Posts

Showing posts from April, 2025

MSHINDI WA KWANZA KUJINYAKULIA MILL 10, NGAO NA CHETI TUZO YA MWALIMU NYERERE

Image
  Na Mwandishi wetu Tuzo ya kitaifa ya Mwalimu Nyerere ya uandishi wa bunifu itatolewa April 13 jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa super Dome Masaki ambapo itahusisha mkusanyiko wa mashairi, tamthilia, hadithi za watoto na Riwaya . Aidha, mshindi wa kwanza wa tuzo hiyo atajinyakulia kitita cha shill mill 10, ngao pamoja na cheti na muswada wake utachapishwa na kusambazwa shuleni na kwenye maktaba za taifa, Mshindi wa Pili: Tuzo ya Shilingi Milioni 7 pamoja na Cheti, Mshindi wa Tatu: Shilingi milioni 5 na Cheti.  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo hiyo, Prof. Penina Oniviel Mlama, amesema Kamati imetoa taarifa hiyo leo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya hafla ya kilele cha utoaji wa tuzo hizo. Aidha, Prof Mlama ameishukuru jamii ya wanahabari kwa mchango wao mkubwa katika kuitangaza Tuzo hiyo tangu ilipoanzishwa katika mwaka wa fedha 2022/23. "Kamati ya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu leo imetangaza zawadi ...

PROF LIPUMBA ATOA RAI HII KWA SERIKALI

Image
  Na wandishi wetu  Chama cha Wananchi (CUF) kimeitaka Serikali kupitia hotuba za bajeti ya mwaka huu kuchambua sababu za nini haifikii malengo ya Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo. Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Chama hicho Prof. Ibrahim Lipumba Wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juu ya mtazamo wa CUF kuhusu Bajeti ya Mwisho ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo 2021/22 hadi 2025/26. Amesema kuwa kikao cha Bunge la Bajeti kinatarajiwa kuanza Aprili 8, 2025 na kwamba hii itakuwa Bajeti ya mwisho ya utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo 2021/22 – 2025/26 na mwaka wa mwisho wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, bajeti za Serikali zilizopita hazijajikita katika utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo.  Prof. Lipumba amebainisha kuwa utaratibu wa zamani wa hotuba za Bunge la Bajeti ulianza na hotuba za Waziri wa Mipango na Waziri wa Fedha kueleza hali ya uchumi na utekelezaji wa mipango ya maendeleo na mapendekezo ya mapato na matumizi.  "Hiv...

MRADI WA KUFUA UMEME WA JNHPP WAKAMILIKA RASMI: DKT BITEKO

Image
Asema ni ndoto ya watanzania,awataka wategemee umeme wa uhakika Asisitiza kazi iliyobaki ni kuimarisha miundombinu ya kuwafikishia wananchi umeme Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Misri kuuzindua rasmi Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka Watanzania kutegemea kupata umeme wa uhakika baada ya Mradi wa kufua umeme kutoka Bwawa la Julius Nyerere uliokuwa ukisubiriwa kwa shauku kubwa na Watanzania  kukamilika  rasmi. Waziri Biteko ameyasema hayo leo April 5, 2025 baada ya kutembelea Mradi huo akiwa ameambatana na Mawaziri ambao ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mha. Hamadi Masauni. Amesema hivi sasa mitambo yote tisa inafanya kazi ambapo amefafanua kuwa  kukamilika kwa Mradi huo kumechangiwa na maono ya Rais wa Awamu ya Sita Mhe. Dokta Samia Suluhu Hassan ambaye aliupokea Mradi ukiwa katika asilimia 33 ya utekelezaji wake na ndani y...

TIMU YA YANGA YAKOSHWA NA "MAAJABU" YA TABORA ZOO

Image
Pacome, Diarra wavutiwa na mnyama Simba Na Beatus Maganja, TABORA   Viongozi na wachezaji wa Timu ya Young Africans (Yanga) leo hii wamefanya ziara katika Bustani ya Wanyamapori Hai Tabora, maarufu kama Tabora Zoo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kukuza utalii wa ndani na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini. Ziara hii iliongozwa na Rais wa Klabu ya Yanga, Injinia Hersi Said ikijumuisha wachezaji maarufu wa klabu hiyo. Katika mazungumzo yake baada ya ziara, Injinia Hersi Said alisema kuwa lengo kuu la ziara hiyo ni kuonyesha mchango wa klabu ya Yanga katika kukuza utalii wa ndani na vilevile kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kutangaza vivutio vya utalii vya nchi yetu.   “Ziara yetu hapa ni sehemu ya kuonyesha michango yetu katika kukuza utalii wa ndani, ikiwa ni njia mojawapo ya kuhamasisha Watanzania kutembelea vivutio vyetu vya utalii, lakini pia kuchang...