WAZIRI WA UCHUKUZI WA JAPAN KUFANYA ZIARA NA UJUMBE WA WATU 40 NCHINI TANZANIA

 


Na mwandishi wetu

Waziri wa Ardhi, Miundombinu, Uchukuzi na Utalii wa Japan, Mhe. Konosuke Kokuba anatarajia kufanya ziara ya kikazi nchini mnamo mwezi Januari mwaka 2024.

Katika ziara hiyo, Mhe. Kokuba ataongozana na ujumbe wa watu 40 kutoka kampuni binafsi zinazojihusisha na masuala ya miundombinu na baadhi ya watumishi wa Wizara yake.

Ziara hiyo imelenga kujadili fursa mbalimbali zinazotokana na ushirikiano kati ya Tanzania na Japan katika maendeleo ya miundombinu.

Hayo yamejiri katika kikao cha pamoja cha maandalizi ya ziara hiyo kilichoshirikisha viongozi wa Wizara ya Uchukuzi na Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Bwana Plasduce Mbossa pamoja na Menejimenti yake kilichofanyika jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara.

Kwa upande wa Japan, ujumbe wake uliongozwa na Bwana Yoshihiro Kakishita kutoka Sekretarieti ya Wizara ya Ardhi, Miundombinu, Uchukuzi na Utalii ya Japan.

Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Bwana Plasduce Mbosaa ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Japan kuja kuwekeza kwa upande wa miundombinu ya Bandari nchini.

Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI