DOYO AFANYA ZIARA ZANZIBAR APOKELEWA KWA SHANGWE NLD

 



Zanzibar.

Katibu Mkuu wa  chama cha National League for Democracy (NLD), Mhe. Doyo Hassan Doyo, leo tarehe 11-09-2024 amewasili Visiwani Zanzibar kwa ziara ya chama cha NLD. Katika ziara hiyo, Mhe. Doyo ameambatana na viongozi mbalimbali wa chama hicho kutoka upande wa Bara na kupokelewa na baadhi ya viongozi wa chama hicho upande wa Zanzibar, akiwemo Mwenyekiti wa chama cha NLD Taifa, Mhe. Mfaume Khamis Hassan.

Mhe. Doyo na Mwenyekiti wa NLD walifanya kikao cha ndani na baadhi ya wanachama wa chama hicho upande wa Zanzibar, ambapo wote kwa pamoja walitoa mwito wa kuimarisha ujenzi wa chama na ushirikiano kati ya wanachama wa NLD kutoka Bara na Zanzibar.

Akizungumza na wanachama wa NLD, Mwenyekiti wa chama hicho Mhe. Mfaume Khamis Hassan aliwataka wanachama wa NLD nchini kumuunga mkono Mhe. Doyo ili kuleta mabadiliko ndani ya chama hicho, akimwelezea Mhe.Doyo kama mtu muadilifu na mtendaji mzuri wa kazi za chama. Mwenyekiti alisisitiza, "Hakuna chama chochote kinachoweza kumkataa mtu kama Doyo, mtu mwenye historia ya utendaji bora katika siasa za nchi hii."

Kwa upande wake, Mhe. Doyo aliwashukuru wanachama wa NLD kwa utayari wao wa kufanya kazi naye, na akawahakikishia kwamba atafanya mabadiliko makubwa ndani ya muda mfupi. Aliahidi kukifanya chama hicho kuwa miongoni mwa vyama shindani katika chaguzi zijazo. Aidha, Mhe. Doyo alimuahidi Mwenyekiti wa NLD kuwa tayari kupokea baadhi ya wanachama wanaomuunga mkono kutoka sehemu mbalimbali nchini katika harakati za muendelezo wa kuimarisha demokrasia.

"Nyuma yangu kuna kundi kubwa lililofurahishwa na sera nzuri za NLD hasa inayosisitiza uzalendo, haki, na maendeleo kwa umma," alisema Mhe Doyo, na kuimiza kwamba ukombozi wa umma utakuja chini ya mwamvuli wa NLD.

Kesho, viongozi wa chama hicho wataendelea na ziara yao ya ujenzi wa chama katika jimbo la Chaani.

Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI