RAIS DKT SAMIA ASEMA AFRIKA INAHITAJI MAGEUZI




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Bara la Afrika linahitaji mageuzi katika nyanja zote muhimu kwa ajili ya maendeleo ya bara hilo.

Kauli hiyo ameitoa leo wakati akihutubia katika kilele cha mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu uliofanyika Jijini Dar es Salaam.

"Ni wazi kuwa Bara letu bado linahitaji mageuzi makubwa katika nyanja zote muhimu za uzalishaji na maendeleo. Na haya ndio malengo na madhumuni ya ajenda ya Maendeleo ya Afrika tunayoitaka ya mwaka 2063 ambayo imeweka malengo 7", alieleza Mhe. Rais Samia.

"Nataka nijielekeze kuyazungumzia malengo manne, ambayo ni Afrika ambayo mafanikio yake yanajikita kwenye ukuaji jumuishi wa uchumi na maendeleo endelevu, Bara lenye utangamano kisiasa kwa kuzingatia fikra za kimajumuishi na mwelekeo wa kimapinduzi, Afrika inayozingatia misingi ya utawala bora, demokrasia, haki za binadamu na utawala wa sheria na Afrika ambayo maendeleo yake yanatokana na watu kwa kutumia vipaji vyao, hususan wanawake na vijana pamoja na kutoa makuzi bora kwa watoto".Rais Dkt Samia 




Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI