NCHI 43 ZASHIRIKI MKUTANO WA RASIMALI WATU AFRIKA TANZANIA
Na Mwandishi wetu,Dar
NCHI 43 za bara la Afrika zashiriki mkutano wa Rasilimali Watu Afrika ambao unafanyika Tanzania kuanzia Julai 25 na 26 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Idadi hiyo ya nchi shiriki imetolewa na Benki ya Dunia (WB) ambao wameshirikiana na Serikali ya Tanzania kuandaa mkutano huo muhimu katika eneo la rasilimali watu.
Kwa mujibu wa taarifa ambayo imesambazwa kwa waandishi wa habari imeonesha kuwa katika nchi hizo 43 zipo ambazo zimewakilishwa na Marais wenyewe, makamu wa rais, mawaziri wakuu, makamu waziri wakuu, mawaziri na watendaji wengine hii ni kuonyesha ushirikano ulipo baina ya nchi hizo .
Mkutano huo ulioanza Julai 25 ulifunguliwa na Makamu wa Rais Dk Philip Mpango ka ngazi ya mawaziri na watendaji wa nchi shiriki Kabla ya mkutano huo kuanza Julai 24 walikutana watendaji wa ngazi mbalimbali wa nchi shiriki na kujadiliana mambo mbalimbali ikiwemo namna ya kusaidia suala la ajira kwa vijana,raslimali za Afrika zitakavyoinua Uchumi,Suala la taasisi la kifedha .
Taarifa iliyotolewa leo imeonesha nchi zilizowakilishwa na marais ni Kenya, Afrika ya Kati, Madagascar, Malawi, Sao Tome na Principe, Msumbiji na Sierra Leone.
Aidha taarifa hiyo imesema nchi zilizowakilishwa na Makamu wa Rais ni Benin, Sudan Kusini, Zazmbia na Uganda.
Kwa upande wa nchi zilizowakilishwa na mawaziri wakuu ni Burundi, Ethiopia, Somalia, Eswatin na Cape Verde.
Pia wapo wawakilishi kutoka Nigeria, Algeria, DRCL Congo, Tunisia na kwingineko.
Comments
Post a Comment