Posts

Showing posts from January, 2023

MATHAMANI - SIJAKATAA UTEUZI

Image
Na mwandishi wetu,HPMedia, Kigoma Aliyekua Makamu wa Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Dinah Elias Mathamani amesema hajakataa uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mkoani kigoma aliyoteuliwa na Rais wa Jamhuribya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan uliofanyika January 25, 2023. Kauli hiyo ameitoa  January  31 mbele ya waandiahibwa habari mara baada ya kula kiapo cha uongozi kwa nafasi ya Mkuu wa Wilaya mbele ya mkuu wa Mkoa wa kigoma Thobias Andengenye katika ukumbi wa Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma. Amesema kuwa, amesikitishwa na taarifa zilizokua zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii ya kuwa amekataa nafasi ya uteuzi aliyopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kudai kuwa hazina ukweli wowote bali amefurahishwa sana na uteuzi huo na kuwa yupo tayari kuitumikia katika kiapo cha maadili ya uongozi. "Baada ya majina kutangazwa na kuona jina langu ni mmoja wa wateule nilifurahi na nikaanza kufanya mawasiliano na viongozi wa Wilaya yangu na kujiandaa na safari ya k

TANESCO YAJA NA MATUMAINI TELE KWA WANANCHI

Image
Na mwandishi wetu HPMedia, Dar es Salaam  I meelezwa kuwa katika kuhakikisha upatikanaji wa umeme nchini unakuwa wa kudumu, Shirika la Umeme nchini TANESCO linaendelea na ujenzi wa mradi wa bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere (JNHPP) ambalo limefikia asilimia 80.22 hadi kufikia tarehe 31 Desemba 2022. Aidha, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema kwa sasa hali ya upungufu wa umeme nchini umepungua kwa kiasi kikubwa na kufanya hali ya upatikanaji wa umeme kuboreka zaidi hivyo kupunguza adha ya mgao wa umeme uliokuwepo hapo awali. Akizungumza na waandishi wa habari  Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Maharage Chande amesema maboresho ya upatikanaji wa umeme yametokana na mipango ya muda mfupi na wakati ambayo imekwishatekelezwa na shirika hilo pamoja na uwepo wa mvua za vuli. Amesema kuwa,  urefu wa kina cha maji la bwawa hilo umefikia mita 126.12 kutoka usawa wa bahari na bado wanaendelea kujaza maji na linatarajiwa kujaa baada ya misimu minne ya mvua za vul

HUU HAPA UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO

Image
 Usikose kufuatilia utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo kila siku

BINT CCM YAWASHIKA MKONO KCC, KUELEKEA MIAKA 46 YA CCM

Image
  Na Mwandishi wetu HPMedia, Dar es Salaam  Katika kuelekea miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mabinti wa Chama cha Mapinduzi ( Binti Ccm) wametembelea kituo cha KCC kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam cha kulea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi na kutoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani isiyopungua millioni moja 1. Akizungumza na Mtandao wa Habari Plus Media, Mmoja wa wanzilishi wa Kampeni ya Binti CCM Twilumba Jane amesema msaada huo walioutoa kwa watoto hao ni muendelezo wa kuwafikia watu wenye mahitaji mbalimbali ya kijamii,ambapo wamekua wakifanya hivyo kwa miaka kadhaa tangu kuanzishwa kwa umoja huo.  Amesema kuwa, miongoni mwa vitu ambavyo wametoa katika kituo hicho ni pamoja na mchele kilo 50, unga kilo 50, mafuta lita 10, sukari kilo 20, maharage kilo 20, counterbook dozen 2, sabuni ya unga kilo 25, sabuni ya mche dozen 1 na nusu, viatu pea zisizopungua 20,nguo pamoja na mabegi ya shule 10. Aidha, amesema kuwa pamoja na mambo me

BENKI YA MAENDELEO YAFUNGA MWAKA KIBABE

Image
Na Mwandishi wetu, HPMedia, Dar es Salaam Benki ya Maendeleo Plc imesema imepata faida mara mbili kwa mwaka 2022, ikipata shilling bill 1.3122 ikilinganishwa na mwaka 2021 ambapo ilipata milioni 587 ikiwa ni sawa na ongezeko la zaidi ya mara mbili ya faida iliyopata iliyochangiwa na kutoa mikopo ya riba nafuu,kupata wanahisa wapya,ulipaji wa gharama mbalimbali kupitia benki hiyo . Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Benki wa benki ya Maendeleo Dkt Ibrahim Mwangalaba wakatib akitoa ripoti ya ufanisi na utendaji kazi wa Benki hiyo Kwa mwaka 2022 ambapo amesema benki hiyo imeweka historia yenye faida kwa Miaka 8 tangu kuanza kufanya kwake kazi mwaka 2015 . Dkt Mwangalaba amesema  kuwa faida hiyo imetokana na ukuaji wa jumla wa mapato kwa asilimia 22 mwaka hadi mwaka kutoka shilingi za kitanzania Bilioni 12.8 hadi shilingi za kitanzania Bilioni 15.6 mwaka 2022. "Tunafurahi kuripoti matikeo mengine ya kifedha ya Mwaka thabiti yayoongeza ufaulu ambao M

HAYA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE

Image
Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mitihani ya kidato cha nne yaliyofanyika Novemba 14 hadi Desemba 1, 2022, Tanzania Bara na Visiwani. Matokeo hayo yametangazwa Jumapili, Januari 29, 2023, makao makuu ya Necta jijini Dar es Salaam na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Athumani Amasi. Tazama kwa Kubofya  <HAPA> MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2022 MATOKEO YA MTIHANI WA MAARIFA (QT) 2022

ASKARI POLISI WALIPJIUNGA NA JESHI LA POLIS WATOA .SAADA

Image
Na Mwandishi wetu HPMedia, Dar es Salaam  Baadhi ya Askari Polisi aliojiunga na Jeshi la Polisi na kuhudhuria mafunzo ya awali mwaka 2000/2001 leo wametembelea Taasisi ya Saratani Ocean road na kutoa misaada kama sadaka kwa wagonjwa wanaougua maradhi ya saratani ikiwa ni namna ya kumshukuru Mungu kwa afya na uzima katika kipindi chote  cha kazi tangu walipojiunga na Jeshi la Polisi. Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya maofisa, wakaguzi na askari Polisi walipotembelea hospitalini hapo Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya jinai (DCI), Kamishna wa Polisi, Ramadhani Kingai amesema kwamba misaada hiyo imetokana na michango ya askari hao ambao walichanga na kununua zawadi kwa watu wenye uhitaji kama wagonjwa. Aidha, Kamishna Kingai amesema sadaka ni jambo ambalo linatimiza maelezekezo ya Mungu kutoka katika vitabu vitakatifu kwa kuwahurumia watu wenye uhitaji hivyo wanachi watambue kwamba Askari Polisi ni miongoni mwa wanajamii ambao wanajali na kuwathamini hivyo wanawaombea wapo

WAZIRI MKUU AWASISITIZA WABUNGE WASHIRIKI MICHEZO

Image
Na mwandishi wetu, HP Media, Dodoma WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo Jumamosi, Januari 28, 2023 ameshiriki Bunge Bonanza lililofanyika katika viwanja vya shule ya msingi na sekondari ya John Merlin ya jijini Dodoma ambapo ametumia fursa hiyo kuwasisitiza wabunge na wananchi wengine washiriki katika michezo ili kuipa miili yao nguvu na uwezo wa kutekeleza majukumu yao ya kikazi. “…Michezo kwetu sisi wabunge ni muhimu zaidi kwa sababu inatufanya tuwe na afya bora zaidi na pia michezo inasaidia watu kukutana pamoja na kuimarisha undugu, kujenga urafiki pamoja na kukuza vipaji. Nampongeza Mheshimiwa Spika Dkt. Tulia Ackson kwa ubunifu huu wa kuanzisha Bunge Bonanza ambalo litakuwa linafanyika mara kwa mara.” Waziri Majaliwa ameyasema hayo wakati akizungumza na wabunge, baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Watumishi wa Bunge pamoja na maafisa wengine wa Serikali walio shiriki katika bonanza hilo. Amesema bonanza lingine kama hilo linatarajiwa kufanyika Juni 24, 2023. Kwa upande wake,

DCEA YAKAMATA KILO 399.28 ZA BANGI

Image
   Na mwandishi wetu, HPMedia, Morogoro Mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na Dawa za (DCEA) imekamata jumla ya kilo 399.28 za dawa za kulevya aina ya bangi katika kitongoji cha sokoni, kijiji cha Chogoali kata ya Iyogwe, tarafa ya Gairo, Mkoani Morogoro. Ukamataji huo umefanyika kufuatia Operesheni iliyofanywa na mamlaka mkoani humo hivi karibuni ambapo watu wawili wanashikiliwa kuhusika na usafirishaji wa kiasi hicho Aidha watumiaji hao wamekutwa na bunduki mbili aina ya gobole zenye namba MG-188 na MG-148 pamoja na ngozi ya Mnyama anayedhaniwa kuwa kakakuona, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na na Dawa za kulevya inaendelea kufanya Operesheni nchi nzima ili kuhakikisha inadhibiti usafirishaji wa Dawa za Kulevya na inawaomba wanachi kuwaunga mkono katika mapambano hayo.

RAIS DKT SAMIA AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MTENDAJI WA KAMPUNI YA MAFUTA YA MAFUTA (UAE)

Image
Na Mwandishi wetu, HPM Dar es salaam  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Taifa ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ENOC LLC, Bw. Saif Al Falasi aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Januari, 2023. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Nishati tarehe 27 Januari, 2023 walisaini Mkataba wa makubaliano (Memorandum of Understanding) na Kampuni hiyo ya ENOC LLC kuhusu Ujenzi wa Kitovu cha Mafuta (Fuel Hub) hapa nchini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Taifa ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ENOC LLC, Bw. Saif Al Falasi pamoja na Ujumbe wake mara baada ya mazungumzo yao Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Januari, 2023.

RC MAKALLA ATOA AGIZO HILI KWA WAFANYABIASHARA MBAGALA

Image
Na mwandishi wetu, HPMedia, Dar es Salaam Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla Leo amefanya Zoezi la usafi Wilaya ya Temeke eneoa la Mbagala ambapo amepiga marufuku ufanyaji Biashara kwenye  ujenzi wa Barabara ya mwendokasi na maeneo yaliyokatazwa. Akizungumza na wananchi wakati akifanya zoezi hilo, amewakumbusha wananchi na viongozi kuanzia ngazi ya mtaa hadi Wilaya kuhakikisha wanasimamia usafi kila jumamos ya mwisho wa mwezi ili kuhakikisha maeneo yote ya jiji la Dar es salaam yanakua masafi. Aidha, amewaelekeza Wakurugenzi kusimamia Wakandarasi kuondosha taka kwa wakati na Wakandarasi watakaoonyesha kulegalega wasipatiwe mkataba. Pamoja na hayo amewapongeza Wananchi kwa mwamko Mkubwa wa kufanya usafi jambo lililopelekea Jiji la Dar es salaam kushika nafasi ya sita kwa usafi Barani Afrika na kuondosha magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindipindu. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Dar es salaam, zaidi ya shilingi bilioni 3.2 zimetolewa kama  mkopo kwa Wafanyabiashara Wan

MWENYEKITI ILALA ATOA MAAGIZO HAYA KWA VIONGOZI KATA YA LIWITI, SEGEREA NA TABATA

Image
  Na Mwandishi wetu, HPMedia, Dar es Salaam Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Said Sidde amewataka Madiwani na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kutoa taarifa za utekelezaji wa Ilani ya chama hicho kwa wenyeviti wa mashina ili waweze kuwaambia wanachama wao kazi zilizofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan.  Rai hiyo ameitoa alipokuwa katika Mkutano na viongozi wa Kata ya Liwiti, Segerea na Tabata ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake pamoja na kamati ya siasa wilaya kujitambulisha na kuwashukuru wanachama kwa kuwachagua kushika nafasi hizo, na kuahidi wapo tayari kutekeleza majukumu yao hususani katika kipindi hiki cha mkakati wa kufanya kazi za chama ndani ya chama na nje ya chama. Amesema kuwa, mikakati yao kama viongozi wa CCM Ilala ni kuhakikisha kuwa wanashinda uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024 kwa mitaa yote 159 na uchaguzi mkuu 2025 kushinda kata zote 36 na majimbo 3 na kura za ndio kwa Rais Dkt. Samia hivyo uongozi wa wilaya wamefanya vikao na

HAKI ELIMU YALAANI VITENDO VYA KIKATILI DHIDI YA WANAFUNZI

Image
  Na Mwandishi wetu, HPMedia,Dar es Salaam Shirika lisilo la kiserikali la HAKI ELIMU limelaani vikali tukio la adhabu ya kikatili waliyoipata wanafunzi wawili wa shule ya msingi Majanja wilayani Kyerwa Mkoani Kagera kutoka kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo. Hatua imekuja mara baada  kusambaa kwa video fupi katika mitandao mbalimbali ya kijamii nchini ikimuonyesha Mkuu huyo wa shule Isaya Benjamin akiwacharaza bakora kwenye nyayo za miguu wanafunzi wawili. Akizungumza na waandishi wa habari leo januari 26,2023 Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Haki elimu,Dkt John Kalage amesema kuwa kitendo hicho kinakiuka siyo tu haki za watoto bali pia ni kinyume na maadili ya kazi ya ualimu na malezi bora kwa wanafunzi. Dkt Kalage ameongeza kuwa shirika hilo linaipongeza Serikali kupitia Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda na uongozi wa mkoa wa Kagera kwa kuchukua hatua za haraka na za awali dhidi ya mwalimu aliyehusika na ukatili huo ikiwa ni pamoja na kumvua nafasi yake ya ualimu