IET NOV 30 KUANZA KONGAMANO

Na Mwandishi wetu, Dar 

Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET) inatarajia kufanya kongamano kubwa la 32 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa .

 Aidha, IET inawakaribisha wahandisi na wadau wote wa sekta mbalimbali za uchumi nchini kwenda kushiriki kwenye kongamano hilo muhimu ambalo litahudhuriwa na washiriki zaid ya 1000.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Rais wa Taasisi hiyo, Eng Mgema Mudo amesema kuwa, kongamano hilo litafanyika tareh 30 mwezi wa 11 hadi tarehe 2 mwezi wa 12 mwaka 2023 katika ukumbi wa kimataifa Arusha (AICC) jijini Arusha .

Aidha amesema kuwa, miongoni mwa watu watakaoshiriki ni mafundi, wahandisi, wanafunzi na wadau wengine kutoka mikoa mbalimbali nchini na nje ya nchi watashiriki kongamano hilo muhimu ambapo wengine watashiriki kwa njia ya mitandao.

Aidha, amesema kuwa miongoni mwa mada zitajazojadiliwa ni pamoja na kutoa elimu ya ubunifu na zinalenga kuhimiza na kuchochea ari ya kuondoa  dhana ya ufanyaji kazi kwa mazoea na kusisitiza kuzingatia ubunifu, umakini, ufanisi na weledi pamoja na uwajibikaji.

"Tunapaswa kufahamu kuwa utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya maendeleo unahitaji sio tu kukuza ujuzi na maarifa katika uhandisi bali pia kukuza kiwango na uwezo wa ubunifu  wa kisayansi na teknolojia na ujuzi nyengine karne ya 21, zikiwemo nidhamu, umakini, ufanisi, uwezo, juhudi na weledi"amesema Eng Mgema.

Hata hivyo, amesema katika kila nyanja Ili kuboresha au kuibua suluhu mpya katika utekelezaji wa kazi mbalimbali za kihandisi ambpo hiyo itafungua njia katika safari ya kufikia maendeleo endelevu na kuifanya Tanzania kuwa mshindi katika ngazi za kikanda na kimataifa.


Aidha, amesema kuwa, taasisi hiyo ina malengo ya kufungua matawi katika mikoa yote nchini ili kuongeza wigo na ushiriki wa wahandisi katika katika kutekeleza dira na dhamira ya taasisi hiyo.


Kwa upande wake, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji IET Eng Upendo Haule amewataka wahandisi wazama kujitokeza kwa wingi kushindania zabuni zinapotangazwa ili kuweza kufanya kazi kwa uadilifu na kuonesha uwezo wao.

Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI