ACT WAZALENDO YAISHAURI SERIKALI KUSHUSHA GHARAMA YA NISHATI MBADALA

Na Mwandishi wetu, HPMedia 

Chama cha ACT wazalendo kimeishauri serikali kuangalia namna bora ya kusaidia wananchi  wanaoshindwa kumudu gharama za kununua nishati mbadala ikiwemo gesi ili kusaidia uharibufu wa Mazingira.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Waziri Kivuli chama cha ACT Wazalendo Is-haka Mchinjita wakati akichambua bajeti iliyosomwa Jana Bungeni na Waziri wa Nishati January Makamba wameona katika kutekeleza hilo Serikali imetenga Shilingi bilioni 10 ruzuku ya  mitungi ya gesi na vifaa zaidi ya 200,000 Vijijini ili watumiw nishati mabadala ya kupikia na kusaidia kupunguza uharibifu wa Mazingira.

"Serikali imekuwa kwenye mpango wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia (Clean cooking) ambayo ni rafiki wa Mazingira na afya ya mwanadamu na inakadiriwa kwamba kila mwaka hekari milioni moja ya mita inakatwa kwa matumizi ya mkaa na Kuni na tayati matamko yametolewa yakisisitiza taasisinza umma na binafsi kusitisha matumizi ya kuni na mkaa ifikapo 31 mwaka 2025" amesema Mchinjita

Sanjari na hayo amesema Serikali ifanyie kazi mapendekezo yanayotolewa bei ya gesi ya Shirika la maendeleo la petroli Tanzane inawezwa kupunguzwa kutoka Dola za Marekani 5.19 kwa mmBTU hadi 4.359 hiyo itasaidia kupunguza gharama kwani TPDC ingewezekana wenyewe ndiyo mauzo yao yawe chini kuliko Mkampuni mengine 

Manjita akizungumzia kuhusu suala la umeme ameshauri Serikali iangalie sana suala hilo kwa jicho la tatu kwani Vijivini maeneo mengi hawajafikiwa na Umeme hivyo wanaishi katika Mazingira magumu na gharama ya kuingiza umeme majumbani mwao hivyo bei iangaliwe ili vijiji vyote vifikiwe na umeme ili kusaidia Shughuli za Kiuchumi zifanyikwe kwa wepesi

Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI