HESLB YAWATAKA WANUFAIKA KUREJESHA MIKOPO, YAZINDUA KAMPENI MAALUM KUWASAKA


Na Mwamdishi wetu,HabariPlus

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ( HESLB) leo imezindua kampeni yake ya kwanza ya Fichua "Kuwa Hero wa Madogo"ambayo imelenga kuhamasisha wanufaika wa mikopo hiyo ili na wengine waweze kusoma kupitia bodi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akizindua kampeni hiyo Mkurugenzi Mtendaji Bill Kiwia amesema kuwa kampeni hiyo itadumu kwa miezi miwili lengo ikiwa ni kuhamasisha watanzania kuwafichua wanufaika wote ambao ambao wamepata mikopo hiyo ili na wengine waweze kutimiza ndoto zao za kusoma.

Amesema kuwa, kampeni hiyo ni ya kizalendo ambayo inawataka wadaiwa wote ambao wamemaliza kusoma na wameajiriwa na wale ambao hawajaariwa wapo mtaani hawajalipa kurejesha pesa hizo, huku wakiahidi wapo tayari kupokea maoni ili kuendelea kufanya vizuri zaidi kwa awamu inayofuata.

"Kuna wanufaika wa mikopo hii wengi wapo mtaani na hawajalipa, tunawaomba warejeshe mikopo hii ili wengine wenye mahitaji waweze kunufaika na wao, hii kampeni ni endelevu tutatumia njia mbalimbali kuweza kuwafikia ikiwemo mitandao ya kijamii, Tv na Radio"amesema Kiwia.

Aidha, akizungumzia hali ya urejeshaji wa mikopo, Kiwia amesema ipo vizuri ambapo imeongezeka kutoka shill bill 2 kwa mwezi kwa mwaka 2016 hadi kufikia shill bill 15 kwa mwezi kwa mwaka 2024 kutoka kwa wanufaika 220,000 ambapo wengine wameajiriwa na wengine bado.

Amesema kuwa, ukusanyaji wa mikopo Tanzania imefikia asilimia 70 ambapo Amerika ya Kusini wapo kati ya asilimia 50 hadi 55, hivyo Tanzania ipo juu kwa Afrika katika ukusanyaji wa marejesho ya mikopo ya wanafunzi .

Comments

Popular posts from this blog

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU NDIO USHAURI WA TMA KWA SEKTA HIZI ...