Posts

Showing posts from June, 2024

RAIS FILIPE NYUSI KUZURU TANZANIA SIKU 4

Image
Na mwandishi wetu, HabariPlus, Dar Rais wa Jamuhuri ya Msumbiji Filipe Nyusi anatarijiwa kuwasili nchini Tanzania kwa ziara ya siku 4 ambapo pamoja na mengine anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (Saba saba) ambayo atayafungua Julai 3, 2024. Akizungimza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa, Januari Makamba amesema kuwa Rais Filipe Nyusi anakwenda Tanzania kwa mwaliko wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Amesema kuwa, Rais Nyusi anakwenda nchini humo kwa sababu mbili ya kwanza ziara ya kitaifa ambapo atakutana na Rais Samia ikulu jijini Dar es Salaam ambapo watajadili mambo mengi ikiwemo na ushirikiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili ili kuimarisha mahusiano yao. "Rais Filipe Nyusi anakuja nchini kwetu kwa ziara ya siku nne kwa sababu ya kufungua maonyesho ya sabasaba na ziara ya kitaifa ambapo atawasili tarehe 1 atapokelewa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius nyerere na vio

SPIKA WA BUNGE AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA NSSF

Image
Na MWANDISHI WETU, Dodoma. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na Bw. Masha Mshomba, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), baada ya kuhitimisha Bunge Jijini Dodoma, tarehe 28 Juni, 2024. Mazungumzo hayo yalihusu utaratibu wa ulipaji mafao ambao NSSF imeendelea kuuboresha kupitia mifumo ya TEHAMA. Aidha, Bw. Mshomba ameelezea maandalizi ya ulipaji mafao kwa kuzingatia maboresho ya kanuni ya kikokotoo, na ameipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya Uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kujali maslahi ya watanzania. Pamoja na hayo, Bw. Mshomba alitumia fursa hiyo kumpongeza Mhe. Dkt. Tulia Ackson kwa kuhitimisha Bunge la Bajeti kwa mafanikio makubwa.

HESLB YAWATAKA WANUFAIKA KUREJESHA MIKOPO, YAZINDUA KAMPENI MAALUM KUWASAKA

Image
Na Mwamdishi wetu,HabariPlus Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ( HESLB) leo imezindua kampeni yake ya kwanza ya Fichua "Kuwa Hero wa Madogo"ambayo imelenga kuhamasisha wanufaika wa mikopo hiyo ili na wengine waweze kusoma kupitia bodi hiyo. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akizindua kampeni hiyo Mkurugenzi Mtendaji Bill Kiwia amesema kuwa kampeni hiyo itadumu kwa miezi miwili lengo ikiwa ni kuhamasisha watanzania kuwafichua wanufaika wote ambao ambao wamepata mikopo hiyo ili na wengine waweze kutimiza ndoto zao za kusoma. Amesema kuwa, kampeni hiyo ni ya kizalendo ambayo inawataka wadaiwa wote ambao wamemaliza kusoma na wameajiriwa na wale ambao hawajaariwa wapo mtaani hawajalipa kurejesha pesa hizo, huku wakiahidi wapo tayari kupokea maoni ili kuendelea kufanya vizuri zaidi kwa awamu inayofuata. "Kuna wanufaika wa mikopo hii wengi wapo mtaani na hawajalipa, tunawaomba warejeshe mikopo hii ili wengine wenye mahitaji waweze kunufaik

DKT. BITEKO KUHITIMISHA KONGAMANO LA MAKANDARASI NA WATOA HUDUMA SHIRIKISHI TANZANIA

Image
  Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akiwa ameambatana  na Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa amewasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Dar es Salaaam (JNICC), kwa ajili ya kufunga Kongamano la Makandarasi na Watoa Huduma Shirikishi Tanzania, leo tarehe 28 Juni 2024. Dkt. Biteko amemwakilisha Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kongamano hilo la siku mbili lililoandaliwa na Chama cha Umoja wa Makandarasi na Watoa Huduma Shirikishi Tanzania (TUCASA), likiongozwa na Kauli mbiu isemayo; “Mjenga Nchi ni Mwananchi, Makandarasi Wazawa Tunaweza”.

USIKOSE KUFUATILIA UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO KUANZIA SAA 3:00 USIKU

Image
 

MKANDARASI ATAKIWA KUHARAKISHA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UMEME WA JUA KISHAPU

Image
picha mbalimbali za matukio  *Amtaka Meneja kuhakikisha  anawasimamia vema mkandarasi *Mradi kuleta tija kwenye upatikanaji wa Umeme  Kishapu, Shinyanga Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu Wizara ya Nishati, Mhandisi Innocent Luoga ameridhishwa na hatua mbalimbali za maendeleo katika upatikanaji wa huduma ya Umeme mkoani  Shinyanga huku akimsisitiza mkandarasi mradi wa umeme wa Jua wilaya ya Kishapu kukamilisha mradi huo kwa wakati utakaozalisha Megawati 150. Kamishna Luoga amempongeza Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga na menejimenti yake kwa usimamizi mzuri wa miradi ya umeme huku akiwasisitiza wakandarasi kukamilisha kwa wakati miradi inayoendelea ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na serikali  "Nikupongeze meneja kwa usimamizi mzuri kwa wakandarasi maana ukimsimamia hawezi kuacha kufanya kazi ,mara nyingi sana wakandarasi wanazembea au wanakimbia ni kwa sababu tu haupo usimamizi mzuri kwahiyo ongezeni usimamizi kwa hao wakandarasi ikiwa ni pamoja na kutembelea miradi na kuf

NAIBU WAZIRI MKUU DKT BITEKO KUFUNGUA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA UCHUMI WA BLUU

Image
Na Mwandishi wetu, HabariPlus Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI)  kwa kushirikiana na Chuo Cha Bahari cha Ghana wameandaa kongamano la 3 la kimataifa la uchumi wa bluu ambalo pamoja na mambo mengine wanakwenda kujadili maendeleo ya teknolojia ili kuhakikisha uchumi wa bluu unakua endelevu. Aidha, Naibu Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Dotto Mashaka Biteko anatarajiwa kufungua kongamano hilo la siku mbili  ambalo litahudhuriwa na wadau mbalimbali wa mnyororo wa thamani wa uchumi wa bluu. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkuu wa Chuo cha DMI, Dkt Tumain Gurumo amesema kuwa lengo la kongamano hilo ni kuiangalia kesho ya uchumi wa bluu inayojumuisha ulinzi, usalama na mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na maendeleo ya teknolojia kwa ukuaji wa uchumi wa bluu . Amesema kuwa, katika kongamano hilo litahudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo taasisi za umma, binafsi, Serikali, wanasiasa , wataalamu wa bahari, utalii, bandari, mafuta na gesi pamoja na u

LHRC YATOA MAPENDEKEZO HAYA KWA SERIKALI

Image
Kituo cha Sheria na Haki za Binaadam (LHRC) kimeiomba Serikali kupunguza kodi ya ongezeko la thamani kwenye bidhaa zote zenye uhitaji mkubwa kwenye matumizi ya nyumbani kama vile bidhaa za Chakula ili kupunguza ukali wa maisha. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mapema leo hii Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Wakili Fulgence Massawe wakati akitoa maoni ya kituo hicho, kuhusu bajeti ya serikali kwa mwaka 2024/25 ambapo amesema kuwa katika kipindi cha miaka miwili mfululizo kutokana na sababu mbalimbali za siasa za ulimwemguni gharama za maisha zimepanda. "Gharama za maisha zimepanda kwa miaka miwili mfululizo ikilinganishwa na kipindi kabla ya miaka miwili, msingi wa mapendekezo haya unaendana na ibara ya 14 ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania , 1977 inayobainishwa haki ya kuishi"amesema Wakili Massawe. Amesema kuwa, makadirio ya mapendekezo ya bajeti ya Serikali yamekuwa ya matumizi ya  kawaida zaidi kuliko maendeleo ambapo asilimia 70 ni matumizi ya

DOYO AAHIDI KUONDOA UMASKINI TANZANIA

Image
MGOMBEA wa Nafasi ya Uenyekititi Taifa wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Doyo Hassan Doyo amesema akichaguliwa kwenye nafasi hiyo kipaumbele chake ni kuhakikisha anapambana na hali ngumu ya Maisha anayodai inawakumba watanzania. Doyo ameyasema hayo leo mapema jijini Dar es Salaam wakati akirudisha fomu kwenye ofisi za chama hicho Buguruni jijini hapa. “Watanzania wanahali ngumu ya maisha ,vitu vimepanda bei,nikipata nafasi hii nitakuwa mstari wa mbele kuwatetea watanzania”Amesema Doyo. Hata hivyo,Doyo amezungumzia mikopo ya wanawake ambayo amesema imekuwa ikiwaumiza wanawake nchini kwa kufilisiwa mali zao. “Mimi nimeezunguka mikoani nimeona watanzania wakiumizwa na mikopo umiza,nikipata nafasi nitahakikisha sheria ya mikopo inabadilishwa ili waweze kusaidiwa”Amesema Doyo.

MCHAMBUZI WA SIASA AMJIA JUU MBUNGE MPINA KUHUSU SAKATA LA KUMUITA WAZIRI BASHE FISADI

Image
Msomi na Mchambuzi wa maswala ya  Siasa na uchumi Nchini, Kasim kibao amemjia juu mbunge was kisesa  Luhaga Mpina kwa kitendo chake cha kupotosha umma  juu ya shutuma alizozitoa kwa Waziri wa kilimo na Chakula Hussein Bashe ambapo amemshutumu kwa kumuita fisadi kufuatia kutoa vibari vya uagizaji sukari kwa wafanyabiashara. Akizungumza na waandishi wa habari Leo Jijini dar es salaam, Kibao amesema kitendo alichofanya mh.mpina ni kukosa subra kwani alipaswa kufuata ushahuri wa Mheshimiwa spika bunge la jamhuri ya Muungano WA Tanzania Turia Akson ambaye alimtaka kuleta ushahidi juu ya shutuma hizo na nyingine mbalimbali. katika hatua nyingine Kibao amemesa kitendo kinachofanywa na mbunge huyo ni kuleta taharuki kwa Wananchi jambo ambalo amesema ni kinyume na taratibu na Sheria za nchi. Hata hivyo,  amesema anachokifanya Mhe. mpina ni kutafuta huruma kwa Wananchi jambo ambalo amesisita kuwa halina afya kwa Taifa Aidha Kibao amefafanua kuhusu sakata Mheshimiwa Waziri kilimo mh bashe ambaye

HUU HAPA UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24,

Image
 

BENKI YA AKIBA YATOA ELIMU YA FEDHA KWA WADAU MBALIMBALI

Image
Na mwandishi wetu, matukio Daima Benki ya Akiba imesema itaendelea kuunga mkono Serikali kwa kutoa elimu ya fedha huku ikiboresha huduma zake nchi nzima ili kusaidia kuwafikia wananchi wengi zaidi na kuchochea  kukua kwa  uchumi wa Taifa. Kauli hiyo imetolewa jijini Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Akiba Silvest Arumasi wakati wa kuhitimisha mafunzo ya elimu ya fedha yaliyojumuisha viongozi wa benki hiyo, watumishi kutoka Wizara,  taasisi na ofisi mbalimbali za Serikali lengo likiwa ni kubadilishana ujuzi na kujenga mahusiano mazuri huku wakifahamiana na kuweka mikakati ya pamoja namna ya kuwahudumia watumishi wa Umma kwa weledi zaidi na kujibu maswali na kujibu maswali huku wakitatua kero zinazojitokeza kiutendaji. Mkurugenzi Arumasi amebainisha kuwa benki hiyo itawaangalia wananchi wa Dodoma kwa upekee kutokana na fursa mpya zilizopo katika Jiji hilo kwani serikali  imekuwa ikiendeleza na kustawisha Makao makuu ya Nchi hivyo ametoa rai kwa wananchi  kujishughulisha na biasha

BODI YA TAWA KUJA NA MIKAKATI KABAMBE YA KUIBORESHA HIFADHI YA PANDE

Image
Picha mbalimbali za matukio Na Beatus Maganja, Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TAWA Mej. Jen. (Mstaafu) Hamis Semfuko amesema Bodi anayooingoza imejipanga kuja na mipango madhubuti ya kuifanya Hifadhi ya Pande iliyopo Jijini Dar es Salaam kuwa kivutio kikubwa kwa watu waishio  ndani na nje ya Jiji hilo. Akizungumza na waandishi wa habari    katika ziara  iliyofanyika Juni 13, 2024 hifadhini humo, Semfuko amesema  Bodi yake imedhamiria kuwafanya watanzania waione Hifadhi ya Pande kuwa ni sehemu ya kipekee kwa ajili ya kustarehe na kupumzisha akili zao, na kwa kuanzia imeanzisha bustani wa wanyamapori hai ndani ya hifadhi hiyo ambao wako huru kutembea "free roaming" ikiwa na wanyamapori mbalimbali kama vile nyumbu, pundamilia, swala n.k Katika hatua nyingine amebainisha mikakati ya  kuendelea kuboresha miundombinu ya hifadhi hiyo sambamba na kuongeza aina mbalimbali za vivutio vya utalii ikiwemo wanyamapori aina ya twiga na faru lakini pia kuongeza kasi ya k

SGR KUANZA SAFARI RASMI KESHO

Image
  Na Mwandishi wetu,HabariPlus Shirika la Reli Tanzania (TRC) limezindua rasmi kampeni ya kuanza safari kwa treni ya kisasa ya SGR yenye kiwango cha kimataifa   June 14, 2024 kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro kwa bei ya sh 13000. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Massanja Kadogosa amesema kuwa uzinduzi rasmi utafanyika Juni 25 mwaka huu ambapo utazinduliwa na Rais Dkt Samia Suluh Hassan. Amesema kuwa, uwepo wa treni hiyo utarahisisha usafiri kwa wananchi kwa gharama nafuu zaidi na usalama wa hali juu ambapo abiria watakapokuwa kwenye treni hiyo watafurahia huduma bora zitakazotolewa na wahumu . Aidha, amesema ujio wa reli ya kisasa SGR haijaja kuchukua nafasi ya basi, reli ndege wala treni ya zamani bali ni mabadiliko ya kiuchumi na maendeleo ya taifa. Hata hivyo, amesema wameshirikiana na Tanzania Commercial Benk (TCB) katika suala zima la ukatishaji wa tiketi ambapo wateja watatumia benki hiyo

ACT YAPINGA TAMISEMI KUSIMAMIA UCHAGUZI

Image
  Na Mwandishi wetu, Habari Plus Chama cha ACT-Wazalendo kimesikitishwa na taarifa walipokea kutoka kwa msajili wa vyama vya siasa kuwataarifu kuwa Wizara Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) itaendelea kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwani kufanya hivyo ni kuvunja sheria.  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Chama hicho Ado Shaibu amesema wapokea barua ambayo inaeleza TAMISEMI inaendelea na maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ambapo Juni 15, 2024 itafanya kikao cha wadau kukusanya maoni ya rasimu ya kanuni zitakazosimamia uchaguzi huo. Amesema kuwa kitendo cha Tamisemi kusimamia uchaguzi wa Serikali za mitaa ni kuvunja sheria kwani kifungu cha 10(1)(c) cha Sheria ya Tume Huru ya Uchaguzi ya Mwaka 2024, kinaeleza tume hiyo ndio  imepewa jukumu la kusimamia uchaguzi wa mitaa, vijiji na vitongoji.  "Msimamo wa muda mrefu wa Chama chetu ni kuwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa usimamiwe na Tume Huru ya Uch

TAASISI YA MAMA ONGEA NA MWANAO YATOA VITI MWENDO 250 KWA WATOTO WENYE UHITAJI

Image
Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wametoa msaada wa viti mwendo 250 kwa ajili ya watoto wenye uhitaji maalum ambavyo vitawasaidia kutimiza ndoto zao za kupata elimu. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Steve Nyerere amesema kuwa kampeni hiyo ya kugawa viti mwendo kwa watu wenye mahitaji maalum ni juhudi za kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluh Hassan katika kuhakikisha watoto wote wanapata elimu. Amesema kuwa, kuna baadhi ya wazazi wamekuwa wakipitia wakati mgumu mara baada ya kujifungua watoto wa aina hiyo kwani hutelekezwa na waume zao. "Kuna wanaume ni wazembe katika kulea watoto wenye ulemavu ambapo hufikia kusema watoto hao sio wa kwao na kuwatelekeza, kuwaacha katika mazingira magumu"amesema Steve. Ameongeza kuwa, mtoto kuzaliwa na hali ya ulemavu haimzui kupata haki yake ya msingi ya kupata elimu bora kwani kupata mtoto mwenye hali hiyo ni mip

JUMIKITA :SERIKALI ISIINGIE KWENYE MTEGO WA KUFUNGIA MTANDAO WA 'X ' ZAMANI TWITTER

Image
Baada ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi chini ya Mwenyekiti wake  Mohammed Ali Kawaida kuitaka Serikali kupitia Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kufungia Mtandao wa X ambao Zamani ulijulikana kama Twitter kutokana na mtandao huo kuruhusu mambo ambayo ni kinyume na Utamaduni wa Watanzania  Leo Juni 12,2024, Jukwaa la wanahabari wa mitandao ya Kijamii Tanzania(JUMIKITA) likiongozwa na Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Ndg.Shabani Matwebe limeiomba Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania chini ya Uongozi makini wa Dkt.Samia Suluhu Hassan kutokubali kamwe kuingia kwenye mtego wa kufungia mtandao huo wa Kijamii  "Ni kama ilivyo Instagram  ,Facebook na YouTube, 'x' au Twitter  ni sehemu ambayo vijana wa Kitanzania wamekua wakilitumia Jukwaa hilo kujipatia riziki mfano Matangazo lakini pia hata Kazi nzuri za Serikali mbalimbali Wanahabari wa mtandaoni wamekua wakizichapisha 'x' " Taarifa ya Jukwaa imeongeza kua "JUMIKITA ipo tayari kushir

USIKOSE KUFUATILIA UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24, ZIJAZO

Image

KAWAIDA - VIJANA KEMEENI MATUMIZI YA MTANDAO WA X

Image
  Na Mwandishi wetu, HabariPlus Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mohamed Kawaida amewataka vijana wa Chama hicho kukemea juu ya matumizi mabaya ya mtandao wa Twitter  maarufu kama X nchini Tanzania kutokana na kubadilika kwa maudhui ya mtandao huo. Kauli hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa hivi karibuni wamepokea taarifa ya kushtua kutokana na mtandao huo kubadilisha maudhui yake na kuanza kuruhusu kutumika kwa picha za ngono maarufu kama ponogroph. Amesema kuwa, picha zinazorushwa kwenye mtandao huo hazina maadili kwa kizazi cha kitanzania hasa ukilinganisha watoto wengi na vijana wamekua wakitumia simu kuingia kwenye mitandao hivyo kuwepo kwa picha hizo mtandao ambapo zinapotosha watoto kufuata na kufanya mambo yasiofaa. Amesema kuwa, Uvccm wamekua wakua walezi wazuri wa maadili kwa vijana wote hivyo hawapendezwi na mtandao huo kuamza kubadilisha maudhui yake na kuruhusu matumizi ya picha

VIONGOZI WA DINI WAIOMBA SERIKALI KUUFUNGIA MTANDAO WA X

Image
  Viongozi wa Dini nchini Tanzania wamezitaka mamlaka za Serikali kuufungia mtandao wa Kijamii wa Twitter maarufu kama X kwa kuhamasisha vitendo vya mapenzi ya jinsia moja (ushoga) Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Alhaj Dkt Abdul Suleiman amesema mtandao huo umekua ukihamasisha vitendo vya ushoga, jambo ambalo limepigwa vita vimepigwa vita hata katika maandiko ya dini. Dkt Sule amesema kuwa, kufuatia mtandao wa X (Twitter) kuruhusu kuchapisha maudhui yanayohamasisha vitendo vya mapenzi ya jinsia moja ikiwemo ushoga na usagaji mamlaka zinazohusiana na mawasiliano zinatakiwa kuchukua hatua za haraka  ikiwemo kuufungia kabisa mtandao huo. Kwa upande wake,  Katibu mkuu wa Kanisa la Methodox Tanzania Askofu Allen Siso amesema katika vitabu vya dini zote havikubaliani na ndoa za jinsia moja akitolea mfano kitabu cha Warumi 1:26 kinachosema 'hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili na wa

FRIENDS OF SERENGETI YATOA UFADHILI WA VIFAA VYA DORIA VYENYE THAMANI YA ZAIDI YA TZS. MILLIONI 40 KWA ASKARI WA UHIFADHI WA TAWA

Image
Na Beatus Maganja, Arusha. Katika kuunga mkono jitihada za Serikali za kuhifadhi na kulinda rasilimali za wanyamapori nchini ikiwa ni pamoja na  kudhibiti wa wanyama wakali na waharibifu,  Marafiki wa Serengeti Uswisi "Friends of Serengeti Switzerland" wametoa msaada wa mahema 20, mabegi ya kulalia "Sleeping bags" 20 yenye  thamani ya Shillingi Millioni thelathini laki tisa na elfu arobaini (30,940,000/=) pamoja na Lita 2,120 za mafuta ya gari zenye thamani ya Shillingi Millioni Saba (7,000,000/=) kwa ajili ya kusaidia shughuli za doria kwa Askari wa TAWA Kanda ya Kaskazini. Akimkabidhi Kaimu Kamanda wa Uhifadhi TAWA Kanda ya Kaskazini Privatus Kasisi msaada huo Katika Ofisi za Kanda zilizopo jijini Arusha Juni 09, 2024, Bi Suzan Peter Shio Kwa niaba ya bodi ya Marafiki wa Serengeti Uswisi amesema lengo na shabaha yao ni kusimamia uhifadhi wa mazingira na wanyamapori ili kuhakikisha Tanzania inakuwa katika hali yake ya uasili kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo.

USIKOSE KUFUATILIA UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO

Image
 
Image
 ACB PLC YAZINDUA VIUNGA VILIVYOBORESHWA VYA INDEPENDENCE SQUARE, DODOMA  Na Mwandishi wetu  Meneja wa tawi la Benki ya Akiba Dodoma Upendo Makula amesema benki hiyo imepunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya karatasi kwa kuboresha huduma zake za kidijitali, zikiwemo Akiba Mobile, Akiba Wakala, kadi za VISA, taarifa za kielektroniki (E-statement), na huduma za benki Mtandao (Internet Banking). Kauli hiyo ameitoa katika hafla ya kukabidhi awamu ya pili ya uboreshaji wa viwanja vya independence square ambapo amesema jitihada za benki hiyo ni kubwa katika  kujitolea kuhifadhi na kutunza mazingira. Amesema kuwa, huduma hizio si tu kwamba zinapunguza matumizi ya karatasi, bali pia huleta urahisi na uhakika, hivyo kukidhi mahitaji ya soko kwa ufanisi.  Aidha, benki hiyo inatoa huduma mbalimbali kama mikopo, akaunti na bima, zinazowafikia wateja tofauti kuanzia mtu binafsi hadi makampuni makubwa na taasisi za serikali. Samba samba na kaulimbiu ya Siku ya Mazingira Duniani ya mwaka huu, isemayo

TAWA YANG'ARA MAONESHO YA UTALII NA BIASHARA TANGA

Image
Yanyakua tuzo na kujikusanyia vyeti kadhaa vya pongezi Na Beatus Maganja Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA imepokea tuzo ya mshindi wa pili wa jumla kwenye maonesho ya  11 ya utalii na biashara almaarufu "TANGA TRADE FAIR" yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya shule ya sekondari usagara Mkoani Tanga  kuanzia Mei 28, 2024 mpaka Juni 06, 2024. Sambamba na tuzo hiyo, TAWA pia imetunukiwa vyeti vitatu kwa ushindi  na  pongezi kwa kushiriki na kufanikisha maonesho hayo. Tuzo na vyeti hivyo vilitolewa Juni 06, 2024 na  Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Dkt. Batilda Buriani ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa hafla ya kuhitimisha maonesho hayo kwa Mwaka 2024 ambapo taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za Serikali zilishiriki. Licha ya kujikusanyia tuzo na vyeti mbalimbali vya pongezi, TAWA pia imepongezwa kwa kufanikisha uwepo wa wanyamapori hai ambao walikuwa   kivutio kikubwa na hamasa ya watu wengi kuhudhuria na kushiriki katika maonesho hayo. TAWA imeshiriki

JESHI LA POLISI LAJIPANGA KUKABILIANA NA VITENDO VYA KIHALIFU

Image
Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam Aprili mwaka huu,limesema limeongeza nguvu ya kukabilli viashiria vya vitendo vya kialifu na waarifu na kufanikiwa kukamata watu 13 wanaotuhumiwa kutumia, kuuza na  kuusambaza dawa za kulevya jijini humo. Pia kuanzia kipindi hicho limefanikiwa kukamata watuhumiwa hao wakiwa na kete 2,639, misokoto 158 na Puli 531 za bangi iliyokuwa imefungashwa tayari kwa matumizi,  viroba vinne vya dawa hizo pamoja na pikipiki mbili ambazo zinaaminika kutumika kisafirishia. Hayo yamebanishwa leo, Juni 7, 2024 jijini Dar es Salaam na  Kamanda wa Kanda Maalumu  wa jiji hilo SACP, Jumanne Muliro wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari. "Hatutaki kurudi nyuma tulikotoka ambako kulikuwa na vitendo vingi vya kiarifu, tutaendelea kudhibiti viashiria vyote vya kiarifu na waharifu ili  kulifanya Jiji hili kuendelea kuwa tulivu na usalama wakati wote. "Katika operesheni ambayo tumefanya baada kubaini uwepo wa viashiria vya vitendo vya kiharifu kutaka k

DOYO AJITOSA KUWANIA UENYEKITI ADC

Image
  Na Mwandishi wetu Ikiwa ni siku chache baada ya Mwenyekiti wa Chama chaAllience for Democratic Change, ADC,  Hamad Rashid kutangaza kuachia nafasi hiyo kwa mujibu wa katiba, amejitokeza Katibu Mkuu wa chama hicho Doyo Hassan Doyo kuwania nafasi hiyo. Akizungumza mbele ya waandishi wa Habari Katibu Mkuu wa Chama hicho, Doyo Hassan amesema amesema ameamua kuwania nafasi hiyo kutokana na uzoefu aliona ndani ya chama hicho ambapo atachukua fomu hiyo Jun 11 mwaka huu. "Sababu kubwa ambayo imenifanya kuwania nafasi hii ni kutokana na kuwa na uzoefu wa kutosha baada ya kulelewa  vema na aliyekuwa Mwenyekiti wetu, Hamad Rashid. Ameongeza "Nimekaa na Mwenyekiti wetu kwa muda wa miaka 10 nikiwa Katibu Mkuu na sikuwahi hata siku moja kutofautiana naye na nimejifunza mengi ikiwemo suala uvumilivu na kuheshimu Katiba, ambayo ameitekeleza kwa vitendo kwa kuondoka madarakanj kwa mujibu wa sheria tulizojiwekea," amesema. Amefafanua kuwa katika chama hicho ameweza kufanya kazi na viong