimu kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi hivyo februari 22 mwaka Mkoa huo utazindua rasmi mpango shughuli za kibiashara kufanyika saa 24, kwa sasa wanaendelea kufunga taa za kutosha na maandalizi ya kufunga kamera yanaendelea vizuri kwa ajili ya usalama. Aidha akizungumzia Mkutano wa Nishati wa wakuu wa Nchi za Afrika RC Chalamila amewashukuru na kuwapongeza wananchi wa Mkoa huo kwa ushirikiano mkubwa walioutoa ikiwemo kuimarisha amani, utulivu na usafi hivvyo ameelekeza wilaya zote kuendelea...