WANANCHI WAHIMIZWA KUTEMBELEA MAONESHO YA MUHARRAM EXPO 2025

Na Mwandishi wetu Wananchi wametakiwa kujitokeza kwa wingi kutembelea mabanda ya maonesho ya pili ya huduma za kifedhanq kijamii 'Muharram Expo 2025' yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam Kiongozi Mwandamizi wa Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Mohamed Issa, amesema maonesho hayo ni ishara ya kuingia mwaka mpya wa Kiislamu ambao ni Muharram sawa na mwezi wa kwanza wa kiislamu Hijiria. Amesema kuwa, katika maonesho hayo kutakua na mada mbalimbali ambazo zitatolewa kwa wananchi na wataweza kupata elimu kuhusu uwekezaji ambao hauna riba na watapata elimu namna ya kuweka akiba, kupata mikopo au uwezeshwaji usio na riba. Pia amesema wananchi watapewa elimu kuhusu huduma za Masoko ya mitaji na dhamana na uwekezaji wa pamoja (Collective Investment Schemes) isiyo na riba kama vile mifuko ya Uwekezaji Halal au Halal Fund, hati fungani zisizo na riba inayofahamika kama Sukuk. Aidha, katika Maonyesho h...