UWOYA AJA KIVINGINE, AMPA HEKO RAIS DKT SAMIA "KILIMO KINALIPA"





Mwenyekiti wa mradi wa Kilimo Jembe ni Mama Msanii wa bongo movie Iren Uwoya amesema  Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassani na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe katika kipindi cha miaka minne  kumekuwa na mageuzi makubwa sana kwenye sekta ya Kilimo chini ya .

Kauli hiyo ameitoa leo Janiari 26, 2024 jijini Dar es Salaam katika hafla fupi ya  kutambulisha mradi huo wa Jembe ni Mama katika mkutano na waandishi wa habari amesema kuwa Serikali imeota ruzuku ya mbolea, pembejeo,mikopo, na kuwatafutia masoko wakulima ili wauze mazao ya Kwa bei nzuri bila ya kupata hasara hivyo hilo ni jambo la kipekee.

 " Mradi huu wa Jembe ni Mama wataungana kufanya ziara nchi mzima Kwa wanawake wote wanafanyia Kilimo Kwa kuwatia moyo wasikate tamaa kwani Kilimo ni uti wa mgongo wa mtanzania na husaidia kusomesha watoto kulisha familia kujenga mkazi bora wanawake tutambee sisi ni nguzo muhimu Kwa familia Kilimo hakimtupi mtu " amesema Irene Uwoya.

Irene Uwoya Amesema  2018 aliamua rasmi kujiunga na Kilimo 2018 Kwa kuanzia kulima Mkoani Tanga na Mbeya zao la mpinga na Tangawizi licha ya kuwa na shughuli nyingine lakini aliona  mafanikio na alifanya tafiti kuhusu wanawake wanaojishaghulisha na Kilimo na kugundua walikuwa wanakumbana na changamoto ya kulim Kilimo duni hivyo alifanya mahojiano nao na kuwapatia elimu namna na kulima Kilimo cha kisasa .

Aidha amesema kuwa katika kuhakikisha Iren Uwoya anaisaidia sekta ya Kilimo na Serikali ya Jamuhuri wa Muungano Tanzania ameamua kufanya tamasha kubwa (Jembe ni Mama Festival) ambalo limelenga kuwainua wakulima wadogo wadogo hasa wanawake kila Mkoa watakaopita watahamasisha kuhusu Kilimo.

Hata hivyo, amesema kuwa tamasha hilo kubwa la Kilimo ambalo litalenga kutengeneza mtandao wa Kilimo siku rasmi ya wakulima wanawake Tanzania.

"Mwanamke ndie anaetumika kwenye mnyororo wa thamani wa Kilimo lakini mwanaume ndie anampangia bei baada ya kuvuna, wanaume hawashiriki kuanzia mwanzo wanakuja mwisho wa mavuno"amesema Uwoya.

"Tutaanza kuwatembelea wakulima wanawake wote nchini Tanzania wanaojishulisha na Kilimo kuwavumbua hasa wale wanafanyia Kilimo duni na kuwasaidia kwa kuwawezesha katika kilimo cha kisasa"

Ameongeza kuwa Rais DKT Samia Suluh Hassan na Waziri wa Kilimo Hussen Bashe wametengeza njia kwenye Kilimo ikiwa ni pamoja na kupata pembejeo , mikopo ya Kilimo na matumizi Tehama kwenye Kilimo.

Comments

Popular posts from this blog

HUU NDIO USHAURI WA TMA KWA SEKTA HIZI ...

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI