KIGOGO MWENGINE CHADEMA ATIMKIA CHAUMMA

 




Na Mwandishi wetu

Aliyekua Katibu Mwenezi wa Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA)Taifa, Sigrada Mligo, ametangaza kujiondoa rasmi ndani ya Chama hicho na kujiunga na Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kwa madai kuwa amechoshwa na kauli mbaya zinazotolewa dhidi yake.

Uamuzi huo ameutoa  ikiwa ni miezi kadhaa baada ya kuripotiwa kujeruhiwa na mmoja wa walinzi wa Chadema wakati wa kikao cha ndani kilichoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho John Heche March 25, 2025, mjini Njombe.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar-es Salaam katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama cha Chaumma Kinondoni amesema baadhi ya wanachama na viongozi wa Chama cha Chadema wamekuwa wakimtolea maneno na kumdhihaki kwa kumuita msaliti wa Chama licha ya kujitoa maisha yake yote.

Mligo amesema kuwa ameumizwa na namna anavyotajwa kuwa chanzo cha migogoro, licha ya kuwa mmoja wa waliokibeba chama wakati wa kipindi kigumu, hivyo ametumia busara ya kuhama Chama cha Chadema.

"Mwaka 2019 tuliendesha Chadema  Digital ambayo ilikuwa inasajili wanachama na kushughulikia masuala ya uchaguzi, lakini kwenye uchaguzi wa Januari 2025, Chadema ilishindwa kufanya operesheni kwenye majimbo ya Makete, Wang’ing’ombe na Ludewa kwa sababu ya ukosefu wa bajeti. Mimi ndiye nilimpigia Katibu Mkuu Mnyika kuuliza sababu, na yeye akathibitisha kuwa hawana fedha" amesema Mligo.

Mlingo amebainisha kuwa, aliamua kufadhili operesheni hiyo kwa fedha zake binafsi, akitumia zaidi ya shilingi milioni 15 kuhakikisha kuwa majimbo hayo matatu katika Mkoa wa Njombe yanashiriki mchakato wa uchaguzi wa ndani ya chama.

Ameongeza "Niliigharamia kwa fedha zangu hadi majimbo yanapata uongozi ambao ulipiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa chama, zipo kwenye kumbukumbu rasmi, hawawezi kubisha," amesisitiza.

Hata hivyo, Sigrada amesema licha ya kujitolea kwake kwa hali na mali, amekuwa akidhihakiwa na baadhi ya wanachama na viongozi wa Chadema ambao, kwa maneno yake, wanajifanya kuwa wao ndio waliokifia chama kuliko wengine.

"Sasa unakutana na lugha za kienyeji sana ambazo zinataka kuonesha kwamba kuna watu wameipambania Chadema, wameifia kuliko watu wengine, sisi wengine sio watu wa matangazo wala mitandaoni, nikisema niliyoyafanya kwenye chama hiki halafu mtu anakuja na lugha laini kwamba Sigrada anakiua chama, unamshangaa" ameeleza Sigrada.

Comments

Popular posts from this blog

MALYA ACHUKUA FOMU YA UDIWANI VITI MAALUM

MAKAMO WA RAIS SMAUJATA ATIA NIA UBUNGE KIVULE

MWINJUMA AUTAKA UBUNGE KIVULE