ACT YATOA HOJA 7 KWA SERIKALI
Na Magrethy Katengu,HPMedia,Dar Chama cha ACT Wazalendo kimetoa hoja 7 mara baada ya hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu mapitio ya kazi na mwelekeo wa serikali na makadirio ya matumizi kwa mwaka wa fedha 2023/2024 hoja ikiwemo hali ngumu ya maisha,suala la ukosefu wa ajira,kukosekana kwa utaratibu wa kukabiliana na maafa ,kuchelewa kwa Miradi ya kimkakati. Hoja hizo saba zimetolewa leo Jijini Dar es saalam Waziri Mkuu kivuli chama cha ACT Wazalendo Dorothy Semu wakati akichambua Hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu mapitio ya kazi na mwelekeo wa serikali makadirio ya matumizi kwa mwaka wa fedha 2023/2024 iliyowasilishwa Aprili 05 2023 Bungeni na Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa ambapo amesema Serikali iliyo chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan inahitaji Mabadiliko makubwa ya kiuchumi hivyo wametoa hoja zao zifanyiwe kazi. Dorothy akifafanua hoja ya hali ngumu ya maisha amesema kutokana na Mabadiliko ya hali ya hewa serikali iangalie na namna ya kununua chakula cha kutosha angalau m