MAKONDA AWAJIA JUU TANESCO, ATOA RAI KWA WANANCHI
Na fatma Ally, Habari Plus Media
KATIBU wa Itikadi na Uenezi Paul Makonda amelitaka shirika la umeme Tanesco kujitafakari upya kwa hali ya ukatikaji wa umeme ovyo ambapo imekua ni changamoto kubwa jambo ambalo limekua linarudisha nyuma harakati kubwa za maendeleo kwa taifa.
Kauli hiyo, ameitoa leo jijini Dar es Salaam wakati alipokua akitoa tathmini ya robo mwaka ya chama cha mapinduzi amesema kuwa, hivi karibuni Tanesco wamemuahidi Rais Samia ya kwamba ifikapi Januari kuwa kinu cha umeme kitawashwa hivyo ni vyema ahadi hii ikatekelezwa kwa vitendo.
Aidha amewataka watendaji wote kuanzia ngazi shina hadi mkoa kusikiliza kero za wananchi Ila kutatua changamoto zinazowakabili na sio kukaa ofisini
"Nataka niwakumbushe ndugu viongozi tuliopewa dhamana na Rais Samia ya kuwatumikia wananchi ni vyema tukatekeleze wajibu wetu tusisubiri mpaka Rais Samia anzishe ziara aanze kasimamishwa njiani na wananchi ili watoe malalamiko yao"amesema Makonda.
katika hatua nyengine amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika suala la utoaji wa maoni ya dira ya Maendeleo ya Taifa ya miaka 30.
"Niwaombe wananchi kujitokeza kwa wingi katika suala zima la utoaji wa maoni ya nini wanachotaka kiwekwe, na mpango huu utawafikia wananchi wote kwa sababu tayari tume maalum imewekwa kwa ajili ya kukusanya maoni hayo"amesema Makond
Akizungumzia suala la kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa Makonda amesema ni vyema wanachama wenye nia ya kugombea uongozi kuacha viongozi waliopo madarakani waendelee kutekeleza majukumu yao kwa kuwa wao bado ni viongozi halali wanaotambulika kisheria.
"Najua wapo watu ambao wameanza kampeni za hapa na pale mimi niwambie tu ndugu zangu waacheni viongozi wafanye kazi kwa sababu muda wao haujaisha na wao bado ni viongozi wanaotambulika na bado wanahaki ya kuwatumikia wananchi", amesema Makonda.
Hata hivyo Pauli Makonda amebainisha kuwa kuanzia Januari 13 /2024 ataanza ziara ya kikazi katika mikoa 10 ikiwemo Tanga, Pwani,Kilimanjaro,Arusha,Manyara,Singinda,Tabora,Shinyanga na Simiu.
Aidha kupitia ziara hoyo amewataka watendaji wa halmashauri zote watakaopitiwa na ziara hiyo waanze kujitathmini kabla ya kiongozi huyo kupita maeneo hayo.
Comments
Post a Comment