Tanzania kupitia Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), Dkt. Ladislaus Chang’a, amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi, “Intergovernmental Panel on Climate Change (IPCC)”, katika Mkutano wa 59 wa IPCC (IPCC-59) unaoendelea katika Ofisi za Umoja wa Mataifa Jijini Nairobi, Kenya kuanzia tarehe 25 hadi 28 Julai, 2023. Dkt. Chang’a amechaguliwa katika nafasi hiyo katika uchaguzi wa viongozi wa IPCC (IPCC Bureau) uliofanyika tarehe 26 Julai, 2023. Wagombea katika nafasi ya Makamu wa Mwenyekiti wa IPCC walikuwa jumla nane, kutoka Tanzania, Australia, Cuba, Eswatini, Germany, Hungary, Urusi na Afrika Kusini. Katika kinyang’anyiro hicho zilihitajika nafasi tatu na waliochaguliwa ni Tanzania, Cuba na Hungary. Aidha, Dk. Chang’a kwa kushirikiana na Maafisa wengine wa ngazi ya juu wa IPCC waliochaguliwa katika Mkuta...