NAIBU WAZIRI MKUU DKT BITEKO KUFUNGUA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA UCHUMI WA BLUU


Na Mwandishi wetu, HabariPlus

Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI)  kwa kushirikiana na Chuo Cha Bahari cha Ghana wameandaa kongamano la 3 la kimataifa la uchumi wa bluu ambalo pamoja na mambo mengine wanakwenda kujadili maendeleo ya teknolojia ili kuhakikisha uchumi wa bluu unakua endelevu.

Aidha, Naibu Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Dotto Mashaka Biteko anatarajiwa kufungua kongamano hilo la siku mbili  ambalo litahudhuriwa na wadau mbalimbali wa mnyororo wa thamani wa uchumi wa bluu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkuu wa Chuo cha DMI, Dkt Tumain Gurumo amesema kuwa lengo la kongamano hilo ni kuiangalia kesho ya uchumi wa bluu inayojumuisha ulinzi, usalama na mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na maendeleo ya teknolojia kwa ukuaji wa uchumi wa bluu .

Amesema kuwa, katika kongamano hilo litahudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo taasisi za umma, binafsi, Serikali, wanasiasa , wataalamu wa bahari, utalii, bandari, mafuta na gesi pamoja na uvuvi.

"Lengo la kuwaalika wadau wote hawa ni kutaka ushiriki wa kila mdau katika mnyororo wa thamani wa uchumi wa bluu, mfano samaki anapovuliwa baharini kunakuwa na wadau wengi wanahusika hadi anapokufikia wewe mlaji, hivyo hawa wote wanatakiwa wapate mafunzo na elimu"amesema Dkt Gurumo.

Aidha, amesema kuna fursa nyingi kwenye uchumi wa bluu hivyo ni vyema kuzingalia kwa pamoja kwa kuwashirikisha vijana kwani wasipozifahamu hawawezi kuzindea wala kutoa msaada wowote wa ukuaji kwenye uchumi wa bluu .

Hata hivyo, amesema tafiti mbalimbali zimefanywa na wadau hivyo, kupitia kongamano hilo zitajadiliwa na wadau hao kutoka na   mapendekezo ambayo yatasaidia nchi ya Tanzania katika kukuza uchumi wa bluu.

Ameongeza kuwa, pia kongamano hilo linatarajia kujumuisha nchi 11 ikiwemo Kenya, Comoro, Liberia, Ghana Nigeria, Sieraleone, Denmark, Italy, Sweeden, Korea Kusini na China ambapo lengo ni kutoa elimu na mafunzo pamoja na kuangalia vyanzo vya maji na faida zake katika kukuza kipato.

Aidha, Kongamano la kwanza lilifanyika mwaka 2022, la pili lilifanyika mwaka 2023 na la tatu linatarajiwa kufanyika Julai 4  hadi 5 mwaka huu katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere ( JINCC) ambapo mambo mbalimbali yatajadiliwa na wadau hao ikiwemo kujifunza namna ya kukuza uchumi wa bluu kwenye nchi zao.

Comments

Popular posts from this blog

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU NDIO USHAURI WA TMA KWA SEKTA HIZI ...