JUMIKITA YAALANI VIKALI WANAOTUMIA MITANDAO YA KIJAMII VIBAYA

 

Na mwandishi wetu, HabariPlus, Dar

Mwenyekiti wa Jukwaa la wanahabari wa Mtandao wa kijamii Tanzania (JUMIKITA ) Shabani Matwebe amelaani vikali vitendo vinavyofanywa na baadhi ya watu kutumia mitandao ya kijamii vibaya kwa kutoa lugha za matusi ambazo zimelenga kumdhalilisha mwanamke. 

Akizungumza na waandishi wa habari  Jijini Dar es salaam Matwebe amesema kumekuwepo na tabia kwa baadhibya watu kutumia mitandao hiyo vibaya kujadili matusi badala ya kujadili mambo ya maendeleo, huku tabia hiyo ikichukuliwa ni hali ya kawaida kwa baadhi ya watu.

Amesema kuwa, matusi yanayoendelea si kitendo cha kiungwana, matusi yanayojadiliwa mengi ambayo sasahivi yameshika hatamu ni kwamba mwanamke amekuwa mtu wa kutwezwa utu wake.

"Kwenye mitandao panapotokea matusi ya kuondoa utu wa mtu kwa namna ambavyo heshima na utu wake unavyotwezwa kutokana na kafsha au kebehi au dhalilishaji maana yake sisi kama taaisisi tuna wajibu wa kutoa mawazo yetu", amesema Matwebe.

Amesema kuwa, leo dunia nzima inapambana namna ya kumlinda mwanamke, na hakuna namna ya kulifanikisha jambo hili kama kwa kauli Moja tukikubaliana kwamba tujadili hoja, tuikosoe serikali, tuseme mahitaji ya wananchi, tuseme changamoto za wananchi ili Serikali ichukue hatua.

Hata hivyo, amesema wao kama Taasisi wameona wana mambo makuu mawili,wayatoletee ufafanuzi ikiwemo kukemea, kuendelea kunyamaza kimya ni kwamba tunaendelea kufanya jambo liendelea pasipo na msingi maalumu.

"Serikali mwaka huu inaingia kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa na mwakani uchaguzi mkuu, wapo watu mbalimbali watagombea wenye jinsia ya kike, kama leo hii watatwezwa na kudhalilishwa, nani mtoto wa kike atapata ujasiri wa kwenda kuchukua fomu,? anasimamaje jukwaani kusema chochote!"amesema Shaban.

Aidha, amevitaka vyombo na tasisi zote zinazotetea masuala ya wanawake kuacha kukaa kimya na badala yake wakemee na kulaani matusi ya mwanamke mwenzao kwa kuwa kukaa kimya kwao kuna maslahi wanayoyapata na matusi hayo.

Comments

Popular posts from this blog

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU NDIO USHAURI WA TMA KWA SEKTA HIZI ...