Posts

Showing posts from June, 2025

MASELE MASUNGA ATIA NIA UBUNGE SEGEREA

Image
Kada wa Chama Cha Mapinduzi Masele Masunga amechukua fomu kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Segerea.  Masunga amekabidhiwa fomu hiyo Juni 30,2025 na Katibu CCM Wilaya ya Ilala Sylvester Yared.  Amesema kuwa amepata msukumo kutoka kwa Wananchi wa Jimbo hilo kumtaka agombea kwa madai kuwa bado kuna mambo yanatakiwa kuongezewa nguvu ili kuwaletea maendeleo wananchi. Ameongeza kuwa kuna matatizo mbalimbali yanayoilikabili Jimbo hilo ikiwemo ukosefu wa ajira kwa Vijana,pamoja na miundombinu ya Barabara.

MJUMBE WA HALMASHAURI KUU KATA YA LIWITI ACHUKUA FOMU YA UDIWANI VITI MAALUM

Image
Mjumbe wa Halmashauri kuu Jumuiya ya Wazazi kata ya Liwiti Segerea Hindu Ally Senyange amechukua fomu ya kugombea Udiwani Viti maalumu Halmashauri ya Ilala.  Hindu amekabidhiwa fomu hiyo leo Juni 30,2025 na Katibu Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya ya Ilala Rosemary Mwakisalu Senyange amesema kwamba ameamua kugombea nafasi hiyo ili kuunga mkono jitihada zianazofanywa na Mwenyekiti Taifa wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea maendeleo Watanzania.

TUWE NA MAONO YA KUIONA KESHO YETU – DKT. BITEKO

Image
  Ni katika Bonanza la Wizara ya Nishati na Taasisi zake Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Taasisi zake kuwa na maono ya kuweza kuona mbali hali itakayowasaidia  katika utendaji wa kazi na kupata suluhisho ya changamoto zinazoweza kutokea kabla ya changamoto hizo kutokea. Dkt. Biteko ameyasema hayo leo Julai 28,2025 katika viwanja vya Jamhuri  Jijini Dodoma, wakati akizungumza na watumishi wa wizara na Taasisi zake wakati wa kufunga Bonanza la michezo mbalimbali lililohusisha Wizara ya Nishati na Taasisi zake.

MFAMASIA RAGI ACHUKUA FOMU YA UBUNGE UKONGA

Image
Kada wa Chama cha Mapinduzi CCM ambaye amewahi kuwa Rais wa Wanafunzi Chuo kikuu Cha kimataifa Cha Kampala nchini Tanzania mwaka 2018/20 Mfamasia Ragi Samweli amechukua fomu kugombea Jimbo la Ukonga. Kada huyo amekabidhiwa fomu hiyo leo June 30,2025 na Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ilala Sylvester Yaredi katika Ofisi ya CCM wilaya ya Ilala.

MWINJUMA AUTAKA UBUNGE KIVULE

Image
Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa Kipunguni Mwinjuma Abdul Seke amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Ubunge Jimbo la Kivule. Seke amekabidhiwa fomu hiyo leo June 30,2025 na Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ilala Sylvester Yaredi. Aidha Seke amesema endapo atapata ridhaa ya kugombea katika Jimbo hilo atahakiksha anaunga mkono jitihada za Rais Dkt Samia Suluh Hassan za kuwaletea Maendeleo.

MALYA ACHUKUA FOMU YA UDIWANI VITI MAALUM

Image
Katibu wa Shina na mwanachama wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM,( UWT) Kigezi chini Kata ya Buyuni, Happyness Malya amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Udiwani wa Viti Maalumu  Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Amekabidhiwa fomu hiyo leo June 30,2025 na Katibu Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Wilaya ya Ilala Rosemary Mwakisalu Ofisini kwake Ilala

RAIS WA SHIRIKISHO LA FILAM TANZANIA ALITAKA JIMBO LA SEGEREA

Image
Rais wa Shirikisho la Filam Tanzania Rajab Amiry leo June 30,2025 amerudisha fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Ubunge Jimbo la Segerea . Rajab Amiry amekabidhiwa fomu hiyo June 28 na Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala Sylvester Yaredi katika Ofisi za Chama Wilaya ya Ilala. Aidha amesema amejitathimni ameona ana sifa ya kugombea nafasi hiyo, kwani Chama hicho kimetoa fursa kwa kila mwanachama kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO

Image
 

NGOWI AUTAKA UBUNGE KIVULE

Image
Mjasiriamali Agustino Ngowi leo June 29,2025 ametimiza haki yake ya kikatiba amefika katika Ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Jimbo la Kivule Amekabidhiwa fomu hiyo Mapema leo hii na Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ilala Chief Sylvester Yaredi katika Ofisi za Chama cha Mapinduzi . Aidha amesema endapo atapewa ridhaa kugombea Jimbo hilo atashirikiana na wananchi katika kutatua kero zinazowakabili ikiwemo miundombinu ya barabara.

MWENEZI TAWI LA NANE NANE MSONGOLA ACHUKUA FOMU YA UBUNGE KIVULE

Image
Mchumi na Mkurugenzi Wa Kamarlon Microfinance, Mwezeshaji Wa Wafugaji wa Kuku na Mwenezi Wa Tawi la CCM Nane nane Kata ya Msongola Florian Karugaba amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Ubunge Jimbo la Kivule kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM). Karugaba amechukua fomu mapema leo Juni 29,2025 na kukabidhiwa na Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Ilala, Sylvester Yeredi.

KHIMJI ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA KATA YA ILALA

Image
Mjumbe wa Baraza kuu la wazazi CCM Taifa Saady Khimji (Home Boy) leo June 29,2025 amechukua fomu ya kugombea Kata ya Ilala akitetea kiti chake

SIDODO ACHUKUA FOMU YA UDIWANI VITI MAALUM

Image
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kata ya Ukonga Wilaya ya Ilala Magreth Sidodo amechukua fomu ya kugombea Udiwani wa Viti maalumu.  Magreth Sidodo amekabidhiwa fomu hiyo na Katibu Umoja wa Wanawake (UWT) wilaya ya Ilala Rosemary Mwakisalu Ofisini kwake Ilala Dar es salaam.  Magreth Sidodo amesema ametumia haki yake kikatiba ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi hiyo ili kuunga mkono jitihada zinazofanywa Mwenyekiti Taifa wa Chama hicho na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea maendeleo watanzania.

WAKILI MSOMI MANDESI ACHUKUA FOMU YA UBUNGE SEGEREA

Image
Mkurugenzi wa Mandesi Wakili Msomi Gidioni Mandesi amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Jimbo la Segerea . Amekabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ilala , Chief Sylvester Yared mapema leo hii

MSAMA ALITAKA JIMBO LA UKONGA

Image
Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama leo Juni 29, 2025 amefika katika Ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala na kuchukua Fomu ya Kugombea Ubunge Jimbo la Ukonga. Amekabidhiwa Fomu hiyo na Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Ilala, Chief Sylvester Yaredi.

RAIS SAMIA ATAJA MAFANIKIO SEKTA YA NISHATI 2020-2025

Image
Ni wakati akihitimisha shughuli za Bunge jijini Dodoma JNHPP, Umeme Vijijini, Umeme wa Gridi Kigoma na  Katavi; Ni baadhi ya Vielelezo vya mafanikio Ataja miradi mikubwa ya usafirishaji umeme iliyokamilika Ataka TANESCO  kuanza kuiangalia  Nyukilia kama moja ya vyanzo vya kuzalisha umeme nchini. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameeleza kuwa Sekta ya Nishati imekuwa na mafanikio makubwa  katika kipindi cha miaka mitano.  Ameyasema hayo wakati akihitimisha shughuli za Bunge Jijini Dodoma tarehe  28 Juni 2025. "Mheshimiwa Spika kutokana na umuhimu wa Sekta ya Nishati kwa maendeleo ya nchi, Serikali imeimarisha upatikanaji wa nishati nchini ikiwemo kukamilisha mradi wa bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere (JNHPP)”. Amesema Mhe. Samia Ameongeza kuwa, mbali ya kukamirisha mradi wa Julius Nyerere pia Serikali imekamilisha upelekaji wa umeme katika Vijiji vyote 12,318  nchini. Ameongeza kuwa, msukumo uliofanywa na Serik...

TFS YAPONGEZWA KWA KUTANGAZA HISTORIA NA MAZINGIRA BAGAMOYO

Image
Na Mwandishi Wetu  Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe Shaibu Ndemanga, ameipongeza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa kazi nzuri ya kuendeleza utalii wa kihistoria na uhifadhi wa mazingira, akibainisha kuwa juhudi hizo zimechangia kuongeza pato la wananchi na kuvutia wageni wilayani humo. Mhe. Ndemanga ametoa pongezi hizo leo Juni 25, 2025 wakati wa mapokezi ya Mjumbe wa Bodi ya TFS, Bi Piencia Kiure, aliyekuwa katika ziara ya siku ya pili ya kikazi Kanda ya Mashariki kwa kutembelea maeneo ya uhifadhi katika wilaya za Bagamoyo (Pwani) na Kinondoni (Dar es Salaam). “Nawapongeza TFS kwa miradi inayoleta manufaa ya moja kwa moja kwa wananchi. Ukarabati wa maeneo ya kihistoria kama Kaole na Bagamoyo Mjini Mkongwe si tu kuwa unahifadhi urithi wetu, bali pia unachochea utalii wa ndani na kimataifa,” alisema Mkuu huyo wa wilaya. Akiwa Bagamoyo, Bi Kiure alitembelea Makumbusho ya Kale ya Kaole na Mji Mkongwe wa Bagamoyo, ambapo alikagua miradi mbalimbali ya TFS ikiwemo ujenzi wa nj...

DKT. BITEKO AZIPONGEZA SSF NA TOTAL ENERGIES KUFIKIA VIWANGO VYA JUU VYA USALAMA VYA USAFIRISHAJI

Image
Asema Serikali inaweka sera za kulinda na kuvutia wawekezaji Wenye malori watakiwa kuweka vifaa vya usalama Rais Samia apongezwa kwa kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji nchini  Wasafirishaji watakiwa kuzingatia usalama barabarani Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amezipongeza Kampuni za Total Ernergies na Super Star Fowarders – SSF  kwa kuweza kufikia viwango vya juu vya usalama vya usafirishaji huku akiwataka wasafirishaji wengine kufuata  nyayo zao kwa kuwa kampuni hizo ni mfano mzuri wa kuigwa. Dkt. Biteko amesema hayo Juni 25, 2025 jijini Dar es salaam wakati akishiriki katika maadhimisho ya miaka 30 ya ushirikiano kati ya Kampuni ya Super Star Fowarders (SSF) na Total Energies.   “ Leo tumekusanyika hapa kusherehekea hafla ya miaka 30 ya ushirikiano baina ya Kampuni zetu hizi mbili za Total Ernergies na Super Star Fowarders. Katika kipindi hicho chote, mmekuwa washirika wakubwa wa k...

WANAOTAKA KUHARIBU UCHAGUZI MKUU WAONYWA, VIJANA WA CCM WACHARUKA

Image
Na Mwandishi wetu Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam wamewaonya wanasiasa na wanaharakati wanaohamasisha wananchi wasishiriki Uchaguzi Mkuu kwani ni dai la kikatiba na sio matakwa ya mtu binafsi. Akizungumza na  Waandishi wa habari Makao Makuu ya UVCCM Jijini Dar es salaam,mmoja wa Vijana hao Isack Sumbali amesema kuwa mabadiliko ya Sheria ya Uchaguzi yamefanyika kwa kiasi kikubwa ikiwemo Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) kubadilishwa nakuwa Tume huru ya Taifa ya  Uchaguzi(INEC). Amesema kuwa, tume miongoni mwa mabadiliko ni pamoja na kua na uhuru wa vyanzo vya mapato, ambapo awali ilikua haiwezi kujiendesha kwa fedha za ndani,na kutegemea ufadhili kutoka UNDP, ambapo uchaguzi mkuu wa mwaka huu utagharamiwa na fedha za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha Sumbali amesema kuwa kwa sasa Uhuru wa Tume hiyo umeongezeka katika sehemu kuu mbili ambazo ni uhuru wa kitaasisi na uhuru wa kiutendaji,pamoja na kutungwa Sheria maalumu inayoongoza kupatikana kwa...

TANESCO YAWAPA SOMO WENYEVITI WA MITAA WILAYA YA KINONDONI NA UBUNGO

Image
Shirika la umeme TANESCO leo limekutana na wenyeviti wa mitaa kutoka Wilaya ya Kinondoni na Ubungo lengo ikiwa ni kutoa elimu kwa watendaji hao kwani shirika hilo asilimia kubwa utendaji unaanzia kwenye mitaa. Akifungua kikao kazi hicho, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Altbert Chalamila  kilichoandaliwa na TANESCO kwa ajili ya Wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Halmashauri za Manispaa ya Kinondoni na Ubungo amesema wenyeviti wa Serikali za mitaa ni wadau muhimu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Serikali kwa kuwa miradi hutekelezwa katika maeneo yao. "Hata miradi mingi ya TANESCO iko kwenye mitaa hivyo, ni imani yangu kuwa kupitia kikao kazi hiki wenyeviti wote wanakwenda kuwa mabalozi wa kueleza huduma nzuri zinazotolewa na TANESCO pia kulinda miundombinu ya Shirika hilo"amesema RC Chalamila. Aidha ameipongeza TANESCO kwa kuona umuhimu wa kukutana na kundi hilo muhimu ili liweze kufahamu kwa kina majukumu ya shirika hilo lakini pia kutoa mawazo na ushauri wa namna b...