WAWILI WAHUKUMIWA KUNYONGWA, WATUHUMIWA 47 WAKAMATWA
Na Mwandishi wetu Dar
Mahakama ya Wilaya ya Kigamboni imewahukumu kunyongwa hadi kufa kwa nyakati tofauti Abdala Athumani miaka 31 mkazi Yombo na Iddy Omary Ndekae miaka 26 mkazi wa Mbagala kwa makosa ya mauaji.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari
Kamanda Kanda Maalum ya Polisi
Dar es Salaam SACP Muliro J. Muliro amesema kuwa watuhumiwa hao walihukumiwa baada ya kesi zao kufanyiwa uchunguzi na kukutwa na hatia.
Amesema kuwa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam kwa kushirikiana na mamlaka zingine za kisheria baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa siku za nyuma na baadae kufikishwa mahakamani wamepatikana na hatia akiwemo Derick Kiyagoka
(32) Mkazi wa Kitunda Kati aliyehukumiwa miaka 30 jela na Mahakama ya Kinyerezi kwa kosa la Kubaka .
Pia Mahakama ya Wilaya Kinyerezi ilimkuta na hatia Saidi Kambi (49) mkazi wa Mbagala kwa kosa la kubaka na kulawiti ambae alihukumiwa kifungo cha maisha jela huku Saidi Abdallah (33) alihukumiwa 23/01/2017 kutumikia kifungo cha maisha jela kwa kosa la kulawiti baada ya kufikishwa
kwenye mahakama ya Wilaya Kinondoni
Hata hivyo, Ayubu Saidi pia alihukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa Unyanganyi wa kutumia silaha kwenye mahakama ya Wilaya Kinondoni.
Aidha, katika kupambana na vitendo vya uhalifu Jeshi la Polisi mwezi Oktoba 2024 kwa tuhuma mbalimbali za kujihusisha na vitendo vya kihalifu, tarehe 29 Oktoba 2024 ambapo limewakamata jumla ya watuhumiwa 47 kwa nyakati tofauti, huku likiwapngeza wananchi Kwa kutoa ushirikiano wanapohitajika kutoa ushahidi jambo ambalo linawarahisishia wao kufanya kazi ya uchunguzi kwa wakati.
Amesema kuwa, kati ya watuhumiwa 47, julma ya watuhumiwa 22 walikamatwa kwa kujihusisha na kusafirisha, kuuza na kutumia dawa za kulevya ikiwemo bangi, pia wamekamatwa watu 10 kwa
tuhuma za kujihusisha na uvunjaji wa nyumba mchana na usiku baadae
kuiba.
Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi lao
ikiwa ni pamoja na kuimarisha mifumo ya ulinzi shirikishi ili kuziba mianya
ambayo wahalifu wanaweza kutumia kutenda uhalifu.
Comments
Post a Comment