SERIKALI KUKUZA BUNIFU, COSTECH YAJIVUNIA

 


Na Mwandishi wetu, HabariPlus,Dar

Serikali imesema itaendelea kusapoti bunifu zote zinazofanywa na watu mbalimbali, huku ikiahidi kukuza sayansi kwa lengo la kuchagiza maendeleo chini Tanzania.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Sayansi na Teknolojia kutoka Wizara ya elimu sayansi na Teknolojia Profesa Ladslaus Mnyone wakati akimuwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Nombo katika mdahalo maalum uliowakutanisha wahariri, waandishi wa habari na wadau wa ubunifu, ulioandaliwa na Tume ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (COSTECH) chini ya programu ya ufunguo.

Amesema kuwa, pia Serikali itahakikisha inakuza sayansi, teknolojia na ubunifu, lengo ikiwa kusaidia kufanyika kwa tafiti zinazojibu changamoto za watanzania, katika kuhakikisha sekta ya teknolojia na ubunifu inakua huku ikikamilisha mkakati wa teknolojia ya TEHAMA

Kwa upande wake,  Mkurugenzi wa COSTECH Dk.Amos Nungu, amesema wiki ya ubunifu, costech na wadau wa maendeleo wanajivunia mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na uwepo wa uelewa wa pamoja ulioleta matokeo chanya.

Amesema kuwa, wiki ya bunifu itazinduliwa leo katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julias Nyerere (JNICC), huku kilele chake kikitarajiwa kufanyika mkoani Tanga.

Amesema kuwa, wiki hiyo ya ubunifu itaenda sanjari na maadhimisho ya miaka 10 ya toka kuanzishwa kwakwake,ambayo kwa mwaka huu imebebwa na kauli mbiu “Ubunifu kwa maendeleo jumuishi ya rasilimali watu”.

Aidha ameongeza kuwa, wiki ya bunifu imeweza kutoa fursa na kuongeza uelewa kwa vijana wengi na baadhi yao wamepata fursa ya kuonekana na kujulikana zaidi.

Hata hivyo, amesema maendeleo jumuishi ya rasilimali watu”.

“Katika kuelekea wiki ya ubunifu COSTECH na wadau wa maendeleo tunajivunia mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na uwepo wa uelewa wa pamoja ulioleta matokeo chanya,”amesema Dkt Nungu

Aidha ameongeza kuwa, wiki ya bunifu imeweza kutoa fursa na kuongeza uelewa kwa vijana wengi na baadhi yao wamepata fursa ya kuonekana na kujulikana zaidi.

Naye, Meneja Progaramu kutoka funguo, Joseph Manirakiza amesemakatika wiki ya uvumbuzi wanafurahia nguvu ya mageuzi ya juhudi shirikishi katika kuendeleza teknolojia na uvumbuzi.

Amesema kuwa, tukio hilo linatoa jukwaa kwa wiki ijayo ya kitaifa ya ujuzi wa elimu na uvumbuzi inayoangazia makutano muhimu ya nyanja hizi.

Janeth Martoo ni Meneja Progaramu wa Umoja wa Ulaya amesema ubunifu unahitajika zaidi kwasababu unasaidia katika kukuza ustawi wa uchumi wa taifa.

Amesema licha ya chagamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabia chi bado anaamini sekta ya ubunifu ikipewa kipaumbele itaongeza nguvu katika kukuza uchumi.

Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI