SIDODO ACHUKUA FOMU YA UDIWANI VITI MAALUM
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kata ya Ukonga Wilaya ya Ilala Magreth Sidodo amechukua fomu ya kugombea Udiwani wa Viti maalumu.
Magreth Sidodo amekabidhiwa fomu hiyo na Katibu Umoja wa Wanawake (UWT) wilaya ya Ilala Rosemary Mwakisalu Ofisini kwake Ilala Dar es salaam.
Magreth Sidodo amesema ametumia haki yake kikatiba ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi hiyo ili kuunga mkono jitihada zinazofanywa Mwenyekiti Taifa wa Chama hicho na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea maendeleo watanzania.
Comments
Post a Comment