TANZANIA YAPOKEA MELI KUBWA YA WATALII, MABORESHO YA BANDARI YAZAA MATUNDA


Na Mwandishi wetu, Dar

Tanzania kupitia Mamlaka ya Bandari TPA imeweka historia kwa kupokea meli kubwa ya watalii ikitokea nchini Norway inayomilikiwa na kampuni ya Norwegian Cruiseline Holdings ya Marekani, yenye urefu wa mita 294 ambapo meli hiyo ni ya kwanza kutia nanga katika bandari ya Dar es Salaam tangu nchi hiyo ilipopata uhuru mwaka 1964.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya maboresho makubwa yanayoendelea kufanyika katika bandari ya Dar es Salaam kupitia mradi wa maboresho ya bandari ya Dar es Salaam (DMGP) ambayo yamechagia ujio wa meli hiyo, hali  itakayopelekea kuongezeka kwa watalii nchini humo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mara baada ya kupokea meli hiyo iliotia nanga majira ya saa 11 alfajiri mapema leo hii, Mkurugenzi Mkuu wa Bandari hiyo, Mrisho Mrisho amesema kuwa,malengo ya bandari hiyo ni kuhudumia meli zenye urefu wa mita 305 hadi 350. 

Amesema kuwa, meli hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 4700 lakini kwa Tanzania wamekuja wageni zaidi ya  2000 ambapo wageni 1100 walishuka katika bandari ya Zanzibar na kuelekea katika vivutio mbalimbali vikiwemo Ngorongoro na Serengeti kupitia ndege za kukodi na hatimaye wataungana na abiria wenzao katika bandari ya Dar es Salaam na kuendelea na safari. 

"Ujio wa meli hii kubwa katika bandari yetu yenye uwezo wa kubeba abiria 4,700 kutafungua milango kwa wadau wengine wenye meli kubwa zaidi duniani kutia nanga kwenye bandari hii,tukumbuka haya ni matunda ya Royal Tour Rais Dkt Samia ametufungulia milango ya kuongeza watalii nchini kupitia filamu yake"amesema Mrisho

Hata hivyo, wageni zaidi ya 300 wameshuka katika bandari ya Dar es Salaam na kufanya matembezi katikati ya jiji la Dar es Salaam (City Tour) kupitia wakala wa utalii. 

Kwa upande wake, Nahodha Mkuu wa Mamlaka ya Bandari TPA, Abdula Yussuf Mwingamno amesema kuwa ujio wa meli hiyo ni jambo la kujivunia sana kwani maboresho yanayoendelea katika bandari hiyo ndio yanatoa fursa kupokea meli zenye urefu mkubwa zaidi kuwahi kutia nanga katika bandari hiyo.

"Meli kubwa mara nyingi sana tumekua tukizipokea mchana lakini kwa maboresho tulioyafanya katika bandari yetu, meli hii imeweza kutia nanga saa 11 alfajiri bila matatizo yoyote na captain wao wameisifia sana bandari yetu katika bandari zote walizopita"amesema Nahodha Mwangamno.

Amesema kuwa, Kwa kushirikiana na waongozaji wa meli nchini wameweza kuweka mazingira wezeshi ya kupokea bidhaa kutoka kwenye meli na rasiliamali za watu hivyo Bandari ya Dar es Salaam, Mtwara na Tanga kutakua na ushindani wa kibiashara.

Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI