Posts

Showing posts from May, 2024

BONGO MOVIE WAFUNGUKA RAIS DKT SAMIA KUWAPELEKA NJE YA NCHI KUJIFUNZA

Image
  Na Mwandishi wetu,HabariPlus, Dar Wasanii wa Filamu za maigizo (BONGO MOVIE) wamempongeza Rais Dkt Samia Suluh Hassan kwa kuwajumuisha kwenye ziara yake ya nje ya nchi kwa ajili ya kujifunza jambo ambalo litafungua fursa mbalimbali kwa wasanii hao. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Taasisi ya Ongea na Mwanao Steve Nyerere amesema kuwa jambo analolifanya Rais Dkt Samia ni mfano wa kuigwa kwani anatambua mchango wa kila  sekta nchini. Amesema kuwa, wao kama wasanii watahakikisha wanaitumia fursa hiyo katika kujifunza, kulinda maadili na kuitangaza Tanzania vizuri kiutamaduni na kiutalii jambo ambalo litaivuta Dunia kuifahamu vyema Tanzania. Hata hivyo Nyerere amewatahadharisha wanasiasa kuwa wasije kusema kwamba jambo analolifanya Rais Samia kuwa ni kampeni kuelekea uchaguzi Mkuu kupitia kwa wasanii. Amesema kuwa, Rais Samia anafanya hivyo kama mzazi anayepaswa kuwakumbatia watoto wake wote, ambapo ameleza kitendo cha Wasanii kupelekwa nje kujifunza

RAIS DKT SAMIA KESHO KUTUA KOREA, MIKATABA SABA KUSAINIWA

Image
  Na Mwandishi wetu, HabariPlus Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kesho anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi ya siku sita nchini korea yenye lengo la kukuza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili. anaenda kufanya  Ziara ya kikazi.  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Waziri wa Mambo ya Nje January Makamba amesema kuwa pamoja na mambo mengine pia atasaini mikataba saba na Rais wa nchi ya korea yenye lengo la ushirikiano kati ya nchi hizo mbili. "Miongoni mwa mikataba  hiyo ni pamoja na mikataba  hati ya makubaliano kati ya Taasisi ya madini Tanzania na Taasisi ya miamba nchini korea, huu ni ushirikiano unahusu utafiti, uchoraji ramani, rasilimali na uchoraji  wa maabara"amesema Waziri Makamba. Ameongeza"mkataba wa pili ambao unaenda kusainiwa ni ushirikiano wa uchumi wa bluu, huku mkataba wa tatu ukihusu kwenda kutambua vyeti vya mabaharia  na tutaweza kusaini tamko la pamoja kuhusu siasa  na makubaliano ya hati ya madini, vi

TRA YATAMBUA NGUVU DIGITAL PLATFORM

Image
Na Mwandishi wetu, HabariPlus, Dar Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA leo imekutana na Jukwaa la wanahabari wa Mtandaoni (JUMIKITA) kwa lengo la kuwajengea uwezo kuhusu namna ya utoaji wa elimu ya mlipa kodi. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mapema leo hii Kaimu Mkurugenzi wa TRA Hudson Kamoga wakati akifungua mafunzo ya siku moja yalioandaliwa na malaka hiyo, amesema TRA imedhamiria kutoa elimu kwa watanzania wote ili waweze kulipa kodi kwa hiari . Amesema kuwa, Serikali ya awamu ya sita imekua na utaratibu maalum wa kutoa elimu ya mlipa kodi kwa wananchi ili kila mtu atakaponunua bidhaa aweze kudai risiti. "TRA imekua na utaratibu wa kufuata kodi kwa wafanyabiasha na kutoa elimu ili waweze kulipa kodi bila shuruti, pia tumekua tukifanya ziara ya mlango kwa mlango kwa ajili ya kuskiliza mteja kama anadai risiti na wanafanyabiashara wanatoa risiti hizo" amesema Kamoga. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mwenyekiti wa Jukwaa la waandishi wa habari za Mtandaoni,

MGOGORO WA MIPAKA PORI LA AKIBA LIPARAMBA WATATULIWA, WANANCHI WAISHUKURU SERIKALI

Image
Na Beatus Maganja  Jitahidi za Serikali za kutatua migogoro ya matumizi ya ardhi baina ya Hifadhi na wananchi zinaendelea kuzaa matunda baada ya kutatua mgogoro uliodumu zaidi ya miaka 20 baina ya Pori la Akiba Liparamba lililopo Mkoani Ruvuma na vijiji vitano vinavyozunguka hifadhi hiyo. Hayo yamebainika Mei 28, 2024 katika ziara ya kuelezea namna TAWA ilivyotekeleza kikamilifu maagizo ya Serikali na mapendekezo ya Baraza La Mawaziri la Kisekta (BLM) kuhusiana na utatuzi wa mgogoro huo. Akizungumzia mgogoro huo,  Kamanda wa Hifadhi hiyo Annzikar Joseph Lyimo amesema Pori la Akiba Liparamba lilikuwa na mgogoro wa mipaka kati yake na vijiji vinavyolizunguka ambavyo ni Ndondo, Mseto, Mipotopoto, Liparamba na Mitomoni. Mgogoro unaotajwa kudumu zaidi ya miaka 20 lakini ulitatuliwa Mwaka 2023 ikiwa ni matokeo ya  ziara ya Mawaziri wa Wizara nane wa kisekta ya kutembelea maeneo yenye migogoro ya matumizi ya Ardhi likiwemo Pori hilo ambapo walitoa maelekezo ya kupitia upya kwa mipaka na hatim

TMA YATOA MWELEKEO WA HALIBYA HEWA KWA KIPINDI CHA JUNI - AGOSTI, 2024

Image

"MIMI MWENYE NYUMBA WAKO APA MBONA SIKU ZINAZIDI?" 12 WAFIKISHWA MAHAKAMANI, WAKABILIWA MASHTAKA 32.

Image
Na. Jeshi la Polisi, Dar es Salaam, Mei 28, 2024 MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewapandisha kizimbani wakazi 12 wa Ifakara, Morogoro akiwemo Barnaba Gidajuri (45) wakikabiliwa na mashtaka ya kuongoza genge la uhalifu na kujipatia pesa shilingi millioni 10 kwa njia ya udanganyifu. Jana Mei 27, 2024 wakiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo Ushindi Swalo, Wakili wa Serikali Tumaini Mafuru alidai watuhumiwa hao wanakabiliwa na mashtaka thelathini na mbili.  Wakili Mafuru alidai mashtaka hayo ni kuongoza genge la uhalifu waliofanya Januari mosi hadi Mei 5, 2024, ambapo walituma  jumbe fupi kwa watu kisha kujipatia kiasi cha Sh millioni 10. Aidha Wakili Mafuru alidai mashtaka ya pili na ya tatu yanayomkabili mtuhumiwa Barnaba Gidajuri  ilitotenda Januari 4, mwaka huu akisambaza jumbe fupi kwa njia ya mtandao wenye maneno "Mzee huyu Mganga wa tiba asili anatoka mali bila kafara, cheo, mapenzi......".."jiunge na chama huru cha freemason (666) Tanzania bila kutoa kaf

USIKOSE KUFUATILIA UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO

Image
 Wananchi wameshauriwa kuendelea kufuatilia utabiri wa hali ya hewa na kuchukua tahadhari

TANZANIA MWENYEJI WA MAADHIMISHO YA MIAKA 20 YA BARAZA LA AMANI NA USALAMA LA UMOJA WA AFRIKA

Image
Na Mwansdishi wetu,HabariPlus RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuongoza maadhimisho ya miaka 20 ya baraza la amani na usalama la umoja wa Afrika yatakayofanyika Mei 25, katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki January Makamba amesema kuwa ni heshima kubwa Tanzania kuwa mwenyeji wa maadhimisho hayo ambapo wageni 120 wanatarajiwa kuhudhuria kutoka nchi mbalimbali. Amesema kuwa, Tanzania kuongoza maadhimisho hayo ni heshima kubwa kwani ni nchi 15 tu kati ya nchi 55 ambazo ni wanachama wa Umoja wa Afrika, ndio wajumbe wanaounda baraza la amani na usalama la umoja wa Afrika. "Nchi ambazo zina wajumbe wa baraza hilo ni Tanzania, Uganda na Djibouti (kutoka Ukanda wa Mashariki), Cameroon, DRC na Equatorial Guinea (Kanda ya Kati), Afrika Kusini, Angola na Botswana (Kanda ya Kusini), Cote d’Ivoire, Gambia, Nigeria na S

WAZIRI MAJALIWA ATOA AGIZO HILI KWA MAMLAKA ZINAZOSIMAMIA SEKTA YA HABARI

Image
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezitaka mamlaka zinazohusika na usimamizi wa sekta ya habari ziendelee kusimamia vyombo vya habari vizingatie maadili na kujiepusha na uchapishaji wa taarifa na picha zinazochochea uvunjaji wa maadili, mila na desturi za Kitanzania. Pia, Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa habari za mitandao ya kijamii na vyombo vya habari ili kuhakikisha kuwa sekta hiyo inaendelea kukua na kuchangia kuleta maendeleo kwa Taifa. “Kupitia vyombo vya habari, hasa vya mitandao ya kijamii, tumeweza kuwahabarisha wananchi kuhusu shughuli na mipango ya Serikali, na kuhamasisha ushiriki na ushirikishwaji wa wananchi katika shughuli na mipango hiyo.”   Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Mei 21, 2024) katika Kongamano la Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandaoni ya Kijamii (JUMIKITA) kuhusu mafanikio ya miaka mitatu ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwenye Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam. Ameongeza kuwa Serikali imechukua hatua mbali

HARMONIZE AMPA "ZAWADI" RAIS DKT SAMIA

Image
  Na Mwandishi wetu, HabariPlus, Dar MSANII wa Bongo Fleva ambae amekua akifanya vizuri katika muziki wa kizazi kipya hapa nchini,  Harmonize anatarajia kuzindua albam yake ya tano Mei 25, 2024, Jijini Dar es Salaam. Staa huyo wa muziki wa kizazi kipya amebainisha hayo jana Mei 20 mwaka huu wakati akizungumza na waandishi wa habari na kufafanua kuwa albamu hiyo imebatizwa jina la Mziki wa Samia. Albamu hiyo imebeba nyimbo 10 za nguvu ambazo zinatangaza mambo mazuri ambayo yamefanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha uongozi wake. Mei 25, itakua ni usiku maalum kwa ajili ya watu kuburudika, hakutakya na kiingilio ispokua ni mialiko maalum kwa wageni kuweza kuhudhuria katika hafla hiyo. Lengo la uzinduzi wa albamu hiyo ni kupongeza na kuunga mkono kazi nzuri inayoendelea kufanywa na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Uongozi wake. Aidha, album hiyo itakua ya mwisho kwake na kusisitiza kuwa ameimba sana kuliko kawaida naame

SERIKALI KUKUZA BUNIFU, COSTECH YAJIVUNIA

Image
  Na Mwandishi wetu, HabariPlus,Dar Serikali imesema itaendelea kusapoti bunifu zote zinazofanywa na watu mbalimbali, huku ikiahidi kukuza sayansi kwa lengo la kuchagiza maendeleo chini Tanzania. Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Sayansi na Teknolojia kutoka Wizara ya elimu sayansi na Teknolojia Profesa Ladslaus Mnyone wakati akimuwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Nombo katika mdahalo maalum uliowakutanisha wahariri, waandishi wa habari na wadau wa ubunifu, ulioandaliwa na Tume ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (COSTECH) chini ya programu ya ufunguo. Amesema kuwa, pia Serikali itahakikisha inakuza sayansi, teknolojia na ubunifu, lengo ikiwa kusaidia kufanyika kwa tafiti zinazojibu changamoto za watanzania, katika kuhakikisha sekta ya teknolojia na ubunifu inakua huku ikikamilisha mkakati wa teknolojia ya TEHAMA Kwa upande wake,  Mkurugenzi wa COSTECH Dk.Amos Nungu, amesema wiki ya ubunifu, costech na wadau wa maendeleo wanajivunia mambo

KIMBUKA "IALY" KIPO KM 500 MASHARIKI MWA PWANI YA DAR

Image
  Dar es Salaam,  Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa kuhusu mwenendo wa kimbunga “IALY” katika Bahari ya Hindi, Kimbunga hicho kwa sasa kipo katika eneo la takriban kilomita 500 mashariki mwa pwani ya Dar es salaam. Mifumo ya hali ya hewa inaonesha kuwa kimbunga “IALY” kinapungua nguvu yake huku kikielekea kaskazini, mbali na pwani ya nchi yetu na kinatarajiwa kuisha nguvu yake kabisa usiku wa kuamkia keshokutwa Jumatano tarehe 22 Mei 2024. Hata hivyo, kutokana na umbali kilipo kutoka nchini, vipindi vya upepo mkali vimeanza kujitokeza katika maeneo ya ukanda wa pwani kama ilivyotabiriwa. Kwa mfano vituo vya hali ya hewa vilivyopo Unguja, Pemba na Mtwara vimeweza kuripoti upepo unaofika kilomita 50 kwa saa katika siku ya leo. Matarajio ni kwamba, vipindi vya upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa saa na mawimbimakubwa yanayozidi mita 2 vitaendelea kujitokeza katika maeneo ya ukanda wa pwani ya nchi yetu na katika Bahari ya Hindi kati ya leo tarehe 20 Mei 2024

KIMBUNGA “IALY” KINAENDELEA KUIMARIKA

Image
  Dar es Salaam, 19 Mei 2024 Kufuatia taarifa iliyotolewa tarehe 17 Mei 2024 na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuhusu kuwepo kwa kimbunga “IALY” katika Bahari ya Hindi kaskazini mwa kisiwa cha Madagascar, Mamlaka inapenda kutoa mrejeo kuhusiana na mwendendo wa kimbunga hicho. Mifumo ya hali ya hewa inaonesha kuwa kimbunga hicho kimeendelea kuimarika na bado kimeendelea kusalia katika Bahari ya Hindi kama ilivyotabiriwa awali, hadi ilipofika saa 3 asubuhi ya leo kilikuwa umbali wa takriban kilomita 680 mashariki mwa pwani ya nchi yetu. Kutokana na umbali huo kutoka nchini, vipindi vya upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa saana mawimbi makubwa yanayozidi mita 2 vinaweza kujitokeza katika Bahari ya Hindi hususan kati ya leo tarehe 19 Mei 2024 na Jumanne tarehe 21 Mei 2024. Vilevile, vipindi vya mvua vinaweza kujitokeza katika maeneo ya ukanda wa pwani hususan kati ya tarehe 21 na tarehe 22 Mei 2024. USHAURI: Watumiaji wa bahari na wananchi wa maeneo ya ukanda wa pwani wanashauriwa

HARMONIZE KUZINDUA ALBAM YA "MZIKI WA SAMIA"

Image
Na Mwandishi wetu, HabariPlus,Dar Msanii wa bongo fleva ambae amekua akifanya vizuri katika sanaa Harmonize anatarajia kuzindua albam yake ya tano Mei 25, 2024 katika ukumbi wa Mlimani Cty ambayo inakwenda kwa jina "mziki wa Samia". Albamu hiyo imebeba nyimbo 10 za nguvu ambazo zinatangaza mambo mazuri ambayo yamefanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha uongozi wake. Mei 25, itakua ni usiku maalum kwa ajili ya watu kuburudika, hakutakya na kiingilio ispokua ni mialiko maalum kwa wageni kuweza kuhudhuria katika hafla hiyo. Lengo la uzinduzi wa albamu hiyo ni kupongeza na kuunga mkono kazi nzuri inayoendelea kufanywa na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Uongozi wake. Aidha, album hiyo itakua ya mwisho kwake na kusisitiza kuwa ameimba sana kuliko kawaida na ametengezeneza nyimbo 10 ambazo zote zinamlenga Rais Samia hivyo baada ya album hiyo atapumzika na kurefresh huku akiwa anaachia wimbo mmojammoja na sio album

MEYA WA JIJI LA DAR ATUMA SALAMU KWA MWARI KIGEGO

Image
Na mwandishi wetu, HabariPlus, Dar Diwani wa Kata ya Vingunguti ambae pia ni Meya wa jiji la Dar es Salaam Omar Kumbilamoto ametuma salamu kwa watu wanaomchafua kuwa hakuna maendeleo yoyote anayoyafanya katika kata hiyo na badala yake ana mpango wa kuuza shule na Zahanati kwa mwekezaji. Salamu hizo amezitoa jijini Dar es Salaam wakati alipokua akizungumza na wachama wa  umoja wa wanawake (UWT) Kata ya Vingunguti na wananchi katika mkutano maalum wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa Serikali za mitaa wa mwaka huu. Amesema kuwa, kuna baadhi ya watu ambao hawana nia njema na Kata wamekua wakisambaza taarifa za uongo hivyo amesema maendeleo yaliofanywa na Rais Dkt Samia katika hiyo ni makubwa kwani amegusa sekta zote kwenye maendeleo. "Nimekua nikisimamia miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata hii ikiwemo sekta ya elimu kama vile ujenzi wa shule, madawati, pamoja na miundombinu ikiwemo barabara na maji na hivi sasa kuna barabara 3 ambazo zimeingia katika mpango wa ujenzi wa lami&