MAMIA YA VIJANA WAJITOKEZA TAMASHA SINGELI KIPAJI VINGUNGUTI

 


Mamia ya vijana wafurika uwanja wa msikate tamaa  kwenye uzinduzi wa Singeli kipaji kata ya Vingunguti Manispaa ya ilala jiji la Dar es salam ambapo vijana kutoka mikoa mbali mbali wamefika ikiwemo Mtwara na Morogoro.



Akizungumza wakati wa kufunga mashindano hayo Meya wa jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto amesema lengo la mashindano hayo ni kutekeleza agizo la Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania la kuibua vipaji vya singeli katika halmashauri zote nchini.

Amesema kuwa, mwitikio wa vijana kujitokeza kwenye tamasha hilo umekua mkubwa kwani wamejiyokeza kutoka mikoa mbalimbali sio Dar es Salaam peke yake.

"Asanteni kwa kuja, mmeitikia wito mmekuja kwa wingi mmeujaza uwanja, kama serikali hatutowaangusha tutahakikisha tunaibua vipaji,leo muda umekua mchache kwa wingi wenu lakini tutairudia tena"amesema Meya Kumbilamoto.

Aidha amewasihi vijana kutokata tamaa katika harakati za kujitafuta kwani wanaweza kuanguka hata mara kadhaa au kutokukubalika baadhi ya sehemu lakini isiwe ni njia ya kutofikia malengo yao.

"Muangaliaeni msanii wa Bongo fleva Hamornize alivyokataliwa bongo star such lakini hakukata tamaa alipambana na sasa hivi amekua msanii mkubwa aneheshimika na kujulikana kila sehemu"amesema Meya Kimbilamoto.

Aidha, amesema kuwa kutokana na muitikio wa vijana kuwa mkubwa mashindano hayo ya kuibua vipaji kwa wasanii wasingeli yatafanyika tena katika kata ya Buguruni ambapoziezi hilo litakua endelevu.



Comments

Popular posts from this blog

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU NDIO USHAURI WA TMA KWA SEKTA HIZI ...