FURAHIKA EDUCATION YAAHIDI KUINGA MKONO SERIKALI, YANADI MATUNDA YAKE
KATIKA kuelekea kutimiza miaka 48 ya Chama cha Mapinduzi (CCM),tangu kuzaliwa kwake, Chuo cha Ufundi Furahika VETA kilichopo Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam kimeipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa kusimamia vyema ilani ya Chama hicho kwa kupiga hatua katika kukuza Sekta ya Elimu nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa bodi ya Chuo hicho Ngwenje Mohamed amesema Sekta hiyo imekuwa Kwa kiwango Cha juu ikilinganishwa na miaka ya huko nyuma kwani sasa shule za kata Kila mahali vyuo vya kati na vikuu vimeongezeka hiyo yote ni jitihada za Chama cha CCM kupitia ilani yake kuhakikisha kila Mtanzania bila kubagua dini Chama ukabila watu wote wanapata elimu.
"Kuelekea maadhimisho ya miaka 48 ya kuzaliwa chama cha CCM Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan tunaona mengi aliyoyafanya ameendeleza utoaji elimu bure vyuo vya Ufundi Veta navyo vikipewa kipaumbele ili kuibua ujuzi na tafitibalimbali hii inaonyesha kuwa, mazingira ya Elimu nchini Tanzania ni mazuri "amesema Mohamed
Sambamba na hayo amebainisha kuwa ni mambo mengi yamefanyika ikiwemo Sekta ya Afya ujenzi wa Zahanati kuongezeka kwa wataalamu wa Afya madaktari amesema kuwa tangu kuzaliwa kwa Chama hicho maendeleo ni makubwa ndani ya nchi ya Tanzania ikiwemo sekta ya uchumi unaku kwa kasi hospital, Shule, ambapo zamani wanafunzi walikua wakitumia umbali mrefu lakini sasa hivi kila Kata kuna zipo hata kiwango cha wasomi kinazidi kuongezeka pamoja na kuwepo kwa vyuo na vyuo vikuu nchini.
"Mazingira ya elimu yameboreshwa vizuri, sisi tunatoa elimu bure tena kwa viwango ambapo wanafunzi wetu waliohitimu zaidi ya 700 wamepata ajira katika sehemu mbalimbali, tuna kila sababu ya kuipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi bora na thabiti wa Dkt Samia"amesema
Aidha, amesema chini ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassani hata wao wadau wa maendeleo wameweza kuendesha vyuo na kutoa elimu bure, hiyo imetokana na Sera nzuri za Chama Cha Mapinduzi CCM pamoja utendaji kazi na ufualiaji ndio maana wamekua na uthubutu wa kukipongeza chama hicho.
Ameongeza kuwa mpaka sasa wanafunzi 1900 wameweza kupata elimu bure, ambapo hiyo imetokana na Sera nzuri za Chama cha Mapinduzi,huku wakipata wafadhili wa kuwalipia ada wanafunzi hali inayompunguzia majukumu mzazi kuweza kumpatia mtoto wake elimu ambapo jukumu lake ikiwa ni kumnunulia madaftari, peni na unform mtoto wake.
Hata hivyo, amesema wakati umefika wa kumuunga mkono Rais Dkt Samia kwa jitihada anazofanya ambapo kwa upande wa Zanzibar Rais Hussen Mwinyi ameleta mabadiliko makubwa ya kimaendeleo ikiwemo kuboresha miundombinu .
"Kutokana na matunda ya Chama Cha Mapinduzi sisi kama Taasisi ya Furahika tutaendelea kuinga mkono Serikali na kumuunga mkono Rais Dkt Samia, huku akiwapongeza wajumbe wa Chama hicho kwa kulipitisha jina la Rais Dkt Samia kugombea tena uchaguzi mkuu wa mwaka 2025"amesema Ngwenje.
Aidha, amesema kuwa Chuo hicho kinatoa elimu bure bila kuangalia mwanafunzi ametoka katika Chama gani wala dini yake wala kabila lake wanachokiangalia wao ni utayari wa mwanafunzi kuweza kupokea mafunzo na kwenda kuwafanyia kazi ili kujikwamua kiuchumi.
Hata hivyo, amesema katika kuharakisha maendeleo na kuwasaidia wazazi kuanzia mwezi wa tano wanafunzi watapewa chakula bure ili kuhakikisha wanapata elimu bora na kupata utulivu wa ajili pindi wanapokuepo darasani
Comments
Post a Comment