SELEMANI AGAI ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUTOA LUGHA ZA MATUSI




Na Mwandishi wetu,  HPMedia Dar 

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata na linamuhoji kwa kina Selemani Agai Gaya (18) mkazi wa Kigamboni, kwa tuhuma za kutoa lugha ya matusi mtandaoni dhidi ya Viongozi wakuu wa Serikali  Tanzania kwa kutumia mitandao wa kijamii wa Tiktok.

Mtuhumiwa huyo amekamatwa Julai 29, mwaka huu na wenzake  wakitengeneza maudhui za mtandaoni (video) na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii zenye kuwatukana na kuwafedhehesha  viongozi wakuu wa Serikali katika akaunti zao za mtandao wa kijamii.

Akizungumza  na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam mapema leo Agosti 1 Kamanda wa Kanda Maalumu  ya Dar es salaam SACP Muliro Jumanne amesema  
Jeshi la Polisi linatoa onyo kali kwa mtu au watu wanaotoa lugha za matusi na fedheha kwa Viongozi wa Serikali kwa njia ya mtandao na njia nyingine yoyote.

Amesema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Mamlaka nyingine za kisheria wamejipanga kuwafuatilia na kuwakamata, kuwahoji kwa kina kuhakikisha wanafikishwa haraka kwenye nyombo vya sheria. 

Katika hatua nyingine, SACP Jumanne amesema Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam  Julai 31, mwaka huu  limewakamata watuhumiwa saba  akiwemo Amani Kipolo mkazi wa Vingunguti kwa tuhuma za kumshambulia na kusababishia kifo Hadija Hamisi na kuwajeruhi watu wengine nane (8).
 
Amesema Watuhumiwa hao wakiwa na wenzao wakiwa kwenye kundi waliwashambulia wananchi mtaani maeneo ya Vingunguti kwa lengo la kulipiza kisasi wakati wakitoka kuzimka mwenzao aliyefahamika kwa jina la Nurdin Bwino. 

Aidha, amesema  awali marehemu huyo Nurdin Bwino aliuwa kwa kushambuliwa na wananchi alipokuwa na wenzake sita wakiwa na visu na vifaa mbalimbali vya kuvunjia alipojaribu kuvunja nyumba moja usiku wa Julai 30, 2023. 

Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI