DOYO AJITOSA KUWANIA UENYEKITI ADC
Na Mwandishi wetu
Ikiwa ni siku chache baada ya Mwenyekiti wa Chama chaAllience for Democratic Change, ADC, Hamad Rashid kutangaza kuachia nafasi hiyo kwa mujibu wa katiba, amejitokeza Katibu Mkuu wa chama hicho Doyo Hassan Doyo kuwania nafasi hiyo.
Akizungumza mbele ya waandishi wa Habari Katibu Mkuu wa Chama hicho, Doyo Hassan amesema amesema ameamua kuwania nafasi hiyo kutokana na uzoefu aliona ndani ya chama hicho ambapo atachukua fomu hiyo Jun 11 mwaka huu.
"Sababu kubwa ambayo imenifanya kuwania nafasi hii ni kutokana na kuwa na uzoefu wa kutosha baada ya kulelewa vema na aliyekuwa Mwenyekiti wetu, Hamad Rashid.
Ameongeza "Nimekaa na Mwenyekiti wetu kwa muda wa miaka 10 nikiwa Katibu Mkuu na sikuwahi hata siku moja kutofautiana naye na nimejifunza mengi ikiwemo suala uvumilivu na kuheshimu Katiba, ambayo ameitekeleza kwa vitendo kwa kuondoka madarakanj kwa mujibu wa sheria tulizojiwekea," amesema.
Amefafanua kuwa katika chama hicho ameweza kufanya kazi na viongozi mbalimbali, akiwemo Mwenyekiti wa kwanza, Said Bilal huku Doyo akiwa Mkurugenzi wa Habari.
Pia amefanya kazi na Lucas Silimu aliyekuwa Katibu Mkuu wakati huo, Mama Lydia Bendera (Katibu Mkuu), Juma Kilagai (Katibu Mkuu) na Abubakari Rakesh.
Aidha, amewataka wanachama wa chama hicho kutokuwa na wasiwasi naye katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Juni 27 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Ameongeza kuwa ikiwa atafanikiwa kushika nafasi hiyo, moja ya mikakati yake ni kukiimarisha chama kiwe kikuu cha upinzani na kifanye vizuri bungeni na kuisimamia vema Serikali maslahi ya Watanzania.
Amesema kuwa, ikiwa atafanikiwa kukaa katika kiti hicho atabeba agenda tatu ambazo ni mabadiliko ya sheria, mabadiliko ya ajira ambayo itafanya wanafunzi kupata elimu bora itakayowasaidia maishani na agenda ya maisha bora kwa mtanzania.
Aidha, akitangaza kuwania nafasi hiyo aliambatana na anayegombea umakamu uenyekiti, Scolastica Kahana aliyekuwa mgombea ubunge wa chama hicho katika Jimbo la Kibaha Mjini katika uchaguzi wa mwaka 2020.
Hata hivyo, ametoa wito kwa wana siasa ambao wameshindwa kwenye chaguzi wa ndani ya vyama kujiunga na ADC ili kuongeza nguvu ya kufanya vema kwenye chaguzi, zijazowa Serikali za Mitaa Oktoba mwaka huu na uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwakani.
"Ni vizuri hata ndg yetu Peter Msigwa ambaye amshindwa kwenye uchaguzi wa ndani wa chama, kama itampendeza anaweza kujiunga kwetu na ninaaminj attuingezea nguvu kubwa kwenye ushindani wa siasa ya vyama vingi," amesema.
Comments
Post a Comment