RC MAKALLA ATOA AGIZO HILI KWA WAFANYABIASHARA MBAGALA
Na mwandishi wetu, HPMedia, Dar es Salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla Leo amefanya Zoezi la usafi Wilaya ya Temeke eneoa la Mbagala ambapo amepiga marufuku ufanyaji Biashara kwenye ujenzi wa Barabara ya mwendokasi na maeneo yaliyokatazwa.
Akizungumza na wananchi wakati akifanya zoezi hilo, amewakumbusha wananchi na viongozi kuanzia ngazi ya mtaa hadi Wilaya kuhakikisha wanasimamia usafi kila jumamos ya mwisho wa mwezi ili kuhakikisha maeneo yote ya jiji la Dar es salaam yanakua masafi.
Aidha, amewaelekeza Wakurugenzi kusimamia Wakandarasi kuondosha taka kwa wakati na Wakandarasi watakaoonyesha kulegalega wasipatiwe mkataba.
Pamoja na hayo amewapongeza Wananchi kwa mwamko Mkubwa wa kufanya usafi jambo lililopelekea Jiji la Dar es salaam kushika nafasi ya sita kwa usafi Barani Afrika na kuondosha magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindipindu.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Dar es salaam, zaidi ya shilingi bilioni 3.2 zimetolewa kama mkopo kwa Wafanyabiashara Wanaofanya biashara kwenye Maeneo rasmi na kutoa wito kwa Wafanyabiashara wengine kuacha kufanya biashara holela.
Comments
Post a Comment