Posts

Showing posts from February, 2024

BABU OWINO ATOA RAI KWA VIJANA WA ACT WAZALENDO, NONDO NAE YUPO

Image
Na Mwandishi wetu, Habari Plus Dar MBUNGE wa Jimbo la Embakasi Mashariki Nairobi, Kenya Poul Owino amewataka vijana nchini Tanzania kupigania kupata haki zao katika kulitetea taifa lao pamoja na kuwa viongozi bora kwa maslah mapana ya Taifa. Rai hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam mapema leo wakati alipokua akifungua kongamano la Ngome ya Vijana lililokwenda sambamba na uchaguzi wa viongozi mbalimbali ikiwemo nafasi ya Mwenyekiti, Makamo Mwenyekiti, Katibu, pamoja nafasi nyengine mbalimbali. Amesema kuwa, Chama cha ACT Wazalendo ni cha kuigwa kutokana na kuwa chama bora chenye mfumo imara wa kupigania haki na kuwalea vijana ambao wana uwezo wa kukipigania kwa  maslahi ya Taifa kwa ujumla. "Vijana ni Taifa la leo sio la kesho, mapambano yanatakiwa kuanza leo,  hivyo usikuabali kukaa kimya kwani usipokubali kuwa kwenye meza ukala utakua menu uliwe, vunja hiyo meza usipokua sehemu yao, Hayyat Mwalim Julias Nyerere, Kawawa na Kwame Nkuruma wangekua waoga unadhani uhuru ungepatikana? &qu

MKUU WA MKOA WA LINDI AWATAKA WAKAZI WA KILWA KUWA TAYARI KUWAPOKEA WATALII

Image
Na. Beatus Maganja Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Rajab Telack amewataka wakazi wa wilaya ya Kilwa na Mkoa wa Lindi kwa ujumla kuwa tayari kuwapokea watalii wanaotembelea Hifadhi ya Urithi wa Dunia ya Magofu ya Kilwa kisiwani na Songo Mnara na kutumia fursa hiyo kufanya biashara za bidhaa za utalii ili kuwaingizia kipato. Mhe. Zainab ameyasema hayo Februari 28, 2024 akiongea na waandishi wa habari ndani ya Hifadhi ya Urithi wa Dunia ya Magofu ya Kilwa kisiwani na Songo Mnara wakati wa mapokezi ya Meli ya Saba kuingia Hifadhini humo katika kipindi cha mwezi Februari ikiwa na idadi ya watalii 120 kutoka Mataifa mbalimbali Duniani. Amesema mfululizo wa safari za Meli za watalii ndani ya Hifadhi hiyo ni kiashiria kwamba filamu ya Tanzania The Royal Tour iliyochezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeleta matokeo chanya kwa Mkoa wa Lindi na Tanzania kwa ujumla. Mkuu huyo wa Mkoa amesisitiza kuwa Hifadhi ya Urithi wa Dunia ya Magofu ya Kilwa kisiwa

USIKOSE KUFUATILIA UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24, ZIJAZO

Image
 

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI

Image
Na Mwandishi wetu, Habari Plus, Dar Mfuko wa Bima wa Taifa wa NHIF imefanya maboresho ya kitita cha mafao kwa wanachama wake ambayo utekelezaji wake utaanza rasmi Machi Mosi mwaka 2024 ikwa lengo ni upatikanaji wa huduma bora wa wanachama pamoja na kuongeza huduma ambazo hazikuepo hapo awali. Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Dkt Bernad Konga amesema maboresho ya mwisho ya kiticha cha mafao ya mfuko huo kichotumika sasa yalifanyika June 2016 sawa na takribani miaka 8 iliyopita na hivyo upo umuhimu wa kufanya marejeo yake kutokana na sababu mbalimbali. Aidha, amesema kuwa,  maboresho hayo ya orodha ya huduma za matibabu ambazo zinatolewa kwa wanufaika wa NHIF na bei zake ambazo hutumika wakati wa malipo kwa madai ya watoa huduma za matibabu yamezingatia maendeleo ya teknolojia na hali halisi ya bei katika soko pia kuwianisha kitita cha mafao na miongozo ya tiba iliyoboreshwa Ili kuongeza ubora wa huduma zinazotolewa Kwa wanufaika wa mfuko.

TREN YA MWENDOKASI YAANZA MAJARIBIO DAR - MOR0

Image
Na Mwandishi wetu, HabariPlus,Dar Shirika la Reli Tanzania (TRC) leo limeanza safari ya kwanza ya majaribio kwa Treni ya umeme ya Abiria (SGR)  kutoka ofisi zake zilizopo jengo la Tinzanite maeneo ya stetion Jijini Dar es salaam kuelekea Mkoani Morogoro. Akizungumza na waandishi wa habari jijini humo mapema leo hii Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Masanja kadogosa amesema Usafiri huo wa Treni utatumia umeme wa kawaida kutoka TANESCO na wanatarajia kuanza safari za abiria hivi karibuni. Aidha amewatoa wasiwasi watanzania wanaodhania kuwa umeme ukikatika utaweza kuleta athari kwa Treni hizo kuwa sio kweli umeme wake umeunganishwa kutoka grid ya taifa hivyo si rahisi umeme kukatika kwenye njia ya Treni. Ameongeza kuwa,katika majaribio hayo walimeambatana pamoja na msemaji wa Serikali, wasanii, waandishi wa habari, wahariri na baadhi ya wafanyakazi wa TRC, ambapo treni hiyo inauwezo wa kutembea Km/h100-160. Kwa upande wake, Msamaji Mkuu wa Serikali Mohbare Matinyi amesema kuwa, ujio wa tren

TAWA IMELETA MAPINDUZI MAKUBWA KATIKA SEKTA YA UTALII KILWA - DC KILWA

Image
Na. Beatus Maganja Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Christopher Emil Ngubiagal amesema Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA ni taasisi iliyoleta mapinduzi makubwa katika Sekta ya Utalii na kuwa chanzo kikubwa cha mapato ya Serikali na wazawa wa wilaya hiyo kutokana na maboresho ya miundombinu ya utalii katika Hifadhi ya Urithi wa Dunia ya Magofu ya Kilwa kisiwani na Songo Mnara yanayopelekea watalii wengi kutembelea Hifadhi hiyo. Komredi Ngubiagal ameyasema hayo Februari 25, 2024 akizungumza na waandishi wa habari wilayani humo ikiwa ni siku moja baada ya meli iliyobeba watalii 146 kutia nanga katika Hifadhi ya Urithi wa Dunia ya Magofu ya Kilwa kisiwani na Songo Mnara. "Naipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa awamu ya sita kwa kuona sasa utalii katika wilaya ya Kilwa ni vyema tupeleke taasisi inayoitwa TAWA ili kusudi ikasimamie, ikaendeleze, ikaboreshe hii Sekta nzima ya utalii ya wilaya ya Kilwa" amesema M

WALIOFUNGA VING'ORA, NAMBA BANDIA, VIMULIMULI KWENYE MAGARI NA PIKIPIKI KIAMA CHAO CHAJA

Image
Na Mwandiahi wetu, Habari Plus, Dar Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani kimepiga marufuku wamiliki na madereva wote nchini kutoweka Ving'ora, Vimulimuli, Namba bandia na taa za kuongezwa kwenye magari na pikipiki kama kuna ulazima wa kufanya hivyo basi wanatakiwa kuomba ridhaa ya kupata kibali cha kufanya hivyo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani. Aidha, Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani kitaanza oparesheni kabambe ya kukamata magari yote na pikipiki ambayo si ya dharura na yamefungwa ving'ora bila kuzingatia utaratibu wa kisheria kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria na hatua kali zitachukulia dhidi yao ikiwemo kupelekwa mahakamani. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Kamanda wa kikosi cha Usalama Barabarani, DCP Ramadhan Ng'anzi amesema kuwa ni kinyume cha sheria kwa mtu yoyote kufunga king'ora katika gari au pikipiki bila kuzingatia utaratibu wa kisheria na kanuni za usalama barabarani zilizowekwa kwa mujibu wa sheria. "Wapo baa

ONGEZEKO LA MVUA MWEZI MACHI , TMA YATOA TAHADHARI

Image
Na Mwandishi wetu, Habari Plus, Dar Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) imetoa mwelekeo wa mvua za masika kwa msimu wa mwezi Machi hadi Mei kwa mwaka 2024 ambapo mvua zinatarajiwa kuwa wastanibhadi juu ya wastani katika maeneo mengi ya nchi yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dkt Lasdaus Chang'a amesema kuwa mvua za masika zinatarajiwa kuanza wiki ya nne ya mwezi febuari 2024 katika maeneo mengi, huku ongezeko la mvua likitarajiwa katika kipindi cha mwezi Machi 2024. "katika maeneo mengi mvua  zinatarajiwa kuisha katika wiki ya tatu na ya nne ya mwezi Mei 2024 katika maeneo mengi, huku miongoni mwa athari zinazotarajiwa kutokea ni pamoja na magonjwa ya mlipuko kutokana na uchafuzi wa maji, kina cha maji katika mito na mabwawa kinatarajiwa kuongezeka na vipindi vya unyevu wa kuzidi kiasi na mafuriko vinaweza kujitokeza na kuathiri ukuaji wa mazao na miundombinu ya kilimo"ame

TMA YAWANOA WANAHABARI KUELEKEA MASIKA 2024

Image
  Dar es Salaam; Tarehe 21, Februari 2024 Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imekutana na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali kujadili kuhusu utabiri wa msimu wa Masika (Machi –Mei) 2024, unaotarajiwa kutolewa tarehe 22 Februari 2024.  Utabiri huo ni mahususi kwa maeneo yanayopata mvua mara mbili kwa mwaka ambayo ni Dar es Salaam, Pwani, Kaskazini mwa Morogoro, Visiwa vya Unguja na Pemba, Tanga, Kilimanjaro,Arusha, Manyara,Simiyu, Mara, Geita, Mwanza, Shinyanga, Kagera na Kaskazini mwa Kigoma. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Chuo cha Biashara (CBE), Dar es Salaam, Tarehe 21/2/2024. Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi, Dkt. Ladislaus Chang’a, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi, alisema “Mkutano huu ni mwendelezo wa sehemu ya ushirikishwaji wa wanahabari katika kuandaa taarifa zinazolenga kuchochea matumizi sahihi ya huduma za hali ya hewa”.  Aidha aliendelea kusisitiza kuwa, uzingatiaj

KUELEKEA MASIKA 2024: TMA YAPONGEZWA KWA USHIRIKIANO NA WADAU

Image
  Na Mwandishi wetu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Mhe. Jaji Mshibe Ali Bakari ameipongeza TMA kwa kuendelea kushirikisha sekta mbalimbali nchini katika shughuli za utoaji wa huduma za hali ya hewa. Alibainisha hayo wakati akifungua rasmi Mmkutano wa 24 wa Wwadau wa Uutabiri wa msimu wa mvua za Masika (Machi hadi Mei), 2024 uliofanyika katika ukumbi wa PSSSF, Dodoma, Tarehe 19/2/2024. “Tunapoelekea kutoa utabiri wa mvua za Masika 2024, lengo kuu la kukutana hapa ni kuwezesha matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa kwa wote na kwa wakati, ninapenda kuipongeza Mamlaka ya Hali ya Hewa kwa kuendelea kushirikisha wadau mbalimbali katika shughuli zao za utoaji wa huduma za hali ya hewa ambazo ni pamoja na utabiri wa misimu ya mvua.  Ushirikiano huu ni mfano wa kuigwa na unafaa kuendelea hasa katika kipindi hiki ambapo dunia pamoja na nchi yetu inakabiliwa na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa”. Alisema Mh.Jaji Bakari “Tunapojiandaa kupokea taarifa ya u

RELAXO MPYA YAZINDULIWA DAR, SERIKALI YAWAHAKIKISHIA USALAMA WAWEKEZAJI

Image
   Na Mwandishi wetu, HabariPlus, Dar Kampuni Best Brand Distributor leo wamefungua duka jipya la tatu la viatu vya Relaxo aina zote 'show room' mtaa wa Morogoro /Samora ambapo ya kwanza lipo Mlimani Cty na la pili Mtaa wa Nkurumah eneo la kati kati ya jiji Clock Tower. Akizungumza jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Best Brand Distributor Khalid Salim amesema kuwa lengo la Kampuni hiyo ni kufungua maduka mengine 20 ifikapo 2025 huku akiahidi kuwa kama soko la bidhaa hizo litakua rafiki wanatarajia kufungua kiwanda kwa ajili ya kuzalisha bidhaa hizo nchini Tanzania. Aidha, amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluh Hassan kwa kuwezesha kuwa na mazingira mazuri kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kwa maslahi mapana zaidi ya nchi ya Tanzania. Awali akikata utepe katika duka hilo kama ishara ya uzinduzi wa show room hiyo Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omar Kumbilamoto amesema Serikali inawahakikishia kuboresha mazingira ya usalama kwa wawekezaji