NAIBU KATIBU MKUU NLD ATOA WITO HUU KWA VIONGOZI




Na Ombe Kilonzo, Zanzibar

Naibu Katibu Mkuu Bara wa chama cha NLD, Mhe. Khamis Said Hamad, akizungumza na viongozi mbalimbali katika ziara ya ujenzi wa chama Zanzibar, alisisitiza umuhimu wa kujipanga kwa viongozi wa NLD kuhakikisha chama kinawakomboa Watanzania Bara na Visiwani. Mhe. Khamis alibainisha kuwa NLD ina sera zinazojibu changamoto za kijamii, kiuchumi, na kisiasa, na akawataka viongozi kuzieneza sera hizo ili kuvutia wananchi zaidi.

Mhe. Khasani aliongeza mwito kwa viongozi hao kuandaa wagombea wenye sifa, waaminifu, na wenye nia ya kweli ya kuwatumikia wananchi kwenye ngazi za mitaa na vijiji, na hatimaye uchaguzi mkuu, hatua itakayoongeza imani ya wananchi katika chaguzi zijazo.

Ziara hiyo ya siku nne, ikiongozwa na Katibu Mkuu Mhe. Doyo Hassan Doyo, inaendelea leo visiwani Zanzibar.

Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI