SERIKALI KUHAKIKISHA ULINZI NA USALAMA MAHALI PA KAZI

 

Na Magrethy Katengu,HPMedia, Dar 

Serikali  imesema itaendelea kuheshimu mikataba ya Kimataifa kwa kuhakikisha kuwa inaweka ulinzi  na Usalama mahali pa kazi ili kusaidia  Wafanyakazi walioajiriwa au kuniajiri wanafanya kazi zao Kwa amani Ili kusaidia kuchochea Ustawi wa Jamii yenye uchumi Imara .

Akizungumza leo Jijini Dar es salaam Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Vijana Ajira na Watu wenye Ulemavu Patrobas Katambi wakati wa ufunguzi wa Warsha ya kwanza ya siku Moja kuimarisha Uhusiano Bora kati ya Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda biashara ,Taasisi za fedha huduma na ushauri(TUICO) na chama Cha Waajiri ATE ambapo amesema Serikali ina imani sekta zote za kazi kwani zina mchango mkubwa kuongeza Uchumi na Pato la Taifa kuongezeka .

"Warsha hii ya leo itakuwa chachu na kiungo muhimu cha ushirikiano wa Waajiri,Wafanyakazi pamoja na taasisi za kifedha katika kutekeleza Maadhimio ya Shirika la kazi Duniani ILO ili kuboresha mazingira rafiki katika eneo la kazi"amesema Waziri

Hata hivyo Waziri amewaasa viongozi wa vyama hivyo  kutotumia wanasiasa katika vyama vyao kuwasemea changamoto zao kwani Wana uwezo wa kukaa pamoja na kusuluhisha palipo na shida siyo kama ni hapo awali miaka ya kadhaa ya nya baadhi yao wametumia vyama hivyo kwa ajili ya maslahi yao ya kisiasa hivyo kupitia Warsha hii ya leo iwasaidie kuzungumza pamoja changamoto zenu na kuzitatua pasipo kupitia viongozi wanasiasa

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda biashara,taasisi za fedha ,huduma na Ushauri (TUICO)Paul Sangeze amesema Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi waandamizi waliohudhuria itakuwa chachu yale yatatakayojadiliwa italeta tija kwa kwa kuboresha mazingira mahala pa kazi.

Kwa Upande wake Afisa Mkuu Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE)  Suzanne Naomba amesema Waajiri haki ya kujiunga na Chama Cha Wafanyakazi ipo kikatiba mtu binafsi hashurutishwi anajiunga kwa hiari yake mwenyewe na anatakiwa afuate utaratibu..

Aidha Waajiri ni Wadau wakubwa hivyo ushirikiano huo utasaidia kutatua changamoto mahala pa kazi hivyo ni vyema mikaba yote yote ya kazi ifanyike kwa uwazi na majadiliano yafanyike Kwa Nia njema pande zote waridhike

Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI