TMA YATOA USHAURI HUU KUELEKEA MVUA ZA MSIMU WA MASIKA
Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania (TMA) imewataka watumiaji wa taarifa za hali ya hewa ikiwa ni pamoja na wakulima, wafugaji, mamlaka za wanyama pori, mamlaka za maji na Afya kuendelea kufuata, kupata na kuzingatia ushauri wa wataalam katika sekta husika ili kuepusha athari zinazoweza kujitokeza katika mvua za msimu wa masika.
Amesema Mwelekeo wa mvua za Masika 2025 kwa Kanda ya Ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara) pamoja na kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma, Mvua za Wastani hadi Chini ya Wastani zinatarajiwa, ambapo zitaanza Machi, wiki ya kwanza hadi ya pili, na kuisha Mei, wiki ya kwanza.
Aidha Pwani ya Kaskazini (kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro, Pwani, Dar es Salaam, Tanga na visiwa vya Unguja na Pemba) Mvua za Wastani hadi Chini ya Wastani zitaanza Machi, wiki ya kwanza hadi ya pili, na kuisha Mei, wiki ya tatu hadi ya nne.
Pia Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro), kutakuwa na Mvua za Wastani hadi Juu ya Wastani ambapo zitaanza Machi, wiki ya pili hadi ya tatu, na kuisha Mei, wiki ya kwanza.
Amesema athari zinazotarajiwa ni pamoja na unyevu na mafuriko, ambapo Mvua nyingi zinatarajiwa katika baadhi ya maeneo, na huenda zikapelekea mafuriko na kuathiri ukuaji wa mazao.
Amesisitiza kuwa taarifa hiyo inatolewa kwa ajili ya kusaidia wadau wa sekta mbalimbali, kama vile kilimo, mifugo, uvuvi, maliasili, afya, nishati, usafirishaji, na usimamizi wa maafa, kuchukua tahadhari stahiki na kupanga mikakati ya kukabiliana na athari za mvua.
Awali alisema Mwenendo wa mvua za Msimu (Novemba 2024 – Aprili 2025) zinatarajiwa kuwa za Wastani hadi Chini ya Wastani katika mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi, Rukwa, Songwe, Singida na Dodoma, huku mvua za Wastani hadi Juu ya Wastani zikitarajiwa katika mikoa ya Njombe, Ruvuma, Mtwara, Lindi na mikoa mingine
Comments
Post a Comment