TAMASHA LA SAUTI ZA BUSARA KUTIKISA ZANZIBAR FEB 14 HADI 16
Na Mwandishi wetu
Wasanii kutoka Bara nzima la Afrika wanatarajia kujumuika kwa pamoja kuonesha vipaji vyao katika jukwaa la Tamasha la Sauti za Busara linalotarajiwa kufanyika Februari 14 hadi 16 Ngome Kongwe Zanzibar huku liongozwa na kauli mbiu ya "Voice For Peace".
Akizugumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa tamasha hilo,Journey Ramadhan amesema tamasha hilo litafanyika kwa siku tatu za amani, umoja, ubunifu pamoja na utofauti .
"Tunawaalika wapenzi wa muziki na wafuasi wa amani kutoka pande zote za dunia kuungana katika tamasha hili kwa siku tatu hivyo tamasha la Sauti za Busara 2025 linatarajiwa kuwa tukio lisilosahulika"amesema Ramadhan
Akitaja majina ya wasanii hao ni pamoja Thandiswa(Afrika Kusini), Blinky Bill(Kenya), Christian Bella&Malaika Bendi (Tanzania), Bokani Dyer (Afrika Kusini) Frida Amani (Tanzania) The Zawose Queens,Kasiva Mutual,(Kenya) Zanzibar Taarab Heritage Ensemble(Zanzibar), Leo Mkanyia & Swahili Blues (Tanzania), Boukouru(Rwanda), Tryphon Evarist (Zanzibar), Charles Obina (Uganda) na Baba Kash(Tanzania).
Wengine ni Assa Matusse (Msumbiji), Mumba Yachi(Congo), Nidhal Yahyaoui (Tunisia), Etinsel Maloya (Reunion), WD Abo (Sudan) uKhoiKhoi(Afrika Kusini), Joyce Babatunde (Kamerun).
Vilevile amesema tamasha hilo pia litajumuisha maonesho ya kipekee ya mchana yatakayofanyika Februari 15 katika mji wa Fumba Town mradi ulichini ya CPS Nyamanzi likitoa burudani huku jukwaa la Forodhani likiendelea kusisimua watanzamaji kwa mziki wa moja kwa moja ukitoa hamasa ya Amani, Umoja na fursa ya kusherekea utamaduni wa mwafrika.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Busara Promotions Lorenz Herrmann amesema wamekuwa wakitegeneza ajira zaidi 200 kupitia Tamasha la Sauti ya busara.
Aidha aliwashukuru wadau mbalimbali ambao wamekuwa wakishirikiana na Taasisi hiyo kwa kutumia nguvu ya muziki kuamasisha amani,maelewano pamoja na kuongeza uelewa kuhusu jukumu la kubadilisha jamii kupitia muziki.
Naye Mwakilishi wa wasanii watakaoshiriki katika Tamasha hilo, Leo Mkanyia amesema anafurahi kuwa mmoja washiriki katika tamasha la Sauti ya Busara 2025 huku akiwaalika wapenzi wa muziki kujitokeza na kuungana nao.
Aidha kiingilio hakuna ni bure usafiri hivyo wapenzi wa burudani wanaalikwa kutakuwa na maada mbalimbali zitakazoendeshwa ikiwemo kutokomeza ukatili wa.kijinsia
Comments
Post a Comment