USALAMA WA BARABARANI KWA WATOTO, WAPIGIWA CHAPUO
KATIKA suala la Usalama Barabarani, Tanzania ni jambo muhimu linalohitaji kuangaliwa kwa haraka na kutiliwa maanai si tu Kwa Serikali bali hata na wadau wa Sekta binafsi kutokana na watoto ni miongoni mwa watumiaji wa barabara wanaokumbwa na hatari kubwa ya kupata ajali.
Takwimu zinatia wasiwasi kwani kuanzia Januari hadi Sept 2023 kuliwa na ajali 1,324 zilizorekodiwa kati ya hizo 834 zilisababisha vifo ikilinganishwa na 2024 hadi Sept ajali zimeongezeka na kufikia 1364, sawa na ongezeko la asilimia 3.vifo vimeongezeka hadi 920 ongezeko la asilimia 10.3 .
Akitoa taarifa ya mradi wa Tathmini za shule usalama barabarani awamu ya pili, Rais wa Chama cha Mbio za Magari Tanzania (AAT) Nizar Jivani amesema kuwa, hali ya usalama barabarani Tanzania, inapswa pia kuangazia jukumu muhimu ambalo pikipiki nazo zimekua ni janga lingine kusababisha ajali hususani kwa watoto.
"Ni lazima wadau mbalimbali waungane kwani takwimu ni mbaya tumefanya tathmini kwa mwaka 2023 kulikua na ajali 481 za pikipiki ambapo zimesababisha vifo 284, lakini mwaka huu hadi Septemba ajali za pikipiki zimeongezeka na kufikia 498 na idadi ya vifo imeongezeka pia hadi 317 ongezeko la asilimia 11.6"amesema Nizar.
Amesema kuwa, kupitia mradi wa Tathmini za shule usalama barabarani wamekua wakichukua hatua za awali kupunguza hatari za ajali kwa kuboresha miundombinu inayozunguka shuleni kwa kuanzisha hatua muhimu za usalama barabarani kama vile vivuko vya waenda kwa miguu,alama za kusimamia na onyo la"shule mbele".
Ameongeza kuwa, ushirikiano kati ya AAT na FIA umechangia sana katika utekelezaji wa juhudi hizo ambapo huo ni mfumo wa dhamira ya pamoja katika kuhakikisha usalama barabarani si kama ndoto tu, bali kama uhalisia unaoweza kubadili jamii ambapo kwa msaada wa FIA wamefanya Tathmini za kina kukusanya taarifa muhimu.
"Tumechukua hatua madhubuti za kuboresha usalama wa barabarani katika maeneo ya shule, huku tukiendelea kufanyia kazi kuhakikisha ajali zinapungua na watoto wanakua salama, kwani hawa ni nguvu kazi ya kizazi cha badae lazima tuwalinde kwa pamoja".
Akifunga mafunzo ya mradi Tathmini za Shule usalama barabarani, Naibu Kamishna wa Polisi, Kamishna wa kikosi cha Usalama Barabarani DCP Ramadhani Ng'anzi amesema kuwa mafunzo hayo yamelenga kupunguza ajali za barabarani husasani kwa watoto.
Amesema kuwa, walimu wanajukumu kubwa kuyaendeleza mafunzo hayo kwa wanafunzi ili kuhakikisha watoto hao wanakua salama na wanaweza kujilinda wanapokwenda shule au wanaporudi majumbani.
Amesema wameamua kushirikiana na wadau hao katika kupunguza ajali za barabarani husasani zinazotokana na watoto kwani watoto ndio nguvu kazi ya kesho ndio maana wameamua kuwekeza kwao kwani watakuwa mabalozi wazuri wa kusimamia juhudi hizo ili kuhakikisha wanajilinda sana.
Naye, Mkurugenzi mtendaji wa AAT Najma Rashid amesema kuwa, katika mzunguko wa kwanza wa mradi huo walizofikia shule 11 katika Wilaya ya Ilala ambapo wamefanya maboresho muhimu katika barabara katika maeneo ya shule, ambapo mradi huo ni hatua muhimu katika kujenga mazingira salama ambapo watoto wanaweza kwenda na kurudi shule kwa amani ya akili.
Amesema kuwa, katika kukamilisha mradi huo awamu ya pili wamezifikia shule 7 katika Manispaa ya Kinondoni ikiwemo Shule ya Sekondari kijitonyama, Magomeni, Turiani, shule ya msingi Tandale Magharibi, Mwalimu Nyerere, Turiani pamoja na Ali Hassan Mwinyi English Medium Pre and Primary.
Ameongeza kuwa, miradi kama hiyo ina nguvu katika kuhamasisha jamii kipaumbele cha usalama na kusaidia watoto wanaotumia barabara kuwa na ujasiri wanapovuka, kuwafumdisha watoto kuhusu misingi ya usalama barabarani ni uwekezaji wa muda mrefu katika kupunguza ajali na kukuza jamii salama.
Janeth Mabusi ni Mwalimu wa Shule ya Sekondari Turiani amesema kuwa, wamepata mafunzo hayo ambayo yatakwenda kuwasaidia ili katika kuwajenga wanafunzi kujilinda wanapokua barabarani kwa kufuata sheria zote, huku akiahidi kuyafanyia kazi ili jamii iwaamini kuwaletea watoto wao.
AAT imewajengea ujasiri watoto wao kwani wamepata mafunzo ya kutosha na wamejifundisha namna bora ya kuwa salama hasa wanapokua barabarani, aidha imeitaka AAT kupanua wigo Kwa kuzifikia shule nyingi zaidi ili elimu hiyo iwafikie watoto wengi.
Mafunzo haya yataleta mabadiliko makubwa kwa wanafunzi kwa kuwajengea uwezo wa kujilinda.
Comments
Post a Comment