WASANII WA BONGO MOVIE KUPEWA TUZO ZA HESHIMA ZA KIMATAIFA

 



Na Mwandishi wetu

Wasanii wa Bongo movie wanatarajiwa kupewa heshima kimataifa kupitia Tuzo za Tamthilia zinazotarajiwa kuzinduliwa rasmi Agosti 24,2024 Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Meneja wa Kitengo cha Uhakiki kutoka Bodi ya Filamu nchini Boppe Kyungu amesema Serikali kupitia Bodi ya Filamu inazitambua tuzo hizo,ambapo pamoja na mambo mengine amewataka wadau wa Filamu nchini kuungana katika kuzifanikisha kwakuwa tuzo ni nyenzo ya kuboresha Sekta ya Filamu na Michezo ya Kuigiza nchini.

Aidha Kyungu ameongoza kuwa wadau wa Filamu wachangamkie Fursa hiyo kwani tuzo hizo zinaenda kuacha alama na kuona kasi mpya ya kutengeneza kazi zenye ushindani Kimataifa pamoja na kutangaza utalii na Utamaduni kupitia sekta ya Filamu nchini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mtendaji wa Tuzo za Tamthilia nchini Eliya Mjata amesema ujio wa tuzo hizo zinalenga kutoa fursa na wigo mpana kwa wasanii kuipa heshima tasnia na Nafasi kwa watayarishaji wa kazi za Sanaa ambao kwa sasa wanachukua nafasi kubwa kuchangia pato la taifa na kukuza Utamaduni na Kutangaza Utalii na Lugha ya Kiswahili.

Aidha ameongeza kuwa Kumekuwepo tuzo mbalimbali ambazo zinaandaliwa akizitaja Tuzo za Filamu zinazoandaliwa na Bodi ya filamu,Tuzo za Muziki chini ya Uongozi wa Baraza la Sanaa taifa(BASATA) lakini kumekuwepo changamoto ya eneo la Tamthilia kutopewa Nafasi kubwa zaidi.

Mjata amesema Tuzo hizo za Filamu zitashirikisha Watayarishaji, Wasanii,Wadau wengine kutoka nchi mbalimbali duniani.

"Tunapenda Kuishukuru Wizara ya Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambapo tulifanya kikao nao nakuomba mambo kadhaa yakiwemo kutafuta fursa kama programu za Kubadilishana uzoefu katika nchi mbalimbali ikiwemo Uturuki, noChina,Japan,Marekani, India,Pakistan, Ufaransa, Ujerumani, Ufilipino na Uingereza."

Nae Mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Idara ya Diplomasia na Uchumi Maryam Vuai amesema Mambo yaliyotumwa na Waandaaji wa Tuzo hizo yamefika Wizarani na watahakikisha wanatoa Ushirikiano Mkubwa kupitia Sekta ya Filamu.

Vuai ameongeza kuwa Wizara inategemea kupitia tuzo hizo zitaweza kubadilishana uzoefu na Utamaduni kupitia nchi shiriki pamoja na Kukuza Lugha ya Kiswahili.

Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI