PURA NA ZPRA WAJADILI NAMNA YA KUENDESHA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA

 

Na fatma Ally, Matukio DaimaApp, Dar 

Mamlaka ya udhibiti mkondo wa juu wa Mafuta na gesi asilia PURA  na Mamlaka ya udhibiti wa utafutaji na uchimbaji wa mafuta na Gesi asilia Zanzibar (ZPRA) leo wamekutana jijini Dar es Salaam kwa lengo la  kuzishauri Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanziba jinsi gani ya kuendesha sekta za gesi na mafuta hapa nchini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Bodi ya PURA, Khalfan Khalfan amesema kuwa baada ya kumaliza kikao hicho ni mashirikiano makubwa kati ya ZPRA na PURA.

Aidha, amesema kikao hicho kinategemea kutengeneza  fursa ya kunadi maeneo wazi (Vitalu) ambayo ni moja ya sera ya Serikali ya kutangaza uwekezaji.

Amesema kuwa, baada ya kikao hicho watakua na msimamo wa pamoja ni kwa jisni gani sekta ya mafuta itapata wawekezaji katika pande zote bara na visiwani.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Udhibiti mkondo wa juu wa Petrol (PURA) Mhandisi Charles Sangweni amesema kuwa leo wamekutana wakurugenzi wa bodi mbili kati ya Pura Zpra ambapo wamekuwa na mahusiano hayo kwa muda mrefu ambapo wameamua kuingia kwenye makubaliano kati yao Feb 19 mwaka 2022 hivyo waliunda timu ya pamoja.

Aidha, amesema kuwa, wao kama watendaji wamekuwa na mahusiano ya muda mrefu ya pande zote mbili ambapo kikao hicho kinalenga kubadilishana uzoefu wa kiutendaji sambamba na kuelekezana kwa yale ambayo upande mmoja hayajui katika utafitaji wa mafuta na gesi asilia.

Hata hivyo, amesema kikao ahiko pia kinalenga kutoa taarifa ambazo zimekuwa zikichukuliwa katika ardhi ya Tanzania, hivyo wameona ni vyema kushirikisha watendaji wa bodi kwani bodi ndio inayokuwa ikiwapa maelekezo ya kiutendaji na kuyatekeleza kiutendaji.

"Moja ya mambo ambayo tunakwenda kutekeleza pande zote mbili ni vitalu, baadae izae mikataba ya utafutaji wa mafuta na gesi, hivyo tumegundua wenzetu wa ZPRA na sisi tunaenda pamoja ndio maana tukaona tushirikiane ili kuleta hamasa na gharama za kutekeleza jambo hili na hii nchi ni moja na faida itakayopatikana ni kwa pande zote mbili"amesema Mhandisi Sangweni.

Naye, Mkurugenzi Mwendeshaji ZPRA,  Adam Abdulla Makame amesema kuwa Taasisi hiyo imekua na majukumu sawa na PURA  ambapo kazi kubwa ni kusimamia sekta ya mafuta na gesi katika mkondo wa juu ili kuhakikisha Tanzania  inanufaika na sekta ya nishati na gesi asilia.

"leo tumekutana hapa ikiwa ni kikao chetu cha kwanza cha bodi zetu mbili ikiwa ni ZPRA na PURA ili kuweza kujadiliana kwa pamoja ni jansi gani tutaweza kufanya kazi kwa pamoja kufungua maeneo yetu na kufanya kazi kwa pamoja katika utafutaji wa mafuta na gesi asilia"amesema  Makame.

Aidha, amesema kuwa katika historia inaonesha kuwa suala la kunadi vitalu ama kuvutia wawekezaji lilifanywa kwa miaka 10 iliyopita ambapo tangu mwaka 2013 hawakuendelea tena na zoezi hilo, hivyo kupitia kikao hicho watapata makubaliano ya pamoja kwa Tanzania bara na Visiwani na kuwa na mkakati wa pamoja ambapo ni kwa namna gani wataweza kuvitangaza vitalu hivyo.

Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI