Katibu wa Shina na mwanachama wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM,( UWT) Kigezi chini Kata ya Buyuni, Happyness Malya amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Udiwani wa Viti Maalumu Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Amekabidhiwa fomu hiyo leo June 30,2025 na Katibu Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Wilaya ya Ilala Rosemary Mwakisalu Ofisini kwake Ilala
Makamu wa RAIS wa Seneti ya Jumuiya (SMAUJATA) shujaa wa maendeleo wa ustawi wa Jamii Fredrick Nelson Rwegasira amechukua fomu ya kutia nia ya kugombea Ubunge Jimbo la Kivule. Rwegasira amechukua fomu hiyo leo Julai 1,2025 katika Ofisi za Katibu wa CCM Ilala Chief Sylvester Yaredi. Aidha amesema kwamba amejipima na kujitambua kua anafaa kugombea nafasi hiyo kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Kivule.
Na Mwandishi wetu Chama Cha National League For Democracy (NLD) leo kimezindua kampeni maalum yaKkukiondoa chama Cha Mapinduzi madarakani "fyeka CCM" ambapo imelenga kuzunguka mikoa 10 ya Tanzania ikiwemo Tanga, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Singida, Dodoma na Mwanza. Akizungumza na waandishi wa habari na wanachama wa chama hicho, jijini Dar es Salaam kwenye makamo makuu ya chama hicho, Katibu Mkuu Doyo Hassan Doyo amesema kuwa, chama hicho kina sera nzuri ambazo zinawabeba wananchi hasa katika kuwakomboa na umaskini. Aidha, uzinduzi wa kampeni hiyo umeenda sambamba na kuwapokea wanachama wapya kutoka chama Cha ACT -Wazalendo na ADC ambapo amesema kuwa, kupitia kampeni hiyo watategeneza wagombea ambao wataweza kushindana kwa hoja, huku akiwataka viongozi na wanachama kutumia lugha nzuri wanapokuwa majukwaani na kufanya siasa za kistarabu. "Siasa lazima zifanyike katika mazingira yanayoheshimika ..wanasiasa tuheshimiane .. wanasiasa tusifanye kiburi kwa viongozi ambao wako mad...
Comments
Post a Comment