BINT CCM YAWASHIKA MKONO KCC, KUELEKEA MIAKA 46 YA CCM

 


Na Mwandishi wetu HPMedia, Dar es Salaam 

Katika kuelekea miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mabinti wa Chama cha Mapinduzi ( Binti Ccm) wametembelea kituo cha KCC kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam cha kulea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi na kutoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani isiyopungua millioni moja 1.

Akizungumza na Mtandao wa Habari Plus Media, Mmoja wa wanzilishi wa Kampeni ya Binti CCM Twilumba Jane amesema msaada huo walioutoa kwa watoto hao ni muendelezo wa kuwafikia watu wenye mahitaji mbalimbali ya kijamii,ambapo wamekua wakifanya hivyo kwa miaka kadhaa tangu kuanzishwa kwa umoja huo. 

Amesema kuwa, miongoni mwa vitu ambavyo wametoa katika kituo hicho ni pamoja na mchele kilo 50, unga kilo 50, mafuta lita 10, sukari kilo 20, maharage kilo 20, counterbook dozen 2, sabuni ya unga kilo 25, sabuni ya mche dozen 1 na nusu, viatu pea zisizopungua 20,nguo pamoja na mabegi ya shule 10.

Aidha, amesema kuwa pamoja na mambo mengine lengo la BintiCCM ni kuhakikisha wanawafikia wahitaji wengi zaidi kwa kuwapatia mahitaji yao muhimu, elimu (capacity building ) n.k.

Ameongeza kuwa, malengo ya kampeni ya Binti CCM ni kujifunza kwa kuhamasishana wenyewe kwa wenyewe kuwa na moyo wa kujitoa kwa ajili ya wahitaji na hata baina yao na kushirikiana katika shughuli zao mbalimbali wanazozifanya za kiuchumi, kijamii, kielimu na hata kisiasa yaani Chama cha Mapinduzi.

"Leo tumefika hapa KCC kigambo na kampeni yetu ya "tuwape tabasamu" kuwafariji watoto hawa, tume furaha pamoja,tumekata keki, tumecheza nao michezo mbalimbali kwa kweli ilikua ni jambo zuri sana kwani hata sisi tumejifunza pia kutoka Kwao"amesema Imelda Antony ambaye ni mratibu wa kampeni ya BintiCcm Mkoa wa Dar es salaam.



Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI