ACB PLC YAZINDUA VIUNGA VILIVYOBORESHWA VYA INDEPENDENCE SQUARE, DODOMA

 Na Mwandishi wetu

 Meneja wa tawi la Benki ya Akiba Dodoma Upendo Makula amesema benki hiyo imepunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya karatasi kwa kuboresha huduma zake za kidijitali, zikiwemo Akiba Mobile, Akiba Wakala, kadi za VISA, taarifa za kielektroniki (E-statement), na huduma za benki Mtandao (Internet Banking).

Kauli hiyo ameitoa katika hafla ya kukabidhi awamu ya pili ya uboreshaji wa viwanja vya independence square ambapo amesema jitihada za benki hiyo ni kubwa katika  kujitolea kuhifadhi na kutunza mazingira.

Amesema kuwa, huduma hizio si tu kwamba zinapunguza matumizi ya karatasi, bali pia huleta urahisi na uhakika, hivyo kukidhi mahitaji ya soko kwa ufanisi. 

Aidha, benki hiyo inatoa huduma mbalimbali kama mikopo, akaunti na bima, zinazowafikia wateja tofauti kuanzia mtu binafsi hadi makampuni makubwa na taasisi za serikali.

Samba samba na kaulimbiu ya Siku ya Mazingira Duniani ya mwaka huu, isemayo “Our Land, Our Future” - “Ardhi Yetu, Mustakabali Wetu,” ambayo  imebebwa na mada  kuu ya “Land restoration, desertification and drought resilience”  ambayo  inalenga urejeshaji (utunzaji) wa ardhi, kupambana na uzalishaji wa majangwa, na ukame. 

Katika tukio muhimu lililofanyika sambamba na Siku ya Mazingira Duniani tawi la Dodoma la Benki ya Akiba  lilikabidhi rasmi awamu ya pili ya uboreshaji wa viwanja vya Independence Square. 


Ameongeza kuwa na kusisitiza juu ya wajibu wa pamoja wa kulinda na kuhifadhi mazingira ili kuhakikisha dunia inabaki kuwa mahali salama pa kuishi kwa  sasa na vizazi  vijavyo.

Aidha, Makula alieleza kuwa Benki ya Akiba inashiriki kikamilifu katika uhifadhi wa mazingira kwa namna mbali mbali kuanzia kupitia huduma zake na ushiriki wa katika shughuli mbali mbali za kijamii.  

Ameongeza kuwa, Akiba Commercial Bank inashiriki kikamilifu katika shughuli za jamii za kuhifadhi mazingira kama sehemu ya Sera yake ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR). 

"Mfano halisi ni jitihada zake za muda mrefu za kutunza na kuboresha viwanja vya Independence Square huko Dodoma, jukumu ambalo limekuwa likitekelezwa kwa zaidi ya miaka kumi, juhudi hizi zinaonyesha nia thabiti ya benki hiyo ya kutunza  na kuhifadhi mazingira   kwa ajili ya urithi bora wa vizazi vijavyo"amesema Makula.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya Dodoma Alhaj Jabir Shakimweri aliipongeza Benki ya Akiba kwa juhudi na jitohada zake katika kuboresha na kuhifadhi mazingira, pia ametoa rai kwa taasisi nyingine kuiga mfano wa Akiba. 

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Silvest Arumasi, pamoja na uongozi na wafanyakazi wote wa tawi la Dodoma, alisisitiza nia ya benki hiyo ya kuendelea kusaidia uboreshaji wa mazingira na miradi mingine ya kijamii, hasa katika sekta za afya na elimu.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaji Jabir Shakimweri, wawakilishi mbalimbali wa vyombo vya habari, na wafanyakazi wa Benki ya Akiba Commercial.

Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI