Posts

Showing posts from December, 2023

KILO 3,182, ZAKAMATWA DAR NA IRINGA,DCEA YAFUNGUKA

Image
Na Mwandishi wetu, Dar Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa Tanzania (DCEA) imekamata jumla ya kilogram 3,182 za dawa za kulevya aina ya Heroin na Methamphetamine katika oparesheni maalum iliyofanyika jijini Dar es Salaam na Mkoani Iringa kati ya tarehe 5 hadi 23 mwezi Dicemba mwaka 2023. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, mapema leo hii Kamishna Jeneral wa DCEA Aretas Lyimo amesema kuwa katika oparesheni hiyo jumala ya watu saba wamekamatwa kuhusika na dawa hizo ambapo wawili kati yao wana asili ya Asia. Amesema kuwa, kiasi hicho cha dawa za kulevya hakijawai kukamatwa katika historia ya Tanzania tangu kuanza kwa shughuli za udhibiti wa dawa za kulevya, hivyo watuhumiwa waliokamatwa ni miongoni mwa mitandao mikubwa ya wauzaji wa dawa za kulevya inayofuatiliwa nchini na duniani. "Kiasi hiki cha dawa za kulevya kinajumuisha kilogramu 2,180,29 za dawa aina ya methamphetamine na kilogramu 1001.71 aina ya heroin zilizokamatwa katika Wilaya  za Kigamboni, Ubu

MAKONDA AWAJIA JUU TANESCO, ATOA RAI KWA WANANCHI

Image
Na fatma Ally, Habari Plus Media KATIBU wa Itikadi na Uenezi  Paul Makonda amelitaka shirika la umeme Tanesco kujitafakari upya kwa hali ya ukatikaji wa umeme ovyo ambapo imekua ni changamoto kubwa jambo ambalo limekua linarudisha nyuma harakati kubwa za maendeleo kwa taifa. Kauli hiyo, ameitoa leo jijini Dar es Salaam wakati alipokua akitoa tathmini ya robo mwaka ya chama cha mapinduzi amesema kuwa, hivi karibuni Tanesco wamemuahidi Rais Samia ya kwamba ifikapi Januari kuwa kinu cha umeme kitawashwa hivyo ni vyema ahadi hii ikatekelezwa kwa vitendo. Aidha amewataka watendaji wote kuanzia ngazi shina hadi mkoa kusikiliza kero za wananchi Ila kutatua changamoto zinazowakabili na sio kukaa ofisini "Nataka niwakumbushe ndugu viongozi tuliopewa dhamana na Rais Samia ya kuwatumikia wananchi ni vyema tukatekeleze wajibu wetu tusisubiri mpaka Rais Samia anzishe ziara aanze kasimamishwa njiani na wananchi ili watoe malalamiko yao"amesema Makonda.  katika hatua nyengine amewataka wana

WAMILIKI WA MALORI WATAKIWA WAWAJALI MADEREVA WAO

Image
Na mwandishi wetu, Dar WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wamiliki wa malori nchini wawajali madereva na wahudumu wa magari hayo ikiwa ni pamoja na kuboresha maslahi yao. Amesema uanzishwaji wa kanzidata ya taarifa za madereva utawawezesha wamiliki hao kutumia taarifa hizo kwa lengo la kusimamia usalama wa madereva pamoja na kufuatilia mienendo na ufanisi wao. “Katika hili, niwasisitize kuhusu kuzingatia usalama na maslahi ya madereva wenu ambao kimsingi ni walinzi wa mitaji yenu kupitia vyombo ambavyo mmewapa dhamana ya kuviendesha. Haki iende na wajibu, yaani mnataka wawatumikie, kwa hiyo na ninyi mboreshe maslahi yao,” amesisitiza. Ametoa wito huo wakati akizungumza na wadau wa sekta ya usafirishaji waliohudhuria uzinduzi wa kanzidata ya madereva wa malori nchini leo (Alhamisi, Desemba 14, 2023) jijini Dar es Salaam. Kanzidata hiyo imeandaliwa na Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA). Akizungumza na wadau wa sekta hiyo, Waziri Mkuu amesema azma ya Serikali ya awamu ya sit

WAZIRI WA UCHUKUZI WA JAPAN KUFANYA ZIARA NA UJUMBE WA WATU 40 NCHINI TANZANIA

Image
  Na mwandishi wetu Waziri wa Ardhi, Miundombinu, Uchukuzi na Utalii wa Japan, Mhe. Konosuke Kokuba anatarajia kufanya ziara ya kikazi nchini mnamo mwezi Januari mwaka 2024. Katika ziara hiyo, Mhe. Kokuba ataongozana na ujumbe wa watu 40 kutoka kampuni binafsi zinazojihusisha na masuala ya miundombinu na baadhi ya watumishi wa Wizara yake. Ziara hiyo imelenga kujadili fursa mbalimbali zinazotokana na ushirikiano kati ya Tanzania na Japan katika maendeleo ya miundombinu. Hayo yamejiri katika kikao cha pamoja cha maandalizi ya ziara hiyo kilichoshirikisha viongozi wa Wizara ya Uchukuzi na Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Bwana Plasduce Mbossa pamoja na Menejimenti yake kilichofanyika jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara. Kwa upande wa Japan, ujumbe wake uliongozwa na Bwana Yoshihiro Kakishita kutoka Sekretarieti ya Wizara ya Ardhi, Miundombinu, Uchukuzi na Utalii ya Japan. Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Bwana Plasduce Mbosaa ametumia fursa hiyo k

PURA NA ZPRA WAJADILI NAMNA YA KUENDESHA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA

Image
  Na fatma Ally, Matukio DaimaApp, Dar  Mamlaka ya udhibiti mkondo wa juu wa Mafuta na gesi asilia PURA  na Mamlaka ya udhibiti wa utafutaji na uchimbaji wa mafuta na Gesi asilia Zanzibar (ZPRA) leo wamekutana jijini Dar es Salaam kwa lengo la  kuzishauri Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanziba jinsi gani ya kuendesha sekta za gesi na mafuta hapa nchini. Akizungumza jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Bodi ya PURA, Khalfan Khalfan amesema kuwa baada ya kumaliza kikao hicho ni mashirikiano makubwa kati ya ZPRA na PURA. Aidha, amesema kikao hicho kinategemea kutengeneza  fursa ya kunadi maeneo wazi (Vitalu) ambayo ni moja ya sera ya Serikali ya kutangaza uwekezaji. Amesema kuwa, baada ya kikao hicho watakua na msimamo wa pamoja ni kwa jisni gani sekta ya mafuta itapata wawekezaji katika pande zote bara na visiwani. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Udhibiti mkondo wa juu wa Petrol (PURA) Mhandisi Charles Sangweni amesema ku

TPA YAPOKEA TUZO YA UTOAJI BORA WA TAARIFA ZA KIFEDHA

Image
  Na mwandishi wetu, Dar Mkurugenzi wa Fedha na Uhasibu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), CPA Miraji Kipande akipokea tuzo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu kutoka kwa Mhe. Jamal Kassim Ali, Waziri wa nchi Afisi ya Rais Ikulu Zanzibar mara baada ya TPA kutangazwa mshindi wa 2 katika kitengo cha wakala wa serikali kwa utoaji bora wa taarifa za fedha. Tuzo hiyo ilitolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) katika hafla ya chakula cha jioni iliyofanyika jijini Da es Salaam.