NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI






Na Mwandishi wetu 

Chama Cha National League For Democracy (NLD) leo kimezindua kampeni maalum yaKkukiondoa chama Cha Mapinduzi madarakani "fyeka CCM" ambapo imelenga kuzunguka mikoa 10 ya Tanzania ikiwemo Tanga, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Singida, Dodoma na Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari na wanachama wa chama hicho, jijini Dar es Salaam kwenye makamo makuu ya chama hicho, Katibu Mkuu Doyo Hassan Doyo amesema kuwa, chama hicho kina sera nzuri ambazo zinawabeba wananchi hasa katika kuwakomboa na umaskini.

Aidha, uzinduzi wa kampeni hiyo umeenda sambamba na kuwapokea wanachama wapya kutoka chama Cha ACT -Wazalendo na ADC ambapo amesema kuwa, kupitia kampeni hiyo watategeneza  wagombea ambao wataweza kushindana kwa hoja, huku akiwataka viongozi na wanachama kutumia lugha nzuri wanapokuwa majukwaani na kufanya siasa za kistarabu.

"Siasa lazima zifanyike katika mazingira yanayoheshimika ..wanasiasa tuheshimiane .. wanasiasa tusifanye kiburi kwa viongozi ambao wako madarakani," Nakuongeza kuwa" kwa uelewa wangu siasa ni tunu inayosogeza  maendeleo kwa wananchi "alisisitiza Doyo 

Ameongeza "juzi tunasikia kuna kongamano lilifanyika nchini la wanawake wanaosadikiwa kuwa ni wanachama wa (CHADEMA) wanasema Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ni muuaji maneno haya katika siasa sio mazuri tena yenye tafsiri mbaya  kwenda kumtuhumu kiongozi wa nchi ni muuaji ni kuikosea siasa za Tanzania na wananchi awawezi kuendeshwa kwa siasa za namna hiyo "amesema Doyo

Aidha amesema Chama cha NLD kinaamimi katika itikadi ya uhuru ambao una mipaka, hivyo mtu anapopewa uhuru asizungumze maneno ya kumdhalilisha mtu wala kumtuka ni kinyume cha sheria, hivyo wanapofanya siasa lazima wajue uhuru walionao pia una mipaka yake, hivyo wazumgumze maneno yenye staha.

"Chama Cha NLD, sisi tunajibu Kwa hoja, juzi Rais Dkt Samia aliwahutubia wanachama wake na kumwambia hajaona mbadala wa chama cha kushika dola, sasa sisi tunajibu chama chetu kinakuja kuonesha njia, ndio chama mbadala kinachokwenda kushika dola kwani tunasera na itikadi nzuri NLD inaamini katika haki na uzalendo "amesema Doyo

Katika hatua nyengine, ameiomba Ofisi ya Rais tawala za Mikoa na Serikali za mtaa (TAMISEMI) kusogeza mbele Uchaguzi wa Serikali za mitaa kwani muda wa kujiandaa uliowekwa ni mdogo, hawawezi kukamilisha ndani ya siku sita.

"Tunaiomba TAMISEMI irekebishe ratiba ya Uchaguzi wa Serikali za mitaa siku za mchakato ziongezwe ili vyama vya siasa viweze kujipanga vizuri, na kushiriki kikamilifu ikiwa ni pamoja na kusimamisha wagombea na kujindikisha  na kupiga kura"amesema Do you.


Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU NDIO USHAURI WA TMA KWA SEKTA HIZI ...