Posts

Showing posts from April, 2024

TAWA YAPOKEA MELI YA WATALII ZAIDI YA 200 KILWA KISIWANI

Image
Na Beatus Maganja  Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA leo Aprili 24, 2024 imepokea meli  ya watalii wapatao 230 kutoka Mataifa mbalimbali Duniani  waliofika katika Hifadhi ya Urithi wa utamaduni wa Dunia ya Magofu ya Kilwa kisiwani na Songo Mnara kwa ajili ya shughuli za utalii. Meli ijulikanayo kwa jina la "Silver Clouds" ndiyo iliyotia nanga katika Hifadhi hiyo ikiwa imebeba watalii kutoka Mataifa ya Australia, Ubeligiji, Brazil, Canada, Chile, China, Ujerumani, Ireland na Norway huku watalii wengine wakitokea Mataifa ya Italia, Ureno, Africa ya Kusini, Hispania, Sweden, Switzerland, Ukraine, Uingereza na Marekani. Huu ni mwendelezo wa safari za watalii kutoka kona mbalimbali za Dunia kuja kujionea fahari ya urithi wa Dunia wa utamaduni, historia na malikale uliopo katika Hifadhi hiyo inayosimamiwa na TAWA. Ikumbukwe kuwa Hifadhi hii imekuwa ikipata wageni wengi wa ndani na nje ya nchi yetu ambapo hivi karibuni (Februari, 2024) Hifadhi hiyo ilipokea zaidi y

TAKUKURU KINONDONI YAPOKEA MALALAMIKO 84, YABAINI MAPUNGUFU MIRADI 6

Image
Na Mwandishi wetu, Habari Plus, Dar Mamlaka ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imebaini mapungufu kwenye miradi 6 ya maendeleo yenye thamani ya bill 61.910.746.284.42 ambapo wameahidi kuifuatilia kwa ukaribu zaidi miradi hiyo ili ikamilike kwa viwango vinavyoendana na thamani ya fedha iliyotolewa. Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kinondoni Elizabeth Mokiwa wakati alipokuwa akitoa taarifa ya kipindi cha miezi mitatu kuanzia January hadi March 2024 ambapo imekua  na utaratibu wa kutoa taarifa ya utendaji kazi kila baada ya miezi 3. Amesema kuwa, miongoni mwa miradi walioifuatilia ni pamoja na ujenzi wa uwanja wa michezo Mwenge wenye thamani ya shill 4.065.100.285.23 ambapo umekamilika kwa asilimia 92  huku ikibaki ubandikaji wa kapeti ya nyasi. "Mradi huu unakaribia kukamilika April 21 2024 kwa mujibu wa makubaliano mkataba, ufuatiliaji wa karibu unaendelea kuhakikisha mradi unakamilika kwa ubora na kuzingatia thamani ya fedha"

JESHI LA POLISI LAKANUSHA TAARIFA ZA KIFO CHA BABU G, FAMILIA YAFUNGUKA

Image
Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam  SACP Jumanne Muliro akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusiana na kifo cha Robart Mushi (Babu G) Gunda Asheri shemeji wa marehemu Babu G akizungumza na waandishi kuhusu kifo cha shemeji yake na kudai taarifa zilizosambazwa na Malisa G na Boniface Jacob wao kama familia hawahusiki nazo. **************--- Na Mwandishi wetu, HabariPlus,Dar Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limekanusha taarifa ya uongo na uzushi inayosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusiana na kifo cha Robart Mushi maarufu kama Babu G. ambaye picha yake imeambatanishwa kwenye taarifa hizo kuwa alipotea Aprili 11, 2024 na baadae kugundulika katika Chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Polisi Kilwa Road huku ikidaiwa Polisi kuhusika na kifo hicho. Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 23, 2024 jijini Dar es Salaam Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Muliro Jumanne Muliro amesema kuwa mtu huyo alifariki baada ya

JESHI LA POLISI LACHUNGUZA MAUWAJI YA WATU WAWILI DAR

Image
  Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linachunguza tukio la mauaji ya watu wawili, Japhari Mwinyimvua (40) mlinzi  na Richard Nonyo (65) baba mzazi wa mtu anayedaiwa ni mganga wa kienyeji wa eneo hilo. Tukio hilo limetokea Aprili 21, 2024 majira  ya saa 3 asubuhi maeneo ya Kigogo fresh, Pugu, Ilala ambapo mlinzi huyo alikutwa ameshambuliwa na baadae kupoteza maisha. Hata hivyo katika mtiririko huo kundi la watu lilimshambulia baba mzazi wa mganga huyo na baadae akapoteza maisha wakimtuhumu mtoto wake kuhusika na kifo cha mlinzi huyo. Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam wanachunguza  kwa kasi tukio hilo na wahusika wote wa tukio hili watakamatwa haraka iwezekanavyo  na kufikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria . Katika hatua nyingne, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata Furaha Dominick Jacobo (32) mkazi wa Masaki na Mustafa Kihenga (28) mkazi wa Mwenge TRA kwa tuhuma za  uhalifu wa kimtandao kwa kusambaza picha chafu za video za watu zisi

DCEA YAKAMATA KILO 767.2 ZA DAWA ZA KULEVYA KATIKA OPARESHENI MAALUM, 21 MBARONI

Image
Magunia ya dawa za kulevya yaliokamatwa na DCEA yakiwa yamefichwa chooni eneo la Zinga Bagamoyo Mkoani Pwani.  Kilo 1.49 ya Dawa za kulevya aina ya skanka zilizokamatwa eneo la Wailes Temeke jijini Dar es Salaam. Nyumba zilizokamatwa kilo 424.84 za dawa za kulevya aina ya Methamphetamine eneo la Zinga Bagamoyo. Picha mbalimbali jumla ya kilo 353.52 za dawa za kulevya zilizokamatwa kata ya Kunduchi Jijini Dar es Salaam. KAMISHNA JENERALI wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya Aretas Lyimo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam. ******************* Na Mwandishi wetu HabariPlus, Dar. Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imefanya operesheni na kufanikiwa kukamata jumla ya kilo 767.2 za dawa za kulevya katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Tanga katika kipindi cha wiki mbili kuanzia Aprili 4 hadi 18, 2024. Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo, ametangaza mafanikio hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 2

USIKOSE KUFUATILIA UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO

Image
 

TANZANIA YACHAGULIWA MAKAMU WA RAIS WA TUME YA SHIRIKIA LA HALI YA HEWA DUNIANI

Image
  Geneva, Uswisi: Tarehe 18/04/2024 Tanzania kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) inayosimamia uangazi, miundombinu na mifumo ya taarifa za hali ya hewa (WMO Commission for Observation, Infrastructure and Systems - INFCOM). Katika uchaguzi huo Tanzania iliwakilishwa na Mkurugenzi wa Miundombinu na Huduma za Ufundi, TMA, , Dkt. Pascal Waniha.  Dkt. Waniha amechaguliwa katika nafasi hiyo  tarehe 18 Aprili, 2024 katika uchaguzi wa viongozi wa Tume ya INFCOM uliofanyika katika Mkutano wa tatu wa Tume hiyo (Third Session of the WMO Commission for Observation, Infrastructure and Systems- INFCOM-3)”, unaoendelea katika makao makuu ya WMO, Geneva- Uswisi tarehe 15 hadi 19 Aprili, 2024. Uchaguzi wa Tume ya INFCOM umefanyika kufuatia muda wa viongozi waliokuwa madarakani kumaliza muda wao ambapo viongozi hao walichanguliwa mwaka 2021 na  waliongoza Tume ya INFCOM katika kipindi cha miaka minne (2020/21 –

USIKOSE KUFUATILIA UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO, LEO APRIL 19,2024

Image
 

TAWA YAFANYA MSAKO WA MAMBA TISHIO KWA MAISHA YA BINADAMU RUFIJI

Image
Katika kuhakikisha usalama wa maisha ya watu  wilayani Rufiji, Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA imefanya msako wa mamba  wanaotajwa kutishia maisha ya watu kutokana na kusogea karibu na makazi ya watu kufuatia kusafirishwa na mikondo ya maji yaliyosababishwa na mafuriko. Afisa habari wa TAWA Beatus Maganja akizungumza na waandishi wa habari katika mji mdogo wa utete wilayani Rufiji leo Aprili 18, 2024 amesema TAWA inaendelea na msako wa mamba tishio kwa maisha ya watu wilayani humo lengo likiwa ni kulinda  usalama wa wananchi wa wilaya hiyo.  " Ni wajibu wetu kuimarisha ulinzi ili yasitokee maafa ya binadamu kupotea kutokana na  kuliwa na mamba wakati  sisi tuko hapa" amesema Afisa habari huyo. "Na ndiyo maana tumekuja hapa kuhakikisha tunawasaka mamba wote ambao ni tishio kwa maisha ya binadamu. Aidha Maganja amesisitiza kuwa Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori Sura ya Na. 283 inaelekeza kuwadhibiti wanyamapori wakali na waharibifu endapo itaonekana wan

ACB BENKI YAZINDUA KADI YA VISA

Image
  Na Mwandishi wetu Benki ya Akiba (ACB) imezindua rasmi huduma ya kadi za VISA ambazo ni mahususi kwa kufanya huduma za miala ya kifedha  ambapo inauwezo wa kutumika sehemu yoyote Duniani. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo wa ACB VISA, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo ,Silvest Arumasi amesema kwamba Benki ya ACB inafanya maboresho makubwa ya huduma za kifedha kwa wateja wake ili kuendana na mahitaji  ya soko. Aidha amesema kwamba maboreshao hayo yatasaidia  kukidhi matarajio ya wateja ambapo hivi sasa huduma nyingi za kibenki zinatolewa kidigitali nakusaidia wateja kupata huduma kwa haraka na rahisi zaidi. "Huduma za ACB VISA CARD zinamrahisishia mteja kufanya miamala mbalimbali kidigitali mfano ;  kutoa pesa kwenye ATM mbalimbali za VISA popote Duniani, na kufanya manunuzi mtandaoni, kufanya malipo kwenye vituo vya mafuta, kwenye migahawa na kwenye maduka makubwa ( Shopping malls & supermarkets) na nyingine nyingi" amesema Silvest Bw. Silvest amewashukuru wateja wote

TAWA YATOA MISAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO RUFIJI

Image
Na. Beatus Maganja Wananchi walioathiriwa na mafuriko  wilayani Rufiji wameiona thamani na umuhimu wa uwepo wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA baada ya leo  Aprili 16, 2024 kupokea misaada mbalimbali kutoka kwa taasisi hiyo  yenye thamani ya shillingi millioni 20 ikiwemo tani 6.4 za unga wa sembe, Kilo 666 za maharage na magodoro 186. Kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi wa TAWA akimkabidhi misaada hiyo  Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakari Kunenge, Kamishna Msaidizi mwandamizi Abraham Jullu amesema TAWA imeguswa na janga la mafuriko lililowapata majirani na wadau namba moja wa uhifadhi wananchi wa Rufiji ambao wamehusika kwa kiasi kikubwa kulinda rasilimali za Hifadhi ya Selous na hivyo imelazimika kuwashika mkono. Jullu amesema tangu changamoto hii ya mafuriko imejitokeza TAWA ilifika kwa haraka na kuongeza nguvu kwa kutoa kikosi cha Askari 24  ili kusaidia katika zoezi la uokozi ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya mbinu za kujikinga na madhara yatokanayo na wanyamapor

TAWA YAWEKA KAMBI RUFIJI, ELIMU YA KUEPUKA MADHARA YA MAMBA NA VIBOKO YATOLEWA

Image
Na. Beatus Maganja Timu ya Maofisa uelimishaji kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA imeweka kambi maalumu wilayani Rufiji yenye lengo la kutoa elimu ya namna ya kuepuka madhara yatokanayo na mamba na viboko kwa wananchi walioathiriwa na mafuriko wilayani humo. Hayo yamesemwa leo na Afisa habari wa TAWA Beatus Maganja alipokuwa akiongea na waandishi wa habari wilayani humo. "TAWA tumeweka Kambi katika wilaya ya Rufiji kufuatia mafuriko yaliyojitokeza katika wilaya hii yaliyoathiri watanzania wenzetu" amesema "Jambo lililotuleta hapa, kwanza ni kutoa pole kwa watanzania wenzetu ambao wamekumbwa na mafuriko haya, lakini pia tumekuja mahsusi kwa ajili  ya kutoa elimu ya namna  wananchi hawa wanaweza kuchukua tahadhari kwa madhara yanayoweza kutokea kutokana na wanyamapori wakali na waharibifu kama vile mamba na viboko" ameongeza Maganja Afisa uelimishaji kutoka TAWA Kanda ya Kusini Mashariki Jimmy Mshana amesema TAWA ilianza kutoa elimu hiyo katika

JUMIKITA YAALANI VIKALI WANAOTUMIA MITANDAO YA KIJAMII VIBAYA

Image
  Na mwandishi wetu, HabariPlus, Dar Mwenyekiti wa Jukwaa la wanahabari wa Mtandao wa kijamii Tanzania (JUMIKITA ) Shabani Matwebe amelaani vikali vitendo vinavyofanywa na baadhi ya watu kutumia mitandao ya kijamii vibaya kwa kutoa lugha za matusi ambazo zimelenga kumdhalilisha mwanamke.  Akizungumza na waandishi wa habari  Jijini Dar es salaam Matwebe amesema kumekuwepo na tabia kwa baadhibya watu kutumia mitandao hiyo vibaya kujadili matusi badala ya kujadili mambo ya maendeleo, huku tabia hiyo ikichukuliwa ni hali ya kawaida kwa baadhi ya watu. Amesema kuwa, matusi yanayoendelea si kitendo cha kiungwana, matusi yanayojadiliwa mengi ambayo sasahivi yameshika hatamu ni kwamba mwanamke amekuwa mtu wa kutwezwa utu wake. "Kwenye mitandao panapotokea matusi ya kuondoa utu wa mtu kwa namna ambavyo heshima na utu wake unavyotwezwa kutokana na kafsha au kebehi au dhalilishaji maana yake sisi kama taaisisi tuna wajibu wa kutoa mawazo yetu", amesema Matwebe. Amesema kuwa, leo dunia n

USIKOSE KUFUATILIA UTABIRI WA HALIBYA HEWA KWA SAA 24, ZIJAZO

Image
 

HUU HAPA UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24, ZIJAZO

Image
 Usikose kufatilia utabiri wa Hali ya Hewa  

SERIKALI YATOA KIFUTA JASHO NA KIFUTA MACHOZI CHA ZAIDI YA TSHS. MILLIONI 399 KWA WANANCHI WALIOATHIRIWA NA TEMBO NACHINGWEA

Image
Na. Beatus Maganja SERIKALI kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imetoa kifuta jasho na kifuta machozi  cha zaidi ya shillingi millioni 399 kwa  wananchi 1,658 walioathiriwa na wanyamapori wakali na waharibifu katika wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi. Kauli hiyo imetolewa Aprili 09, 2024 na Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mhe. Mohamed Hassan Moyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ziara ya kuelezea jitihada zinazofanywa na Serikali kupitia TAWA katika kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu, ziara iliyofanywa na TAWA Mkoani humo. " Serikali kupitia utaratibu wake wa kifuta jasho na kifuta machozi, wahanga zaidi ya 1658 kwenye wilaya ya Nachingwea walipatikana lakini fedha ambazo Dkt. Samia Suluhu Hassan kazileta kwa ajili ya kifuta jasho Mwaka jana ni shillingi 399, 405,000/= na wale wote ambao waliokuwa wanastahili kupata kifuta jasho waliweza kukipata kifuta jasho hicho" alisema Mhe. Moyo Mhe. Mohamed Moyo amesema wilaya yake imekuwa ikikabiliwa na ch

ACT YATOA USHAURI KITENGO CHA MAAFA, MAFURIKO RUFIJI GUMZO

Image
Na Mwandishi wetu IMEBAINISHWA kuwa kuwepo kwa matukio ya majanga kwa miaka mingi ya hivi karibuni imeonesha uwezo mdogo wa kukabiliana na majanga pamoja na kuchukua tahadhari za majanga mbalimbali ikiwemo ajali na moto kutoka kitengo cha maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu Kivuli ACT Wazalendo, Isihaka Mchinjita amesema kuwa mwishoni mwa mwaka 2023 hadi sasa kumekua na udhaifu mkubwa wa kitengo cha maafa katika kuchukua hatua za dharura pindi majanga yanapotokea. "Kwa mfano Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) ilitabiri nchi kupokea mvua kubwa lakini watanzania hatukuona hatua madhubuti zikichukuliwa kujiandaa na kujilinda na janga hili ili kuepusha au kupunguza athari zinazowapata wananchi sasa"amesema Waziri Mkuu Kivuli Mchinjita. Aidha, amesema kuwa, ukanda wa Kibiti Rufiji eneo linalozunguka bonde la mto Rujifi hasa liliopo karibu na bwawa la kuzalisha umeme la Mwalim Nyerere kuna hali mbaya sana, kata zaidi ya