WANANCHI WATAKIWA KUKUZA UCHUMI MKUTANONWA RASILIAMALI WATU

 

Na Mwandishi wetu HPMedia, Dar 

Imeelezwa kuwa kupitia mkutano wa kimataifa wa wakuu wa nchi za Afrika kuhusu rasilimali watu  utakaofanyika Julai 25 hadi 26 jijini Dar es Salaam utasaidia kukuza pato la taifa na kuimarisha uchumi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amesema kuwa, mkutano huo ni matunda ni Rais Dkt Samia katika kuifungua nchi na kutangaza utalii  wa ndani hivyo kupitia mkutano huo kutakua na fursa na nyingi za kukuza uchumi.

Amesema kuwa, mkutano huo utahudhuriwa na wageni 1200 kutoka katika nchi hizo ambao watakula na kulala katika holeti zaidi ya 40 ambapo wafanyabishara zaidi ya 100 wameshaandaliwa vizuri kuhusu bidhaa zao pamoja na uuzaji wao jambo ambalo litatoa fursa nyingi kwa hususani kwa watanzania ambao ndio wenyeji wa mkutano huo.

"Kupitia ugeni huu watanzania hawana budi kutumia fursa hiyo kuweza kutangaza utalii wa ndani pamoja na kutangaza biashara zao, mahoteli, kupika vyakula vya kitanzania kwani hii ni sehemu ya utalii hiyvyo lazima wachangamkie fursa "amesema Rc Chalamila.

Kwa upande wake,Mkurugenzi wa ukumbi wa kimataifa JNCC Ephraim Makuru amesema kumbi zote za JNCC zipo tayari kwa ajili ya mikutano na kuwa kila nchi inahitaji kupata taarifa kwa lugha zao vifaa vimekamilika ili kila mgeni atakapoondoka kurudi nchini kwao aondoke akiwa na furaha na neno Asante Tanzania.



Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI