MEYA WA JIJI LA DAR ATUMA SALAMU KWA MWARI KIGEGO


Na mwandishi wetu, HabariPlus, Dar

Diwani wa Kata ya Vingunguti ambae pia ni Meya wa jiji la Dar es Salaam Omar Kumbilamoto ametuma salamu kwa watu wanaomchafua kuwa hakuna maendeleo yoyote anayoyafanya katika kata hiyo na badala yake ana mpango wa kuuza shule na Zahanati kwa mwekezaji.

Salamu hizo amezitoa jijini Dar es Salaam wakati alipokua akizungumza na wachama wa  umoja wa wanawake (UWT) Kata ya Vingunguti na wananchi katika mkutano maalum wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa Serikali za mitaa wa mwaka huu.

Amesema kuwa, kuna baadhi ya watu ambao hawana nia njema na Kata wamekua wakisambaza taarifa za uongo hivyo amesema maendeleo yaliofanywa na Rais Dkt Samia katika hiyo ni makubwa kwani amegusa sekta zote kwenye maendeleo.

"Nimekua nikisimamia miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata hii ikiwemo sekta ya elimu kama vile ujenzi wa shule, madawati, pamoja na miundombinu ikiwemo barabara na maji na hivi sasa kuna barabara 3 ambazo zimeingia katika mpango wa ujenzi wa lami"amesema Kumbilamoto.

Ameongeza"Nataka nimtumie salamu huyu mwari kigego ambae anapita akisambaza taarifa za uongo Zahanat na Shule ni mali ya Serikali nauza mimi kama nani, Ccm ndio chama pekee ambacho kimeleta maendeleo kabla ya uongozi huu uliopita ulitoka ukanda wa gaza walifanya nini cha maana katika Kata hii"amesema 

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Kata ya Vingunguti, Sharifa Mwendo amewataka wanawake wa kata hiyo kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa Serikali ya mtaa huku akiwapigia kampeni viongozi waliopo madarakani .

"Viongozi waliopo sasa hivi wanatosha kuanzia Diwani, Mbunge na Rais kwani wametumia madaraka yao vizuri kwa kuletea  maendeleo makubwa katika sekta zote, nitawashangaa nikimuona mtu anachukua fomu ya nafasi ya udiwani, ubunge na Urais"amesema Mwendo.




Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI