TAMASHA LA PASAKA LA KUMSHUKURU MUNGU KWA UONGOZI WA RAIS DKT SAMIA YAENDELEA VIZURI
Na Magrethy Katengu,HPMedia, Dar
MKURUGENZI wa Msama Promotion Alex Msama amesema maandalizi ya Tamasha la Pasaka litakalofanyika Aprili 9, 2023 viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam yanaendelea vizuri.
Msama ameyasema hayo leo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kueleza namna maandalizi ya Tamasha hilo yalipofikia na Jumla ya wanamuziki wa nyimbo za Injili waliothibitisha kushiriki.
“Maandalizi ya Tamasha yako vizuri na tumejipanga vya kutosha Tamasha hilo litakuwa ni lakipekee kwani ni urejeo mpya kwa sababu halijafanyika kwa takribani miaka saba (7) iliyopita hivyo watu wote wa dini zote mnaalikwa hakuna kiingilio ni buree"amesema Msama
Msama amesisitiza kuwa lengo la Tamasha hilo ni kuwafanya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kusherehekea Siku Kuu ya Pasaka katika mazingira mazuri na ndiyo maana wameliweka viwanja vya Leaders Club ili iwe rahisi kila mwananchi kufika.
Pia Tamasha la Pasaka litatumika kumshukuru Mungu kwa miaka miwili ya uongozi mzuri wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amefanya kazi nzuri katika Mambo mengo ikiwemo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali.
“Chini ya miaka miwili ya uongozi wa Rais Samia miradi yote imetekelezwa vizuri na biashara zinaenda vizuri, hivyo tunayo kila sababu ya kumshukuru Mungu katika Tamasha hili la Pasaka,” amesema Msama.
Hivyo amewehimiza wananchi hususan wakazi wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kwani usalama utakuwepo wa kutosha na watapata burudani kutoka wa waimbaji wengi nguri ambao wamethibitisha kushiriki.
Baadhi ya waimbaji hao ni Joshua Ngoma kutoka Rwanda, Tumaini Akilimali kutoka Kenya na Zabroni Singers kutoka Tanzaniha.
Wengine ni Upendo Ngoma kutoka Tanzania, Upendo Nkone kutoka Tanzania, Masi Masilia kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Ambwene Mwasongwe kutoka Tanzania na Joshua Mlelwa kutoka Tanzania.
Kwa upande wake Mratibu wa Tamasha hilo Emmanuel Mabisa amesema kwa mwaka huu wamejipanga vizuri kwenye suala la muziki.
“Tumeshapata kampuni itakayofunga vifaa vya muziki vya kisasa,” amesema Mabisa.
Amesisitiza kwamba watafanya tamasha kubwa na lakihistoria huku wakisherehekea miaka miwili ya Rais Dkt. Samia.
Amesema kwamba wameamua kulifanya Tamasha hilo katika viwanja vya Leaders Club kwa sababu ni eneo kubwa na la wazi.
Naye Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Christopher Mwahangila amethibitisha kushiriki katika tamasha hilo.
Amewataka Watanzania kwa ujumla kuhudhuria kwani wamejipanga kutoa burudani nzuri kwani walikuwa wamelimisi Tamasha kwa muda mrefu.
“Mimi nimiongoni mwa waimbaji watakaoshiriki, tulikuwa tumelimisi hili Tamasha, ewe Mtanzania usikose kufika, kwani tamasha ni bure kabisa,” amesema Mwahangila.
Comments
Post a Comment