BABU OWINO ATOA RAI KWA VIJANA WA ACT WAZALENDO, NONDO NAE YUPO


Na Mwandishi wetu, Habari Plus Dar

MBUNGE wa Jimbo la Embakasi Mashariki Nairobi, Kenya Poul Owino amewataka vijana nchini Tanzania kupigania kupata haki zao katika kulitetea taifa lao pamoja na kuwa viongozi bora kwa maslah mapana ya Taifa.

Rai hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam mapema leo wakati alipokua akifungua kongamano la Ngome ya Vijana lililokwenda sambamba na uchaguzi wa viongozi mbalimbali ikiwemo nafasi ya Mwenyekiti, Makamo Mwenyekiti, Katibu, pamoja nafasi nyengine mbalimbali.

Amesema kuwa, Chama cha ACT Wazalendo ni cha kuigwa kutokana na kuwa chama bora chenye mfumo imara wa kupigania haki na kuwalea vijana ambao wana uwezo wa kukipigania kwa  maslahi ya Taifa kwa ujumla.

"Vijana ni Taifa la leo sio la kesho, mapambano yanatakiwa kuanza leo,  hivyo usikuabali kukaa kimya kwani usipokubali kuwa kwenye meza ukala utakua menu uliwe, vunja hiyo meza usipokua sehemu yao, Hayyat Mwalim Julias Nyerere, Kawawa na Kwame Nkuruma wangekua waoga unadhani uhuru ungepatikana? "amehoji Dkt Babu Owino.

Akitoa nasaha za Chama cha ACT Wazalendo, Katibu Mkuu Ado Shaibu amewataka wajumbe wa mkutano huo kuchagua viongozi ambao wataweza kuwaongoza wananchi, kukitetea na kukijenga Chama hicho kwani hilo ndio lengo la chama namba moja katika kuanzisha taasisi ndani ya chama.

Aidha, amesema kuwa, Chama hicho kinawategemea sana vijana kwani wamekua wakiwalea kwenye misingi iliyoimara ya uongozi na kimewaamini ndio maana hawategemei wanachama ambao wanatoka kwenye vyama vyengine kwenda kujinga kwao bali wanachagua viongozi waliowalea wenyewe.

"Kwa miaka minne mfululizo Chama chetu kimeachana na tabia ya kusubiri wanachama waliohama vyama vyao ili kuja kuwapa uongozi bali tunachagua viongozi ndani ya chama kwani wamewalea vizuri, na tunawaamini katika kusimamia katiba hivyo lazima mchague watu ambao wataweza kuwasimia vizuri katika kutatua changamoto za wananchi" amesema  KM Ado.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana Taifa, Abdul Nondo amewataka vijana kuwa tayari katika kukipigania chama na kutokuwa waoga, kwani Hayyat Mwalim Nyerere angekua muoga taifa la Tanzania lisingepata uhuru ili kuwa viongozi bora ni lazima ujitoe kwa taifa lako na kuwatumikia wananchi waliokuamini na kukuchagua.

Aidha, amesema kuwa, asilimia 75 ya watanzania ni vijana hivyo wanatakiwa kusimama imara kushiriki nafadi mbalimbali za uongozi si tu kujenga Chama bali hata kupigania maslahi ya wananchi kwani changamoto nyingi zinapotokea zinawakumba vijana.

Miongoni mwa wageni walioalikwa katika mkutano huo ni pamoja Katibu wa Cha Juvicuf ambapo amesema vijana wanahitaji kuwa na sauti ya pamoja ili kuhakikisha wananchi wanatetewa kwenye changamoto zao.







Comments

Popular posts from this blog

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU NDIO USHAURI WA TMA KWA SEKTA HIZI ...