SUZA YAJA KIVINGINE "SOMA UJIAJIRI"


Na Mwandishi wetu HPMedia, Dar 

Wazazi na walezi wameshauriwa kuwapeleka vijana wao katika chuo cha Taifa, (SUZA) ili waweze kujipatia elimu bora pamoja na maarifa yatakayo wawezesha kujiajiri wenyewe pindi wanapomaliza chuoni hapo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo July 18, Mkuu wa idara ya ujasiriamali wa chuo hicho, Dkt Moh'd Salim Ahmed wakati  walipotembelewa katika banda lao kwenye maonesho ya 18 ya elimu ya juu Sayansi na Teknolojia yanayoendelea katika viwanja vya mnazi mmoja yalioanza July 17 mwaka huu amesema kuwa kozi hiyo ni mpya chuoni hapo.

Amesema kuwa,  katika chuo hicho wameongeza kozi mbili ikiwa ni pamoja na somo la ujasiriamali ambapo mpaka sasa wanafunzi wake wamekua wakifanya vizuri kwa  vitendo ikiwemo kutengeneza bidhaa mbalimbali kwa kutumia mimea, ambapo kwa mwaka huu wanafunzi 19 watahitimu.

"Hii kozi ni mpya lakini mpaka sasa tumeona matokeo mazuri kwa wanafunzi kwani wameweza kutengeneza vipodozi mbalimbali  kama vile lotion, Lipstic, mafuta pamona na viungo vya kupikia" amesema Dkt Moh'd.

Amesema kuwa, kupitia kozi hiyo wanafunzi huwagawa  magrupu ya kuanzia watu watano, hivyo wanaunda kampuni yao na wanafanya shughuli zao baadae huzisajili ili kwenda sokoni kwa ajili ya kununuliwa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo Cha Mahusiano na Masoko wa Chuo hicho, Khadija Maumba amesema kuwa, chuo hicho  kimeongeza kozi mbili ikiwemo ya shahada ya awali ya sayansi ya maabara pamoja na shahada  uzamili ya uendeshaji wa biashara na fedha ikiwa ni jitihada za chuo hicho kuhakikisha wanatoa elimu bora.

Amesema kuwa, Chuo hicho kina Shahada ya Ujasiriamali na Ubunifu ambayo imekuwa msaada mkubwa kwa wahitimu wake kuanzisha biashara na kujitegemea kwa kujiajiri na si kuajiriwa pekee hivyo amewashauri wazazi na walezi watembelee banda lao kujionea mazuri ya chuo hicho.

Hata hivyo, amesema chuo hicho kimejikita kwenye fani nyingi fofauti, ambapo wanatoa fani Afya, utalii, kilimo, ujasiriaamali, biashara, teknolojia ya habari (IT),Tehama lakini pia wanafani ya sayansi ya kompyuta.

Aidha, amesema kuhusu masomo ya kiswahili bado wanaendelea kutoa elimu ya shahada ya uzamili ya kiswahili kwa watumiaji wa lugha nyingine ambayo huwaandaa wanafunzi kwa ajili ya kuwa walimu wa kiswahili kwa watumiaji wa lugha nyingine na chuo hicho pia kimebobea katika ufundishaji wa kiswahili kwa wageni kwani kina wataalam wa masomo hayo.

Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI