TAKUKURU KINONDONI YAJIPANGA KUFUATILIA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

 




Dar es salaam

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Mkoa wa Kinondoni imesema licha ya kutoa huduma bora lakinia pia wamejipanga mwezi  Oktoba hadi Desemba 2024  kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa kuendelea kuelimisha wananchi wajue madhara ya rushwa na wahamasike kutoa ushirikiano mamlaka husika wanapoona viashiria vya rushwa.

Aidha, Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Mkoa wa Kinondoni imesema katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai hadi Septemba 2024 wamepokea malalamiko 104 yaliyohusu rushwa 72, yasiyohusu rushwa 32 .

Akitoa taarifa hiyo, Dar es salaam katika mkutano na Waandishi wa habari  Kaimu Mkuu wa Takukuru (M) Kinondoni Christian Nyakizee  amebainisha kuwa katika kipindi hiko walifungua mashauri mapya mawili katika Mahakama ya Wilaya ya Ubungo na Mashauri 7 yaliyolewa maamuzi na Jamuhuri imeshinda  mashauri matatu huku mashauri 24 yakiendelea mahakamani.

Sanjari na hayo wamefuatilia  miaradi ya maendeleo yenye thamani ya Tsh bilioni kumi na tano milioni mia tisa themanini na mbili laki mbili na ishirini na moja elfu mia tatu hamsini na tano na senti tisa ambayo inaendelea na utekelezaji.

"Katika miradi hii tumebaini mapungufu machache ambayo wahusika wameshauriwa kurekebisha mapungufu hayo na tunaendelea kufuatilia miradi hiuo hadi itakapokamilika ili kuhakikisha inakuwa na ubora kuendana na thamani ya fedha zilizotolewa

Hata hivyo amesema kuwa katika kipindi hiko waliendesha warsha kwa maafisa Ustawi wa Jamii  25 na askari Polisi dawati la jinsia na watoto 37 kutoka kwenye madawati 14 ambayo ni Magomeni,Mburahati,Gogoni,Magufuli Bus terminal, Mavuranza, Kawe , Mbweni, Mabwepande,Goba, na Madale wote ni kutoka  halmashauri ya Kinondoni .

" Takukuru lengo la kuandaa warsha hiyo ni kuwataka washiriki kusimamia maadili ili kuwasidia waathirika wa matukio ya ukatili wa kijinsia ikiwemo watoto na wanawake kupata haki zao kwani mara kadhaa imeshuhudiwa wahusika wakiachiwa huru kutokana na masula ya kindungu kukaa na kukubaliana huku mwathirika akikosa haki yake kwani kitendo hiko kinasababishwa na rushwa" amesema Nyakizee


Comments

Popular posts from this blog

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU NDIO USHAURI WA TMA KWA SEKTA HIZI ...